GE2025 Wenje: Kiongozi aliye tayari kufa ni Kiongozi aliyekata tamaa

GE2025 Wenje: Kiongozi aliye tayari kufa ni Kiongozi aliyekata tamaa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
"Biblia inasema Mungu hafanyi kazi na watu waoga wanaoogopa ushindani. Sasa watu waoga wanaokimbia uchaguzi licha ya mapendekezo na maombi yao kufanyiwa kazi ni hodari na shujaa? Ni hatari sana kuwa na Kiongozi wa Chama Cha Siasa anayesema yupo tayari kufa. Kiongozi aliye tayari kufa ni Kiongozi aliyekata tamaa kwasababu hakuna matumaini kwenye kifo." Amesema Bw. Wenje.

 
Ukifuga jini likakosa damu lazima likunyonye damu mfugaji au liende kutafuta damu sehemu nyingine.
 
Tumuamini Wenje yupi yule wa CHADEMA au huyu wa CCM hawa wanasiasa wa ugagaa na upwa hawa... ni hatari sana.
 
Hyo ndo maana ya demokrasia...
Au wenzetu lile neno la mwisho demokrasia mnalichukulia kama matusi au?
 
Haya matapishi yake anayatoa baada ya kuhongwa pombe, chakula na hela, na Abdul! Msaliti mkubwa huyo aliyekatwa mshipa wa aibu.
 
Huyu mtu ni tapeli wa siasa, ana laana kubwa juu ya kichwa chake. Alijifanya mpinzani wa CCM, wengi wakamwamini, hata wale greenguards wakaamini hivyo, wakamwua hata kaka yake, bila ya kujua kuwa huyu mtu ni mwenzao.

Huyu ibilisi, damu ya kakake itamlilia hadi kiama.

Kwa uongozi wa sasa ndani ya CHADEMA, amegundua hawezi kufanya kikamilifu kazi aliyopewa na CCM ndani ya CHADEMA, maana CCM walitaka awe makamu mwenyekiti, ameamua kurudi kwa shetani aliyemtuma. Na huko, muda si mrefu atapuuzwa maana watagundua hana msaada, zaidi ya kutumika kutoa orodha ya wanaotakiwa kutekwa, kama alivyofanya yule mchungaji fake.
 
"Biblia inasema Mungu hafanyi kazi na watu waoga wanaoogopa ushindani. Sasa watu waoga wanaokimbia uchaguzi licha ya mapendekezo na maombi yao kufanyiwa kazi ni hodari na shujaa? Ni hatari sana kuwa na Kiongozi wa Chama Cha Siasa anayesema yupo tayari kufa. Kiongozi aliye tayari kufa ni Kiongozi aliyekata tamaa kwasababu hakuna matumaini kwenye kifo." Amesema Bw. Wenje.

Tarehe 29.10.2025 tutamtafuta na yeye popote atakapokuwepo Ili tumpe haki yake ya usaliti
 
"Biblia inasema Mungu hafanyi kazi na watu waoga wanaoogopa ushindani. Sasa watu waoga wanaokimbia uchaguzi licha ya mapendekezo na maombi yao kufanyiwa kazi ni hodari na shujaa? Ni hatari sana kuwa na Kiongozi wa Chama Cha Siasa anayesema yupo tayari kufa. Kiongozi aliye tayari kufa ni Kiongozi aliyekata tamaa kwasababu hakuna matumaini kwenye kifo." Amesema Bw. Wenje.


..hata aliowakuta Ccm hawazungumzi mambo ya hovyo kama anavyofanya Wenje.

..awe muangalifu Ccm wasije wakamtupa kama walivyofanya kwa Peter Msigwa ambaye amepotea katika ulingo wa siasa.
 
Back
Top Bottom