Wema Sepetu: Sina amani kabisa kwenye maisha yangu

Wema Sepetu: Sina amani kabisa kwenye maisha yangu

Mchumba

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
280
Reaction score
262
wema-seoetu24-1.jpg


Msanii wa filamu na mjasiriamali Wema Sepetu amefunguka ya moyoni kutokana na namna mashabiki wake wa mitandaoni wanavyomchukulia na kumpa maneno ambayo muda mwingine yanamuumiza na kumkosesha amani na kumfanya ajione ni kama mkosaji mkubwa.

“Kitu ambacho nakiona kutoka mitandaoni, Watu wanapenda sana fujo fujo, Purukushani, mara huyu na huyu hawaongei, flani kamchukulia flani bwana, yule kafumaniwa.

Hicho ndiyo mnachokiona kina kick. Ila mwisho wa siku ukija kuangalia , ni kweli maana dunia ya leo umbea unauza. Ila jamani ifike muda tukue mimi binafsi kuna vitu vinanichosha actually vimenichosha ifike muda kila mtu aangalie maisha yake na afanye kile kinachomridhisha nafsi yake. kwangu naangalia wat God has to say bout wat im doin… Imekuwa too much tokea nilivyopost uzalendo ikaonekana all sorts of Crazy, But u know wat, I dont care” aliandika Wema Sepetu

“Sasa basi, nitapost ninachotaka nyinyi endeleeni kujudge na kuleta conclusion zenu mnazojua… Iwe nataka attention, iwe natafuta kick, iwe nitokeje, iwe najipendekeza, iwe vyovyote It all comes down to me. Kuna msemo unasemaga tenda Wema uende zako… Dats how I roll.

Na nimekuwa nikifanya hivyo siku zote. Sitegemei na wala sitaki mtu ninae msupport au kumuunga mkono na yeye afanye the same na wala sina haja na kupostiwa. Niwe sipindui au napindua It doesnt make A difference.

Kwanza haya mambo ya kupinduana yameanzaga lini Mungu wangu. Ila instagram mna majungu sana. Mimi siwezi jamani mniachage basi sometimes, sina amani imekuwa kama nimeua” aliongeza Wema Sepetu

Source: EATV
 
Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua!!
Hayo ndio maisha aliyoyachagua, kuishi kimjini mjini, ujanja ujanja, kuendesha maisha kwa matukio!! So inapotokea mda mambo yana back fire, asilalame, atulie tu!! Hayo ndio maisha yake na hakuna aliyemchagulia zaidi ya yeye mwenyewe..
 
Mtu mwenyewe fake hiyo amani ataipata vipi, mwambieni awe real(OG)
 
Amesahau alivyotangazia dunia amenunua nyumba kwa mil400, wizi wa umeme na maji ukafichua siri kuwa sio kwake. Kasahau alitangaza ameolewa tena redion anahojiwa na Millard. Juzi katangaza ana mimba baada ya siku nne tunamsikia analia mimba imetoka. Kati ya star atakaejuta kwa kutolitumia jina lake vizuri ni Wema.
 
Amesahau alivyotangazia dunia amenunua nyumba kwa mil400, wizi wa umeme na maji ukafichua siri kuwa sio kwake. Kasahau alitangaza ameolewa tena redion anahojiwa na Millard. Juzi katangaza ana mimba baada ya siku nne tunamsikia analia mimba imetoka. Kati ya star atakaejuta kwa kutolitumia jina lake vizuri ni Wema.
Anayakoroga mwenyewe alafu kuyanywa anaona machungu!!
Alivyohongwa range mwenyewe akaongea kwa nyodo kabisa eti hawezi kuendesha vigari vya elfu thethini.. Hahaaahahh
 
Walichagua kuishi Maisha fake sasa Kila kitu kitakuja kwa style ya Maisha waliyochagua, mbona wapo watu maarufu kibao na wanapesa zao wanaishi Maisha halisi hawayapati kama hayo!?
 
Si mumuache binti wa watu,inawahusu nini awe fake au original,ananijua mwenyewe
 
sasa ugumu upo wapi hapo, si afute account zake zote mtandaoni, awe kama jigga tu, au ndo mojawapo ya kiki hiyo?
Umeongea ukweli kabisa,kama ni kweli hana amani kabisa NI KUFUTA ACCOUNT ZOTE ZINAZOMUHUSU.
 
Atoke ktk hio mitandao ya kijamii inayomkosesha amani na furaha
 
Back
Top Bottom