Wengi wanahoji, kwanini Iran hapigi ndani ya Marekani, Bali anapiga nchi jirani yake?

Nzuri sana hii,nilitamani hata ingekua kwa kiswahili.
Hapa ndio imeelezwa kitaalam zaidi.
 
Sababu ni ndogo tu, Iran to USA ni 10000KM, Unahitaji tekinolojia kubwa ya, ICBM(intercontinental ballistic missile), kufika huo umbali, Iran anazo, ICBM za kilometer 2000 tu, tekinolojia ya long-range ICBM, bado Hana,
Kuna wakati walipiga Khormashar 4 kwenda kisiwa cha Diego Garcia kina umbali wa 4000 KM kwahiyo at least range yao inafika hapo.
 
Sawa umejieleza sana ila kiukw3li iran aache utoto kumpiga marekani kwa makombora ni kujidanganya level ya marekani labda unaweza kumpiga kisaikolojia ila sio makombora wanajlpoteza muda na pesa nyingi bila sababu.
Unazumgumzia makombora?
Marekani alishapigwa kwa AK 47 TU na akakimbia.
Unaposema huwezi kumpiga kwa makombora una maana Yale makambi yaliyopogwa yalikua matoi?
Kwamba kwa sababu ni Marekani hakuna hasara yoyote?
 
Huu ni uvivu wa kufikiri. Kwani Marekani anafanya mashambulizi akitokea North America?
 
Unazumgumzia makombora?
Marekani alishapigwa kwa AK 47 TU na akakimbia.
Unaposema huwezi kumpiga kwa makombora una maana Yale makambi yaliyopogwa yalikua matoi?
Kwamba kwa sababu ni Marekani hakuna hasara yoyote?
Kuna kupiga na kunakujichosha..sasa iran ni kama anajichosha tu..
 
Na wewe iran wa zungu wa jioni toka mbagara
 
Sababu ni ndogo tu, Iran to USA ni 10000KM, Unahitaji tekinolojia kubwa ya, ICBM(intercontinental ballistic missile), kufika huo umbali, Iran anazo, ICBM za kilometer 2000 tu, tekinolojia ya long-range ICBM, bado Hana,
Naifahamu sababu hii,lkn nilijiuliza pia,Urusi na china Zina uwezo wa kupiga popote ndani ya Marekani,nikajiuliza hivi,hivi ikitokea vita kati ya Marekani na Urusi,Urusi haita yashambulia makambi ya Marekani yanayoizunguka Urusi kwanza?
Kumbuka Kuna mamkambi ya Marekani yanayoizunguka Urusi Yana vifaa muhimu sana kuzuia au kupunguza uwezo wa mashambulizi ya Urusi kwenda kwa morekani.
 
Nzuri sana hii,nilitamani hata ingekua kwa kiswahili.
Hapa ndio imeelezwa kitaalam zaidi.
Kosa kubwa ambalo watu wengi hufanya wanapoangalia vita ni kudhani kwamba lengo kuu ni kuipiga mji mkuu wa adui haraka iwezekanavyo. Hiyo ni political theater, siyo military strategy.

Ukiangalia ramani ya mashambulizi (strike map), Iran haionekani kama nchi inayotafuta headlines au propaganda, bali kama jeshi linalojaribu kushape battlespace kabla ya hatua kubwa zaidi za kijeshi.

Malengo yanayoshambuliwa si ya bahati mbaya wala si insignificant. Kinachoonekana ni juhudi za kuvuruga (degrade) mtandao mzima wa miundombinu ya kijeshi ya Marekani katika eneo:

  • Early-warning radar sites (vituo vya rada vya tahadhari ya mapema)
  • Air defense systems (mifumo ya ulinzi wa anga)
  • Aviation facilities na hangars
  • Logistics hubs
  • Fuel na ammunition storage
  • Forward Operating Bases (FOBs)
  • CENTCOM support infrastructure
  • Kambi zinazosaidia operesheni za Marekani Syria na Iraq
  • Naval na maritime surveillance assets
  • Intelligence collection pamoja na communications nodes

Angalia Jordan kama mfano. Watu wengi hata hawawezi kuonyesha Tower 22 au Muwaffaq Salti Air Base kwenye ramani, lakini kwa mtazamo wa kijeshi vinaweza kuwa na umuhimu mkubwa zaidi kuliko kurusha makombora machache katikati ya Tel Aviv.

