Wema Sepetu: Natumia TZS Milioni 1.2 kwa wiki kwa ajili ya nywele zangu

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Msanii wa filamu, Wema Sepetu, ameweka wazi kwamba hutumia shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya kutengeneza nywele zake kwa wiki moja.

Pia hutumia Sh 30,000 ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Wema aliliambia gazeti la Mtanzania kwamba si kila wakati hutumia kiasi hicho cha fedha, bali hutegemeana na aina ya nywele anazotengeneza.

Alifafanua zaidi kwamba gharama hizo pia zinatokana na kutumia ‘weaving original’ lakini wakati mwingine hutumia hadi laki moja na nusu kwa nywele za kawaida kama rasta.

“Huwa nabadilisha nywele kila baada ya wiki ambapo siku nyingine natumia milioni moja, siku nyingine laki saba au tano kwa sababu sipendi kukaa na nywele muda mrefu na nywele zangu ni ‘orijino’,” alisema.

Wema aliongeza kwamba anachopenda zaidi kwake ni kuwa na muonekano mzuri wa urembo kwa kuwa urembo upo kwenye damu yake.

 
kiiruuuu mpenda kiki katika ubora wake....kwa pedeshee yupi uyo ndani ya serekali hii...
 



Nini chanzo cha mapato yake???
 
Hili swali linanigombanishaga na wife. Labda wanamaanisha ni nywele za watu kabisa.

Siku hizi ameshajua akiweka weaving kichwani sina comment yoyote zaidi ya hujapendeza, kwa hiyo inabidi asiniulize tu kama amependeza au la!

Ugomvi wangu uko kwenye neno 'weaving'.

Hayo madubwasha hayaitwi hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…