...Sijui ni kipato kikubwa kiasi gani hicho Mbu ambacho kitakufanya uamue uishi mbali na familia yako. Fikiria raha ya kuona mwanao anazaliwa na kumshika mikononi mwako kwa mara ya kwanza, anakaa chini kwa mara ya kwanza na anakaa kiajabu ajabu 🙂🙂akichoka anaanguka lakini uko nyuma yake kuhakikisha unamdaka kabla hajafika sakafuni/ardhini, kumuona anaanza kutambaa kwa mara ya kwanza wengine hutambaa kiajabu ajabu 🙂🙂 mpaka ile tambaa yake inakuvunja mbavu kupita kiasi 🙂🙂 anapoanza kusimama kwa mara ya kwanza na huku wewe na mwenzio mkijaribu kumpa motisha asimame kwa muda mrefu zaidi huku mkimuimbia simama dede sima dede 🙂🙂 anapoanza kunyanyua mguu mmoja katika kujaribu kuanza kutembea na mambo mengine chungu nzima.
Mhhhhh labda kuwaona kila baada ya miezi miwili lakini miezi sita hadi nane kwa maoni yangu ni mingi saaaaana, sijui ila mimi naona hili ni gumu sana Mkuu. Unaweza kutuwekea hicho kipato kikubwa kinachozungumziwa hapa kiko katika range ipi labda $200,000 to $300,000, $300,000 to $400,000, $400,000 to $500,000 etc. Ukishajibu hili swali langu nitarudi na kisa nilichokiona kwa Oprah cha Mume ambaye almanusura apoteze ndoa yake.