Tower 22 inaunga mkono operesheni za Al-Tanf.
Muwaffaq Salti Air Base inapokea ndege za Marekani na operesheni za muungano (coalition operations).
Erbil ni kitovu cha intelligence na special operations.
Bahrain ndiyo makao makuu ya U.S. Navy Fifth Fleet. (Hii ndio inasimamia operations za US kwenye Arabian Sea, Gulf of Oman, Persian Gulf, Mediteranean Sea, Strait of Hormuz na sehemu za Indian Ocean mpaka Horn of Afrika na karibu na Kenya)
Kuwait ni kituo kikubwa cha logistics na staging.
Qatar inahifadhi forward headquarters ya CENTCOM pamoja na largest U.S. air base in the Middle East.

Kwa kifupi, hizi ndizo eyes, ears, and connective tissue za uwezo wa Marekani wa power projection katika Mashariki ya Kati.

Kwa mtazamo wa military doctrine, huanzi kwa kuupiga sehemu yenye ulinzi mkubwa zaidi wa adui. Unaanza kwa kumtenga (isolate), kuvuruga mtandao wake wa msaada, na kupunguza uwezo wake wa kupigana.

Hapa kuna kanuni kadhaa za vita (principles of warfare) zinazoonekana kutumika:

1. Suppression of enemy support infrastructure – kudhoofisha miundombinu inayounga mkono operesheni za adui.
2. Degradation of intelligence, surveillance and reconnaissance (ISR) – kupunguza uwezo wa kukusanya taarifa na kufuatilia adui.
3. Attrition of air-defense and interceptor inventories – kupunguza akiba ya makombora ya kujihami na vifaa vya kuyazuia makombora.
4. Disruption of logistics and sustainment – kuvuruga usafirishaji wa vifaa, mafuta na mahitaji ya operesheni.
5. Political pressure on host nations – kuongeza shinikizo kwa nchi (Bahrain, Kuwait, UAE, KSA, Jordan) zinazoruhusu kambi za kijeshi za Marekani.
6. Shaping the operational environment kabla ya kuanzisha operesheni kubwa zaidi.

Marekani haipigani vita vya Mashariki ya Kati kutoka Washington pekee, wala kutoka kwenye aircraft carriers pekee. Inategemea mtandao uliounganishwa wa kambi za kijeshi kutoka Jordan, Qatar, Kuwait hadi Bahrain. Mtandao huo ukianza kudhoofika, kila air sortie, kila intelligence feed, kila resupply mission na kila uzinduzi wa interceptor missile unakuwa mgumu zaidi, wa gharama kubwa zaidi, na usio na ufanisi.

Wale wanaopiga kelele wakisema “piga Tel Aviv tu” wanaonyesha kutokuelewa namna modern warfare inavyofanyika. Kijeshi, kuharibu radar inayowezesha operesheni za anga za muungano kunaweza kuwa na thamani kubwa zaidi kuliko kusababisha uharibifu wa juu juu kwenye eneo lenye symbolic value kama mji mkuu.

Kuna jambo lingine ambalo wengi wanalipuuza: Interceptor Economics.

Kila kombora la Patriot interceptor lina gharama ya mamilioni ya dola. Akiba ya makombora hayo siyo isiyo na mwisho. Operesheni za muda mrefu zinaweka shinikizo kubwa kwa maintenance crews, missile stockpiles na logistics chains. Ikiwa adui anaweza kukulazimisha ulinde maeneo kumi au zaidi kwa wakati mmoja, basi tayari ameanza kushinda vita vya resource allocation.

