wafuasi wote wa CHADEMA ni mazwazwa hawajui walifanyalo. CMM chini ya JPM haina mpinzani hata kidogo.
Na hapo ndipo wakina juakali watajua maana ya buti JEJE.Vijana wanasahau kuwa CCM sio umaarufu utakaokutoa, ni pesa na kujuana na wakubwa. Waombe Mungu mwenyekiti awape fadhira, ila kwa hakika wengi hawatatoboa
Yaani pamoja na aliyoyafanya Lowassa bado unaona Membe atafaa Chadema?Comment imejitosheleza kabisa kwa afya ya upinzani nchini Tanzania
Lowasa alikuwa anatafuta urais ndani ya ccm, aliposhindwa akakimbilia upinzani kuutafuta huo urais.Yaani pamoja na aliyoyafanya Lowassa bado unaona Membe atafaa Chadema?
Haya ni maajabu aisee.
Kama akili ndio ziko hivi acha tu wana CCM waendelee kuitumia Chadema kugombea urais then wakimaliza kazi waliyotumwa warudi zao CCM,hakuna namna tena.Lowasa alikuwa anatafuta urais ndani ya ccm, aliposhindwa akakimbilia upinzani kuutafuta huo urais.
Membe amefukuzwa na kufutiwa kabisa uanac
hama
Umekuna na style nzuri ya kuaga "Tata bye"Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1992, CHADEMA ina udhaifu mkubwa mmoja: kuwaamini watu haraka;kuwapa sapoti kubwa na kuwapa maisha. Ndiyo maana, CHADEMA haiishi kupokea wanaokatwa CCM na kuwapa nafasi za kugombea Urais, Ubunge na Udiwani. Hiyo ni kuanzia uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995. Chukulia mfano wa Balozi Dr. Wilbrod Peter Slaa ambaye 'alikatwa' ndani ya CCM na kuaminiwa na CHADEMA mwaka 1995 kule Karatu na hatimaye akawa Mbunge.
Mambo hayo yametokea karibu katika kila uchaguzi mkuu: 2000, 2005, 2010 na 2015. Inasubiriwa mwaka huu kama hali itakuwa tofauti au utaratibu utakuwa ni ule ule. Hopefully, CHADEMA imepata funzo kubwa katika 'udhaifu' wake huo nilioudokeza hapo juu. Lakini, CHADEMA iliwatoa vijana na watu wazima wengi kusikojulikana na kuwapa maisha. Ikiwa na uungwaji mkono mkubwa wa vijana, vijana maskini kabisa waliukwaa Ubunge na Udiwani na kubadili maisha yao.
CCM ni chama kikongwe zaidi hapa Tanzania. Ni chama kikubwa zaidi na ni chama tawala. Kukishinda uchaguzini kwenye nafasi yoyote kama Urais, Ubunge na Udiwani si jambo dogo na rahisi. CCM kama chama tawala na chama dola kimewahi kupoteza Majimbo na Kata kadhaa. Vijana mbalimbali wa CHADEMA, maskini wa kutupwa, waliibuka washindi na kubadili maisha yao: na wao wakaonekana, wakasikika na kuwa maarufu. Vijana hao wasingeweza kupenya na kutamba ndani ya CCM kwakuwa CCM ina wenyewe.
Kwenye vyama, watu hupanga foleni ya kusubiri zamu ya kuwa Rais, Mbunge au Diwani. Foleni ya CCM huwa kubwa na ya kuogofya. Vijana wengi ambao hupungukiwa nguvu za kifedha na kusubiri zamu zao walikuwa wakiitumia CHADEMA kama njia ya mkato kutimiza ndoto zao. CHADEMA haikuwa na hiyana: iliwaamni, ikawasimamia na kuwapa maisha. Lakini, kati ya 2016 hadi mwaka huu wengi wamekihama chama hicho. Tena kwa maneno makalimakali. Uchaguzi mwingine umefika na wapangafoleni ndani ya CCM wameanza harakati zao.
Mchuano ndani ya CCM utakuwa ni wa moto na mwishoni 'wenye chama' wataibuka kidedea. Hapo ndipo wahamaji wa CHADEMA watakapoikumbuka CHADEMA yao iliyowapokea, kuwalea, kuwasimamia na kuwapa maisha. Watalia, ima sirini au hadharani, huku wakisaga meno. Itakuwa wameshachelewa.
