Mdondoaji said:Vile vile ungeliongezea kuwa viongozi wa dini wangelijiepusha kuonyesha wanakubaliana na viongozi wa chama fulani au itikadi ya chama fulani, kwani waumini wao ni wafuasi wa vyama vyote Tanzania. Hivyo basi lingejenga mazingira ya kuaminiana zaidi.
Mdondoaji,
..true .. true.
..labda kuwa specific ni kwamba wasimuunge mkono mgombea wa chama fulani kwasababu tu ni muumini wa dini yao.
..katika uchaguzi uliopita kulikuwa na wagombea watatu wa Uraisi ambao ama wanajulikana kwa uzinzi, au ndoa zao zilikuwa na mgogoro. tatizo ni kwamba viongozi wa dini moja wakaamua kumshambulia mgombea asiye wa dini yao na "kuwamezea" wale wengine.