Wema Sepetu: Natumia TZS Milioni 1.2 kwa wiki kwa ajili ya nywele zangu

"Weaving " ni nomino?

Mkuu mbona nishatolea ufafanuzi hili...Okay...Sisi tusiojua kizungu tumezoea kuita hivyo tu tukiwa tunamaanisha "Weaving hair" au just "Weave"....Ukitaka kuwa kifimbo cheza utapata tabu sana mkuu maana hata hicho kiswahili tu hatukiongei kwa ufasaha wake...As long as tunaelewana haina haja ya kufanya maisha yakawa magumu
 
kuna mtu mmoja humu ndani alishawahi sema mara nyingi matumizi yanapozidi uwezo mwili lazima utumike tuu.hivyo hata si mshangai huyu mwanamke na haya matumizi aliyoorodhesha
I love your Avatar!
Nywele za mil 1.2 kwa wiki! Huna hata nyumba unayomiliki? Kwa biashara gani anayoifanya, hizo lipstic tu au kuna jingine! Huyu Madame wao sijawahi kumuelewa. Anatafuta kick za kipuuzi mno...ningekuwa mimi ndo yeye ningekuwa mbali sana sasa hivi. Anyway..ni maisha aliyoyachagua yeye mwenyewe!
 
Me mkewangu alikua akiweka minywele hiyo hata kama tulitaka kwenda out naahirisha....sasa hivi haweki tena.
Mkuu Kila wakati huwa nagombana Sana na mtarajiwa Wangu kisa kuweka makolokolo kama hayo anaishia kulalama na kusema ukurya Wangu sio kumbe tupo wengi simtaki mwanamke wa kuweka makolokolo kama hayo afu Cost ndefu.
Back to the topic Dada angu Wema. C . Sepetu Hongera Sana kwa matumizi yako mi nadhani Ongeza tena mi naona Kila siku uwe unatumia Milioni Kumi Tsh 10,000,000/ = As your daily expenditures Mi one mil and point sioni kama Ni pesa Kwa Mtu Kama wewe .
Shiit.
 
'Weaving original' ndo nini?

kama ushaskia msemo mmoja unasema ukimloga binti kwa kukata nywele zake unaweza shangaa kuna kiwanda china kinaungua au kuna dada uko india/brazil kawa kichaa.
nahisi ni weave/wig la nywele halisi za mtu mwingine.
 
kama ushaskia msemo mmoja unasema ukimloga binti kwa kukata nywele zake unaweza shangaa kuna kiwanda china kinaungua au kuna dada uko india/brazil kawa kichaa.
nahisi ni weave/wig la nywele halisi za mtu mwingine.

Ni weave kama ulivyosema. Sasa sijui kwa nini watu husema weaving....
 
Weaving za nywele halisi za binaadam na sio plastics

Duu akina dada wametufikisha katika daraja la juu la kumkufuru aliyetuumba! yaani nywele alizokujalia Mola wako alizozikadiria kwa umakini usio na shaka! leo wasichana wetu wanazikana kuwa si kitu chochote bali kwao wanataka nywele za singa kama za mabaniani!!! Kama umamboleo wenyewe ndio kama hivyo basi kiama hakipo mbali...Tujiandae kukabiliana na hukumu ya haki!
 
Huyu dada anamtaji mkubwa sana.lile wezere la kichina linavutia wawekezaji wakubwa wakubwa tu....
 
Kipilipili noma mkuu.
 
I wish ningekua PA wake nimkombe hela. 1.2M kichwa tu hapo bado shopping. Ueke original feki km mbaya mbaya tu. Idris anakonda n mengi masikini
 
Atuondokee hapa na sifa zisizo na tija. Niliwahi kuwakuta American Nails salon, ndiko wanakoenda mara nyingi, pamoja na kidoti, ana deni la 1.8m na mwenye laki 7. akapunguza laki 3 mwenzie akasema atakuja kupunguza siku nyingine.
nilibaki nashangaa. star mzima unakopa mpaka zaidi ya 1m kwa ajili ya urembo...?? hicho kumbwa elf 50 kwa wiki kinakula nini? Usanii mpaka kwenye maisha yao ya kila siku.
 
Kama ana pesa kiasi hiko mbona Range limepigwa mnada.
 
Miss Tanzania 2006, Wema Isaack Sepetu, ameweka wazi kwamba hutumia shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya kutengeneza nywele zake kwa wiki moja.

Pia hutumia Sh 30,000 ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Hata hivyo, Wema amesema si kila wakati hutumia kiasi hicho cha fedha, bali hutegemeana na aina ya nywele anazotengeneza.

Alifafanua zaidi kwamba gharama hizo pia zinatokana na kutumia ‘weaving original’ lakini wakati mwingine hutumia hadi laki moja na nusu kwa nywele za kawaida kama rasta.

“Huwa nabadilisha nywele kila baada ya wiki ambapo siku nyingine natumia milioni moja, siku nyingine laki saba au tano kwa sababu sipendi kukaa na nywele muda mrefu na nywele zangu ni ‘orijino’,” alisema.

Wema aliongeza kwamba anachopenda zaidi kwake ni kuwa na muonekano mzuri wa urembo kwa kuwa urembo upo kwenye damu yake.
 
Maisha ya mwanadamu hapa duniani ni
sawa na msafiri aliyepumzika kivulini huku
akivuta muda wa kuendelea na safari
yake.....
Vifo vya wapendwa wetu ni moja ya matukio
yenye kuumiza lakini vinatakiwa vitupe
fundisho kuwa duniani tunapita...wanadamu
yatupaswa tuishi kwa upendo kwani hakuna
ajuaye muda wala saa ya kunyakuliwa
kwake.........
 
Kama ana pesa kiasi hiko mbona Range limepigwa mnada.
Labda kanunua nyingine
 
Hakuna umaskini mbaya kwa mwanamke kama kutokuwa na nywele nzuri za asili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…