Wenger muache Alexis Sanchez aende zake , anadhalilisha timu

Wenger muache Alexis Sanchez aende zake , anadhalilisha timu

Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha!

Kwa kweli hata mimi nashangaa imekuaje mpaka sasa Alexis Na Ozil wapo Arsenal. Hawastahili kuwa pale.
Si ndio mkuu ..asepe zake tuu anapoteza time palee
 
Yaani watu bhana. Ukishashiba dona na kuungiwa kifurushi na mjomba basi unaandika lolote tu unalojisikia. Unawezaje kumtuhumu mtu bila kuainisha makosa hayo. Dharau zipi unazozizungumzia au tabia zip za kishamba unazozizungumzia?? After all kama ni suala la malipo ile ni kazi yake na anapaswa kuelezea mahitaji yake pia. Maana hata nje ya soka ana maisha mengine pia. He needs to pay bills na pia umri wake ktk soka la ushindani hauna maisha marefu kihivyo. Je anaiandaa vipi kesho yake?? Asijeishia kuwa kapuku kama akina George Best ingawa yeye sana sana aliathiriwa na ulevi na starehe zilizopitiliza.
[HASHTAG]#Tunasemajeeee[/HASHTAG].....
Even if Alexis demands the the palace to stay THE QUEEN HAS TO GO!! [emoji1] [emoji1]
Usisubiri kutafuniwa kila kitu , suala hapa si mshahara , umepewa tip , hebu jiongeze mwenyewe .
 
Mlimuuza Chogo Henry. Vierra. Clinchy. Song. Fabregas. Van magoli. Sembuse huyu. mlishazoea hamtaki mchezaji ghali. akina pogba hamuwawezi nyie.
 
Mpira ni kazi yake, na kipindi cha kucheza ni kifupi sana hakizidi miaka 10 tu mwache akusanye pesa Ndio wakat wake, kama arsenal hamna uwezo mwacheni aondoke tu hakuna namna
 
Wenger aache ubahiri wake. Ni kweli wameondoka wengi wazuri kwa sababu ya ubahiri na matokeo yake mnayajua. No trophy for many many years.
 
Kama wewe ni mfuatiliaji wa soka na unafuatilia mechi za Arsenal hivi karibuni , basi bila shaka utakumbana na tabia za Kishamba kabisa zinazoonyeshwa na Sanchez .

Ni mchezaji anayejiona ni bora kuliko yoyote ndani ya kikosi chake , na anadhani ni bora kuliko hata kocha wake ! Ni mchezaji ambaye anamdharau kila mchezaji wa timu yake , sijui ni nani kamdanganya ?

Kwa manufaa ya timu ni heri huyu mchezaji aruhusiwe kuondoka kwenda china kama anavyotaka , Arsenal itabaki kama ilivyobaki walipoondoka wengine wakali kuliko huyu .

Ni ushauri tu .
Aende tutavumilia kutopata makombe,mbona Liverpool wanaweza
 
Unaongea nn wewe? Sanchez aondoke ili iweje. Hiv unajaribu kumfananisha na nani pale arsenal.
Unamuona Ronaldo? Unaona nyodo zake? Umewahi kuona siku akitolewa? Na mbona hauzwi. Timu haifanyi vzr kwa sbb inashindwa kuwabakisha ma star kama huyu Sanchez. Kama akiondoka basi arsenal inaanza upya. Hakuna mchezaji wa kariba ya sanchez ambae anapenda kuendelea kulipwa pesa kiduchu. Soka la sasa sio la ridhaa tena na watu hawachez kwa kuipenda timu kama Ngasa. Sahau kuhusu china Sanchez kwa sasa anaweza kwenda timu yoyote kubwa na akalipwa pesa ndefu tu. Kitu muhimu ni Wenger kuacha ubahil na kumpa pesa nyingi ili asalie Arsenal.
 
Alipokuwa Barcelona alikuwa analipwa £40,000 kwa wiki kumbuka!
Unajaribu kumlinganisha Sanchez wa barcelona na huyu wa sasa?
Au unataka kusema kuwa anapaswa kulipwa pesa zile zile licha ya kupandisha kiwango chake?
Sanchez huyu wa sasa anapaswa kulipwa pesa ndefu kwa sbb ana kila kitu ambacho unaweza kuhitaji kwa mchezaji wa nafasi yake.
 
Usisubiri kutafuniwa kila kitu , suala hapa si mshahara , umepewa tip , hebu jiongeze mwenyewe .
Hiki ndicho minachokikataa kumtuhumu mtu pasi na ushahidi. Mimi no mfuatiliaji sana wa mambo hususani yanayoihusu klabu yangu pendwa ya Arsenal. Ndio maana hapa naona unaandika porojo tu. Ndo maana ht juzi DT alikwambia "anyone who says Alexis is not happy at Arsenal has to f*...

Hapana shaka km u mpenzi na mfuatiliaji utanielewa
Usisubiri kutafuniwa kila kitu , suala hapa si mshahara , umepewa tip , hebu jiongeze mwenyewe .
Hiki ndicho minachokikataa kumtuhumu mtu pasi na ushahidi. Mimi no mfuatiliaji sana wa mambo hususani yanayoihusu klabu yangu pendwa ya Arsenal. Ndio maana hapa naona unaandika porojo tu
 
Mkuu Muombe Radhi Erythrocyte Kwani Ni Mdau Wetu Wa JF kwa Siku Nyingi.... Si Busara Kumwita Hivyo.....
Mkuu hapa issue sio kaandika nani, issue ni kaandika nini.... Angekuwa kaandika cha maana ama kuleta uthibitisho wa akisemacho nisingethubutu kumpinga. Au basi angesema tu kwa maoni yake Alexis aachwe aondoke sawa. lkn sio kujaribu kutuaminisha uongo.
 
Kama wewe ni mfuatiliaji wa soka na unafuatilia mechi za Arsenal hivi karibuni , basi bila shaka utakumbana na tabia za Kishamba kabisa zinazoonyeshwa na Sanchez .

Ni mchezaji anayejiona ni bora kuliko yoyote ndani ya kikosi chake , na anadhani ni bora kuliko hata kocha wake ! Ni mchezaji ambaye anamdharau kila mchezaji wa timu yake , sijui ni nani kamdanganya ?

Kwa manufaa ya timu ni heri huyu mchezaji aruhusiwe kuondoka kwenda china kama anavyotaka , Arsenal itabaki kama ilivyobaki walipoondoka wengine wakali kuliko huyu .

Ni ushauri tu .
Mkuu Wenger anapitava Jf siku hizi nini?

Ujue Sanchez akiondoka mumekwisha msimu huu mnaweza kushuka daraha.
 
Muacheni aje Chelsea jamani

Sent from my GT-N5100 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom