Wengi Hawako very SERIOUS humu JF

Wengi Hawako very SERIOUS humu JF

YAHERI MUNGU

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
318
Reaction score
215
Nimekuwa nikipitia posts nyingi humu JF, hasa katika jukwaa la Love Connect, wanawake wengi wanaotafuta wanaume wa kuwaoa, kwa kweli nimegundua kuwa wengi wao hawako very serious na kile ambacho wanakuwa wamekichapisha katika jukwaa hili. Wengi wao kuna kitu flani wanakitafuta Different from Love Affairs. Hivyo, kama kweli mwanamke anakuwa anahitaji mwanaume, please, msiweke jokes nyingi maana kuna wanaume wengine wanakuwa wamedhamilia kuwa na mwanamke, lakini mwanamke mwenyewe anakuwa tofauti na hilo lengo. Hivyo, inaonekana kuwa wengi wanafanya jokes au just writing.
 
Mtoa mada, ukiona hayuko seriously nawe ujue kuna mtu yuko serious naye.
JF ni kijiji chenye watu wengi mno. Hawezi kuwa serious kwa wote.
Ipo siku yako utapata aliye serious kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usijali sana mkuu. chukulia maisha rahisi!

Ukiona hivyo ujue ni wewe hujapata umpendae wa kukidhi vigezo vyako. Wako wanaume wengine wanapenda hao hao ambao hawako serious kama unavyotaka wewe...na maisha yanaendelea.

Cheers.
 
Mleta mada umechezea cha mbavu nini?
Siyo kuwa nimechezea cha mpavu! Nimejaribu kuwa ninasoma POSTS zinazochapishwa humu Jf, hasa Love Connect, na nimegundua kuwa wanaokuwa wanachapisha posts ni watu walewale ila wanabadilisha ID zao. Hivyo, naamini kuwa wanawapata wanaume au wanawake halafu pengine unakuta mtu alivyotarajiwa sivyo inavyokuwa. Mimi ni msomaji tu wa POSTS za humu ndani na wala siwezi kutafuta mwanamke kwa njia ya mtandao. Mimi mwanamke wangu tayari ninaye na nimedumu naye kwa muda wa miaka minne na nusu hadi leo. Hivyo, mimi ninawapa ushauri tu maana naona kwa muda mrefu wanaoleta machapisho ni walewale ila kinachobadilika ni IDs zao tu.
 
Upo sahihi kabisa.
 
Jamaa imempain sana naamini wamekupata
 
Jamaa imempain sana naamini wamekupata
Naomba mnielewe vizuri! Mimi sina shida wala sijapost ili kutafuta mwanamke humu wakati huku USWAHILINI WAPO WENGI SANA na ninashinda nao!! Mimi ni msomaji na mchangiaji wa mada zinazoletwa humu ndani ya JF kama ilivyo kwa wasomaji na wachangiaji wengine. Hivyo, kwa muda mrefu unakuta POST na CONTENTS zake ni zilezile ila kinachobadilika ni IDs' tu. Sasa unaweza ukajiuliza swali kuwa "Ni kweli mtu anaweza kuwa anapost humu JF kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja na akawa anakosa tu?" Hili ni jukwaa huru la jamii, hivyo na mimi ninachangia kama walivyo wanajamii wengine na siyo kutafuta mwanamke! Mwanamke tayari ninaye na sikumpata humu, nilimpata kipindi niko mwaka wa kwanza Chuoni.
 
Back
Top Bottom