Wema Sepetu: Sijawahi ku-cheat maishani mwangu, ni kitu kinachochosha sana

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Muigizaji na mfanyabiashara mashuhuri nchini Tanzania, Wema Sepetu, amezua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka wazi kuwa hajawahi kusaliti mpenzi wake yeyote tangu anaanza mahusiano ya kimapenzi.

Wema alibainisha ukweli huo Alhamisi kupitia ujumbe mfupi aliochapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, ikiwa ni sehemu ya kushirikisha mashabiki zake hisia na mtazamo wake kuhusu masuala ya mahusiano.

Akieleza sababu za kushindwa kufanya kitendo hicho, mshindi huyo wa taji la Miss Tanzania 2006 alisema mchakato mzima wa kuchepuka unachosha akili na mwili (draining) kiasi kwamba ameshindwa kabisa kujiingiza kwenye tabia hiyo.

"Kitu nimeshindwaga kufanya maishani ni kucheat... Kwanza its draining balaa..." aliandika Wema kwenye ujumbe huo uliosambaa kwa kasi.

Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na watumiaji wa mitandao ya kijamii; huku wengi wakimpongeza kwa uaminifu na uwazi wake, wengine wameonyesha mashaka kutokana na historia ya mahusiano yake ya nyuma iliyowahi kugubikwa na drama mbalimbali.
1789653780818.png
 
Hahaha kwanza alijuaje it's draining ilihali Hana experience. Diamond alipigwa na kitu kizito kwenye birthday ya wema yeye anapeleka maua akakuta Kuna mwamba amepeleka ndinga ya gharama. Diamond kujifanya kibesi akaambiwa hata hiyo party yenyewe ipo sponsored na huyo mwamba.
 
Hahaha kwanza alijuaje it's draining ilihali Hana experience. Diamond alipigwa na kitu kizito kwenye birthday ya wema yeye anapekeka maua akakuta Kuna mwamba amepeleka ndinga ya gharama. Diamond kujifanya kibesi akaambiwa hata hiyo party wenyewe ipo sponsored na huyo mwamba.
Aaahaaa,kwahiyo Simba alikutana na kiboko yake
 
Muigizaji na mfanyabiashara mashuhuri nchini Tanzania, Wema Sepetu, amezua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuweka wazi kuwa hajawahi kusaliti mpenzi wake yeyote tangu anaanza mahusiano ya kimapenzi.

Wema alibainisha ukweli huo Alhamisi kupitia ujumbe mfupi aliochapisha kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, ikiwa ni sehemu ya kushirikisha mashabiki zake hisia na mtazamo wake kuhusu masuala ya mahusiano.

Akieleza sababu za kushindwa kufanya kitendo hicho, mshindi huyo wa taji la Miss Tanzania 2006 alisema mchakato mzima wa kuchepuka unachosha akili na mwili (draining) kiasi kwamba ameshindwa kabisa kujiingiza kwenye tabia hiyo.

"Kitu nimeshindwaga kufanya maishani ni kucheat... Kwanza its draining balaa..." aliandika Wema kwenye ujumbe huo uliosambaa kwa kasi.

Kauli hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na watumiaji wa mitandao ya kijamii; huku wengi wakimpongeza kwa uaminifu na uwazi wake, wengine wameonyesha mashaka kutokana na historia ya mahusiano yake ya nyuma iliyowahi kugubikwa na drama mbalimbali.
View attachment 3672624
SWALI
Alijuaje kwamba 'cheating' ina chosha /draining balaa?
 
Back
Top Bottom