Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,350
- 26,166
Membe siamini anaweza kujitoa katikati ya kampeni.Vyama vyote vya upinzani nchini vimepata wanachama wengi tu kutoka ccm. Hii ni kawaida pale upinzani unapoanza kujiunda. Siasa ni mzunguko na hasa Afrika unaweza kushangaa Magufuli akaja CDM wakati fulani na Mbowe akarudi CCM. Kinachotakiwa ni kuwa strategic. Lowassa mwaka 2015 sio kwamba aliiangusha CDM, aliijenga sana sana na kuwezesha kupatikana kwa asilimia 40 ya kura za urais na kwa kweli ilikuwa zaidi ya hizo ila mnajua bao la mkono linavyofungwa na ccm. Kama Membe atakuwa aseti akigombea kupitia CDM ni sawa. Siasa zinahitaji mtu mwenye kufikiri haraka na kuweza kubadilisha mambo yaendane na mahitaji ya wakati huo-hence kubadilisha gia angani ni kawaida na inapendekezwa.
uDAS wenyewe kuna foleni kubwa ya makada.Hao waliokimbilia CCM wakidhani wapo salama wanajidanganya, huko kuna wenyewe kweli, wasitarajie ubunge viti maalum, wataishia kupewa u- DAS wapotelee vijijini.
Well said bro!Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992, CHADEMA ina udhaifu mkubwa mmoja: kuwaamini watu haraka;kuwapa sapoti kubwa na kuwapa maisha. Ndiyo maana, CHADEMA haiishi kupokea wanaokatwa CCM na kuwapa nafasi za kugombea Urais, Ubunge na Udiwani. Hiyo ni kuanzia uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Chukulia mfano wa Balozi Dr. Wilbrod Peter Slaa ambaye 'alikatwa' ndani ya CCM na kuaminiwa na CHADEMA mwaka 1995 kule Karatu na hatimaye akawa Mbunge.
Mambo hayo yametokea karibu katika kila uchaguzi mkuu: 2000, 2005, 2010 na 2015. Inasubiriwa mwaka huu kama hali itakuwa tofauti au utaratibu utakuwa ni ule ule. Hopefully, CHADEMA imepata funzo kubwa katika 'udhaifu' wake huo nilioudokeza hapo juu. Lakini, CHADEMA iliwatoa vijana na watu wazima wengi kusikojulikana na kuwapa maisha. Ikiwa na uungwaji mkono mkubwa wa vijana, vijana maskini kabisa waliukwaa Ubunge na Udiwani na kubadili maisha yao.
CCM ni chama kikongwe zaidi hapa Tanzania. Ni chama kikubwa zaidi na ni chama tawala. Kukishinda uchaguzini kwenye nafasi yoyote kama Urais, Ubunge na Udiwani si jambo dogo na rahisi. CCM kama chama tawala na chama dola kimewahi kupoteza Majimbo na Kata kadhaa. Vijana mbalimbali wa CHADEMA, maskini wa kutupwa, waliibuka washindi na kubadili maisha yao: na wao wakaonekana, wakasikika na kuwa maarufu. Vijana hao wasingeweza kupenya na kutamba ndani ya CCM kwakuwa CCM ina wenyewe.
Kwenye vyama, watu hupanga foleni ya kusubiri zamu ya kuwa Rais, Mbunge au Diwani. Foleni ya CCM huwa kubwa na ya kuogofya. Vijana wengi ambao hupungukiwa nguvu za kifedha na kusubiri zamu zao walikuwa wakiitumia CHADEMA kama njia ya mkato kutimiza ndoto zao. CHADEMA haikuwa na hiyana: iliwaamni, ikawasimamia na kuwapa maisha. Lakini, kati ya 2016 hadi mwaka huu wengi wamekihama chama hicho. Tena kwa maneno makalimakali. Uchaguzi mwingine umefika na wapangafoleni ndani ya CCM wameanza harakati zao.
Mchuano ndani ya CCM utakuwa ni wa moto na mwishoni 'wenye chama' wataibuka kidedea. Hapo ndipo wahamaji wa CHADEMA watakapoikumbuka CHADEMA yao iliyowapokea, kuwalea, kuwasimamia na kuwapa maisha. Watalia, ima sirini au hadharani, huku wakisaga meno. Itakuwa wameshachelewa.
Asante sana MkuuWell said bro!
Wenye masikio na macho watatoa ushuhuda baaadaeeeeeee ni swala la muda...
nccr huu ujumbe unawahusu
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992, CHADEMA ina udhaifu mkubwa mmoja: kuwaamini watu haraka;kuwapa sapoti kubwa na kuwapa maisha. Ndiyo maana, CHADEMA haiishi kupokea wanaokatwa CCM na kuwapa nafasi za kugombea Urais, Ubunge na Udiwani. Hiyo ni kuanzia uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Chukulia mfano wa Balozi Dr. Wilbrod Peter Slaa ambaye 'alikatwa' ndani ya CCM na kuaminiwa na CHADEMA mwaka 1995 kule Karatu na hatimaye akawa Mbunge.