Kihistoria, kampeni nyingi zilizofanikiwa kijeshi huanza kwa kudhoofisha command-and-control, communications, air defenses, na logistics, kabla ya kuingia kwenye operesheni za maamuzi (decisive operations).

Kama mtu anakubaliana au hakubaliani na Iran kisiasa siyo hoja ya msingi katika uchambuzi huu wa kijeshi. Kinachoonekana si kulipiza kisasi bila mpangilio, bali ni kampeni yenye malengo maalumu ya kudhoofisha hatua kwa hatua (systematically degrade) usanifu wa kikanda (regional military architecture) unaowezesha Marekani na washirika wake kuonyesha na kutumia nguvu za kijeshi (project military power) kote Mashariki ya Kati.

Mwisho wa siku, vita havishindwi kwa kutengeneza viral videos za makombora yakitua kwenye miji mikuu au kwa symbolic strikes. Vinashindwa kwa kuharibu uwezo (capabilities) wa adui. Mara nyingi, yale malengo yanayoonekana ya kawaida na yasiyovutia kwenye ramani ndiyo yenye umuhimu mkubwa zaidi kijeshi.

DD Geopolitics
 
Why is Iran bombing Gulf states while avoiding US naval assets and Israel? | Conflict News | Al Jazeera Why is Iran bombing Gulf states while avoiding US naval assets and Israel?
 
..watu mnashabikia hii vita utadhani ni mechi ya mpira wa miguu.

..vita ni mbaya. Watu wanakufa na kuteseka.
 
Mkuu Safi sana hii.
Asante kwa kuiweka kwa lugha ambayo wengi tutaelewa.
 
Na wewe iran wa zungu wa jioni toka mbagara
Nilifikiri unajua chochote ,kumbe mtupu TU,haya nenda ukaangalie kwenye ki thread chako watu walivyokupa somo,na usipoelewa huko ntashauri upigwe ban kidogo akili ikukae sawa.
 
Sawa umejieleza sana ila kiukw3li iran aache utoto kumpiga marekani kwa makombora ni kujidanganya level ya marekani labda unaweza kumpiga kisaikolojia ila sio makombora wanajlpoteza muda na pesa nyingi bila sababu.
Soma komenti namba 17 au namba 30 kwa elimu zaidi.
 
Kama vyote hivyo vimepigwa sasa mbona Iran bado tu anapokea kipigo kila uchao na ni wiki takriban mbili sasa na hata hatujasikia hata ndege moja ya Marekani imedondoshwa, hizo Air Defence Systems za Iran mbona zimekuwa (White Elephants)..!!!!
 
1.Kwa nini Venezuela Ina WAKRISTO 87% na mafuta yake yapo chini ya U.S.A?

2.kwa nini Iran in WAISLAM 90% na gesi zake na mafuta zipo chini ya JAMHURI YA KIISLAM YA IRAN?

3.Kwa nini nchi masikini zaidi duniani zipo kusini mwa jangwa ala sahala na 80% ya population yake ni wakristo?

4. Kwa nini Zanzibar Ina WAISLAM 99% na rasilimali zake za mafuta na gesi,si Mali ya muungano na rais mzanzibar yupo hapa anatawala na anauza migodi na rasilimali za bara kama mbuga za wanyama kwa bei ya kutupa?,huku per capital ya Zanzibar ikiwa ni $2500 huku ya Tanganyika ikiwa ni $1200

5.Kwa nini ISLAMIC REPUBLIC OF IRAN na ISLAMIC REPUBLIC OF AFGHANISTAN wanamiliki rasilimali zao,100%?
 
Anayehoji kwa nini irani haipigi usa nyumbani kwake huyo ni taahira
 
Labda sijaelewa swali... anapiga nchi jirani na Marekani???

Uarabuni mujemi anapiga vituo na kambi za wamarekani... na meli zao zimekimbizwa mbali ama nazo zingepigwa tu. Kwangu mm inamaanisha anampiga mmarekani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…