Kwahiyo unaona hii ni bonge la point [emoji23]wafuasi wote wa CHADEMA ni mazwazwa hawajui walifanyalo. CMM chini ya JPM haina mpinzani hata kidogo.
Heheheh... Wakenya wanasema "watajua kuwa hawajui"Na hapo ndipo wakina juakali watajua maana ya buti JEJE.
Membe na Lowassa sio tofauti sana kwa malengo ya kuingia Ikulu.Watu wengi wana mashaka na ujio wa Membe ndani upinzani kupitia kile walichojifunza kwa Lowassa. Lakini kuna jambo la msingi sana ktk kutaka kulitafakari kwa kina suala hili.
Mazingira ya kisiasa yaliyochochea wawili hawa waliotajwa hapo juu kutaka kukimbilia upinzani na kutaka kuungwa mkono yapo ktk mizania tofauti mno. Wakati Mzee Lowassa alitaka kufikia level ya juu kabisa ya kutaka kushika madaraka ya juu kabisa hapa nchini, yaani "self actualisation of needs" iwe ndani ama ndani ya chama chake. Alikuwa akisukumwa zaidi na "personal drive & desire" pasipokuwa na agenda za kimkakati zenye muhamasisho na msukumo wa kutaka kuleta matokeo chanya kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Kwa upande wa Membe, huyu ana kitu cha ziada kwa kumlinganisha na Lowassa. Alikuwa mwanachama mwenye uthubutu wa kumkabili Mwenyekiti taifa ili wanachama wakapate kuwapima na kuwalinganisha ubora wa maono yao. Kwa hakika alikuwa na kiu na dhamira ya dhati ya kutaka kutimiza maono yake kupitia kofia ya chama chake ambacho kimemkuza na hata kufikia hapo alipo.
Tofauti kubwa sana iliyopo kati yake na Lowassa ni kuwa, huyu ni "stateman" tofauti na Lowassa ambaye alikuwa ni kada wa kawaida wa chama cha kisiasa. Lakini anaweza kuaminika kwa urahisi kwa kuwa, jitihada yake ya awali imezimwa kwa zongo na zengwe pasipo yeye kuridhika na hata kujikuta akipoteza uanachama, kitu ambacho kimezima ndoto na maono yake kupitia chama ambacho alikitumainia sana.
Kama akili ndio ziko hivi acha tu wana CCM waendelee kuitumia Chadema kugombea urais then wakimaliza kazi waliyotumwa warudi zao CCM,hakuna namna tena.
Anakimbiza bk7Kwahiyo unaona hii ni binge la point [emoji23]
UVCCM wanaosubiri umewapeleka wapi? Hao ndio imetoka hiyo!Hao vijana wengine hawana cha kukumbuka CHADEMA Isitoshe hata wakikatwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM, hawana cha kupoteza mfano Waitara!
Waitara aliambiwa mapema kabisa na Mbowe kwamba asitarajie kupitishwa 2020.
Itoshe tu kusema kwamba hao vijana waliotimkia CCM ndo DCs wa baada ya uchaguzi ilhali hata wangeendelea kubaki CDM hata hicho kidogo wangekikosa.
Uchaguzi wa 2020 hakuna rough hamtaiona,subiri kuuona ukiritimba utavyoanzia kwenye kurudisha form tu.
Mwisho wa siku hakuna chama kisicho na wenyewe!!
Ngoja tusubiri tuone kama haya yatatimia.Mchuano ndani ya CCM utakuwa ni wa moto na mwishoni 'wenye chama' wataibuka kidedea. Hapo ndipo wahamaji wa CHADEMA watakapoikumbuka CHADEMA yao iliyowapokea, kuwalea, kuwasimamia na kuwapa maisha. Watalia, ima sirini au hadharani, huku wakisaga meno. Itakuwa wameshachelewa.
Kwani akina Katambi,Kafulila,Mtatiro etc walipoteuliwa UVCCM walikuwa wapi?UVCCM wanaosubiri umewapeleka wapi? Hao ndio imetoka hiyo!
Hawa na wale wa viti maalum watategemea mbeleo ya mwenyekiti wa Ccm ni imara kiasi gani, kama italegea ujue imekula kwao.Na hapo ndipo wakina juakali watajua maana ya buti JEJE.
Du!Mkuu Lissu hakupenda kuwa nje ya Tanzania kwa kipindi kirefu, kumbuka masaibu yaliyo mpata.
Angesema abakie hapa hapa kwetu kisa wananchi wamsikie kila siku basi leo hii tusingekuwa naye hapa duniani.