Mambo hayo yametokea karibu katika kila uchaguzi mkuu: 2000, 2005, 2010 na 2015. Inasubiriwa mwaka huu kama hali itakuwa tofauti au utaratibu utakuwa ni ule ule. Hopefully, CHADEMA imepata funzo kubwa katika 'udhaifu' wake huo nilioudokeza hapo juu. Lakini, CHADEMA iliwatoa vijana na watu wazima wengi kusikojulikana na kuwapa maisha. Ikiwa na uungwaji mkono mkubwa wa vijana, vijana maskini kabisa waliukwaa Ubunge na Udiwani na kubadili maisha yao.
CCM ni chama kikongwe zaidi hapa Tanzania. Ni chama kikubwa zaidi na ni chama tawala. Kukishinda uchaguzini kwenye nafasi yoyote kama Urais, Ubunge na Udiwani si jambo dogo na rahisi. CCM kama chama tawala na chama dola kimewahi kupoteza Majimbo na Kata kadhaa. Vijana mbalimbali wa CHADEMA, maskini wa kutupwa, waliibuka washindi na kubadili maisha yao: na wao wakaonekana, wakasikika na kuwa maarufu. Vijana hao wasingeweza kupenya na kutamba ndani ya CCM kwakuwa CCM ina wenyewe.
Kwenye vyama, watu hupanga foleni ya kusubiri zamu ya kuwa Rais, Mbunge au Diwani. Foleni ya CCM huwa kubwa na ya kuogofya. Vijana wengi ambao hupungukiwa nguvu za kifedha na kusubiri zamu zao walikuwa wakiitumia CHADEMA kama njia ya mkato kutimiza ndoto zao. CHADEMA haikuwa na hiyana: iliwaamni, ikawasimamia na kuwapa maisha. Lakini, kati ya 2016 hadi mwaka huu wengi wamekihama chama hicho. Tena kwa maneno makalimakali. Uchaguzi mwingine umefika na wapangafoleni ndani ya CCM wameanza harakati zao.
Mchuano ndani ya CCM utakuwa ni wa moto na mwishoni 'wenye chama' wataibuka kidedea. Hapo ndipo wahamaji wa CHADEMA watakapoikumbuka CHADEMA yao iliyowapokea, kuwalea, kuwasimamia na kuwapa maisha. Watalia, ima sirini au hadharani, huku wakisaga meno. Itakuwa wameshachelewa.
Katika mazingira sawa?wafuasi wote wa CHADEMA ni mazwazwa hawajui walifanyalo. CMM chini ya JPM haina mpinzani hata kidogo.
Wanajidanganya na mbeleko ya Magufuli ilhali nayeye atakua anaipambania roho yake.
Hao waliokimbilia CCM wakidhani wapo salama wanajidanganya, huko kuna wenyewe kweli, wasitarajie ubunge viti maalum, wataishia kupewa u- DAS wapotelee vijijini.
Petro E. Mselewa,
Vyama vyote vya upinzani nchini vimepata wanachama wengi tu kutoka ccm. Hii ni kawaida pale upinzani unapoanza kujiunda. Siasa ni mzunguko na hasa Afrika unaweza kushangaa Magufuli akaja CDM wakati fulani na Mbowe akarudi CCM. Kinachotakiwa ni kuwa strategic. Lowassa mwaka 2015 sio kwamba aliiangusha CDM, aliijenga sana sana na kuwezesha kupatikana kwa asilimia 40 ya kura za urais na kwa kweli ilikuwa zaidi ya hizo ila mnajua bao la mkono linavyofungwa na ccm. Kama Membe atakuwa aseti akigombea kupitia CDM ni sawa. Siasa zinahitaji mtu mwenye kufikiri haraka na kuweza kubadilisha mambo yaendane na mahitaji ya wakati huo-hence kubadilisha gia angani ni kawaida na inapendekezwa.
Petro E. Mselewa,
Nakupa like kwa mara ya kwanza Mkuu umeandika ukweli mtupu, pia tatizo moja hujasema Lisu kukaa mbali na wapiga kura alafu unategemea ushinde, leo hii Lisu angekuwepo angekuwa hata magereza ambapo wananchi wangempa kura za huru na dunia ingeona lakini wanasubiri aje aibuke dak za mwisho huku CCM wanafanya kampeni peke yao.
Kweli Leo umeandika point tupu