Wema Sepetu: Natumia TZS Milioni 1.2 kwa wiki kwa ajili ya nywele zangu

Wema Sepetu: Natumia TZS Milioni 1.2 kwa wiki kwa ajili ya nywele zangu

Msanii wa filamu, Wema Sepetu, ameweka wazi kwamba hutumia shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya kutengeneza nywele zake kwa wiki moja.

Pia hutumia Sh 30,000 ya chakula kwa siku na kama atanunua na chakula cha mbwa wake huwa anatumia Sh 50,000 kwa siku.

Wema aliliambia gazeti la Mtanzania kwamba si kila wakati hutumia kiasi hicho cha fedha, bali hutegemeana na aina ya nywele anazotengeneza.

Alifafanua zaidi kwamba gharama hizo pia zinatokana na kutumia ‘weaving original’ lakini wakati mwingine hutumia hadi laki moja na nusu kwa nywele za kawaida kama rasta.

“Huwa nabadilisha nywele kila baada ya wiki ambapo siku nyingine natumia milioni moja, siku nyingine laki saba au tano kwa sababu sipendi kukaa na nywele muda mrefu na nywele zangu ni ‘orijino’,” alisema.

Wema aliongeza kwamba anachopenda zaidi kwake ni kuwa na muonekano mzuri wa urembo kwa kuwa urembo upo kwenye damu yake.

View attachment 351363
Hivyo hizo filamu za bongo movies zinalipa kiasi hiki? Kweli kuna umuhimu wa kuwa na mtoto, sasa nywele ndio zimekuwa ndio maisha. I feel for her.
 
Kuna jamaa aliniambia kisa kimoja kuhusu wanawake, kuwa anaweza hongwa laki moja, na hela yote akaitumia katika kuinunulia maurembo ili aonekane yuko juu zaidi. Wanaume wamuone ni wanawake wacheche wanaohongwa hela hizo wakazielekeza kwenye maendeleo ili siku moja aondokane na kuwatunga wanaume kwenye cheni, na ajitegemee.
 
Mi hata sijuagi maana siyapendi kama nini, bora mtu usuke rasta tu basi.

Halafu unakuta wengine wana nywele nyingi na nzuri tu.
Huyapendi au waogopa gharama za kumnunulia wife mana yenye quality ni expensive
 
Doooh, ntohooo. 1.2M per week? Hatari. Yan mbwa wake anatumia mipunga mingi kwa siku kuliko hata bili yangu ya msosi kwa mama Caro.
 
Huyapendi au waogopa gharama za kumnunulia wife mana yenye quality ni expensive

Yaani akiwa nayo kichwani hata pa kushika hakuna, ukisema ukune kichwa unakutana na uzi uzi, ndo maana napendaga awe hivyo hivyo au asuke rasta.

Otherwise nakuwa limited pa kudhika aisee.
 
Afu augue tuanze kuombana michango ya matibabu India, hakiyanani jibu nitakolompa huyo mchangishaji atatamani ardhi ipasuke au awe ndani ya ndege afu ipotee angani.
Hawezi omba mchango mtu mwenye baby anayeplan kununua. Ndege binafsi in this year, idd anapesa weww
 
View attachment 351380 View attachment 351380 View attachment 351381
kwa nywele zipi labda alizonazo hizi hahahahahahahahaha akawadanganye makwao unyaturuni
3ba450d39b84771b0e93ad1a6cc9e973.jpg
 
Na gharama za kujaza upepo makalio kwa wiki bei gani?
 
Fahari eeh ndio mama wa ujinga...!!! Ingekuwa ni kweli asingeiba umeme na maji
 
"Nywele zangu ni originall
What a hell?
Nywele za marehemu huko India na China,Israel wakifa zinakatwa unakuja unashinea alafu unasema ni nywele original?/Halisi?

Hizo ni nywele bandia toleo la kwanza!

Nywele original ni ile ulozaliwa nayo tu!Hata kama ni kipilipili cha aina gani,ama rangi yake ugongo ,kahawia kwa kula chips na kukosa virutubisho lakini ni zako!
 
Back
Top Bottom