Wengi wanaomshabikia Lissu hawazingatii maslahi ya Taifa

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
4,274
Reaction score
9,326
Wadau hamjamboni nyote?

Haya ni maoni makini kabisa yasiotia shaka hivyo wewe mchangiaji uache jazba na kejeli unapochangia uzi huu

Ndiyo mashabiki wake wengi hawana shughuli rasmi za kwenye mifumo, hawako makini kuainisha au kuchambua sera husika na hawatangulizi maslahi mapana ya nchi yetu

Nyongeza ni kuwa wengi wao hawana uhakika kushiriki zoezi la kupiga kura sababu kubwa hawajui kuwa uchaguzi ndiyo njia ya kidemokrasia kuingia madarakani

Niwatakie siku njema nyote
 
Wadau hamjamboni nyote?

Huu ni utafiti makini kabisa usiotia shaka hivyo wewe mchangiaji uache jazba na keheli unapochangia uzi huu

Niwatakie siku njema nyote
sure gentleman,
uko sahihi kabisaa,
kwa mfano lisu, heche na lema wote hawana ajira wala kazi za kujipatia kipato, ispokua kazi yao kubwa ni kuomba omba kuchangiwa pesa za matumizi na wanachadema ndio kupona, kujisitiri, kula na kulala yao ilipo , kinyume na hapo na kwa uvivu wao, kwakweli wangekua waokota makopo mtaani saivi 🐒
 
Kwahiyo uzalendo ni kuiba mali za umma,kuua na kuteka raia wako na kuwanyonya watumishi wa umma(mishahara na posho duni).
 
No Reforms No Elections
 
Wanazingatia kushika dola kwa njia ya uasi
 
Kwahiyo uzalendo ni kuiba mali za umma,kuua na kuteka raia wako na kuwanyonya watumishi wa umma(mishahara na posho duni).
(,na Kikotoo cha dhulma ambacho kule PSSSF mafao atayapata mstahafu kwa mujibu wa makisio yao ya kuishi miaka 12 baada ya kustahafu, haifikii hata ule mchango wake aliochangia wa 5%, achilia mbali 15% mchango wa Mwajiri)
 
Hapo mwisho umetutakia siku njema lakini ulichokiandika hapo juu kinatutakia sio tu siku bali maisha mabaya sisi na vizazi vyetu!
 
Kama mpaka unafikia umri wa kuketa mada humu jukwaani, halafu hufahamu tofauti kati ya "maslahi halisi ya Taifa" dhidi ya "maslahi ya watu wachache ndani ya ccm"; maana yake wewe utakuwa ni moja ya hasara kwa hilo Taifa.
 
Duniani kote, kwa kila kitu kitokeacho kuna sababu yake, hakuna kitu kinatokea tu, The Law of Cause and Effect; kama hakuna Haki Uzalendo utatokea wapi? Au unataka tuseme Uchawa. Penye Haki panajenga UZALENDO.
 
Wizi wa kura unadhibitiwa namna gani? jibu swali kwanza kabla ya kusema mambo mengine...
Maslahi ya taifa maana yake ni nini? Nani anayeweka? Ni vyama au ni watu wa aina gani? Nani anatakiwa kuyalinda? Hivi CCM kwa nini haioni umuhimu wa uwazi na ukweli?
Mbona Magu aliwafutilia mbali vyeti feki karibu wote... kwa nini CCM hawataki haya mambo ya uwazi yawe wazi kweli na haki?
 
Wengine hatumshabikii Lissu, tunasimama kwenye hoja ya uchaguzi huru na wa haki.

Binafsi huwa sipigagi kura miaka yote kwasababu hiyohiyo, uchaguzi sio huru na wahaki kwa hiyo kura yangu haitabadirisha kitu.

Hoja aliyokuja nayo LISSU kwangu ndio zilikuwa fikra zangu miaka yote, hakuna haja yakupiga kura kwa aina hizi za chaguzi.

Mfano; kuna haja gani yakufanya uchaguzi na kupoteza hela za walipa kodi wakati Rais anajulikana tayari na mpaka idadi ya kura zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…