SoC03 Wema unadumu

SoC03 Wema unadumu

Stories of Change - 2023 Competition

saadala muaza

Member
Joined
May 12, 2023
Posts
38
Reaction score
38
WEMA UNADUMU

Mwandishi:Saadala Muaza

Hapo zamani kulikuwepo na kijana ambaye alipata riziki yake kwa kuuza mchicha mlango baada ya mlango.Na hivyo ndivyo alivyoweza kupata fedha kwa ajili ya kulipia ada yake ya shule na matumizi mengine madogo madogo.

Siku moja akiwa katika shughuli zake za kila siku kama kawaida yake.Ghafla njaa ilimshika,mwili ukawa ukimtetemeka na kumfanya ahisi huenda akadondoka na kushindwa kuendelea na safari yake hivyo akajikaza na kusogea katika nyumba moja iliyokuwa karibu nae.

Alipofika katika nyumba ile akabisha hodi na binti mmoja mrembo mwenye umri wa lika lake akatoka na kusimama mlangoni ili kumsikiliza."Naomba unisaidie maji ya kunywa tafadhali" kwa sauti ya unyonge na yenye kuonesha ni kwa namna gani kijana yule alikuwa na njaa aliomba msaada kwa binti yule ambaye baada tu ya tukio hili aligundua ni kwa kiasi gani kijana huyu alikuwa na njaa.

Basi yule binti aliingia ndani na baada ya dakika moja alirudi nje kwa yule kijana akiwa na bilauri kuubwa mkononi na kisha akampatia kijana yule.kija ambaye hakuweza kugundua kuwa kulikuwa na kitu tofauti na kile alichokiomba katika bilauri ile.Ndio kulikuwa na maziwa tena maziwa yaliyojaa pomoni katika kikombe.Yule kijana akanywa maziwa yale na baada ya kumaliza akamuuliza binti yule "je nikulipe kwa kitu gani juu ya huu wema ulionitendeaaa?" Yule binti akamjibu "shukrani yako tu inatosha"

Baada ya miaka mingi kupita binti yule akapatwa na maradhi.Maradhi amabayo yalimfanya binti huyu ateseke kwa muongo mzima bila kupata matibabu yaliyomsaidia.Wazazi wake na binti huyu wakaamua kumchukua binti yao na kumpeleka hospitali aliyopatikana mbali kidogo na kijiji chao kwa ajili ya kujaribu matibabu zaidi.

Katika hospitali ile kulipatika daktari mmoja ambaye ndiye alikuwa daktar bingwa kwa maradhi kama yale.Baada ya matibabu ya miezi kadhaa hatimaye binti yule alipona maradhi yake lakini akajawa na khofu kubwa na namna gani ataweza kulilipa deni lile kubwa pale hospitali.Kwakuwa hakukuwa na lingine la kufanya ikambidi binti yule aende akachukue bili yake pale mapokezi.

Ilikuwa ni mshangao mkubwa sana kwake baada kukuta karatasi iliyoandikwa.
"Bili yako ililipwa miaka mingi iliyopita kwa kikombe cha maziwa. Ni mimi daktari wako Saadala."
 
Upvote 2
Back
Top Bottom