Wenye akili kubwa na walioshiba njooni mnisaidie kupata jibu

Wenye akili kubwa na walioshiba njooni mnisaidie kupata jibu

Sijaona sehemu yoyote inayo hitaji mtu mwenye akili kubwa kwenye andishi lako.
 
Natumia akili ndogo tu kujibu.
Mwenye njaa siku zote ndo anae kutana na majaribu.shukuru mungu,sn kua mwenye nyumba wa aina hiyo.akunnuri chakula.ameonyesha uungwana mkubwa sna.bira kujari shida zako,matatizo yako,nawe tenda wema ktk hilo.RUDISHA TENA UKIWA NA FURAHA.
 
Wana JF nisaidien kupata jibu la swala hili mfano, wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga, mambo yamegoma ukalimbikiza deni la kodi ya miezi 3 sawa na Tsh 300,000/= .
Mwenye nyumba akakupa siku tatu uwe umemlipa hiyo pesa ukishindwa anakuondoa kwake,,,, Basi kesho yake ukaamkia kuitafuta hiyo pesa, sasa imefika saa 7 mchana hujapata na unahisi njaa, wakati uko mtaani unajikuta umekatiza karibu na restaurant( hoteli iayouza chakula) ,mara ukasikia mtu anakuita pale restaurant.
Ukaenda ile umefika ukamuona yule mwenye nyumba ndo anakuita, akakuagizia chakula na kukulipia ukaanza kula muda ule ule yeye akaondoka,,,ukahamia kwenye kiti alichokuwa amekalia, ukakuta wallet imejaa noti za elfu 10, ukaichukua na kuiweka mfukoni,
Dakika 3 baadae yule mwenye nyumba akarudi pale akakukuta umekalia kile kiti akakuuliza vipi ndugu umeniokotea waleti yangu hapo kwenye kiti ila sina uhakika kama nimeidondosha hapa ina Tsh Milioni1
....Je UTAKUBALI au UTAKATAA??
Hadithi nyingine bhana...ningemwambia mimi ni mgeni sikuwahi kufika kwenye huo mgahawa!
 
Namrudishia pamoja na proposal ya kuongezewa muda wa kulipa deni, naamini atanielewa tu.
 
Kwa swali hili akili kubwa inatumika wapi?
Unafikiri unaweza ukamjibu mwenye wallet ki urahisi tu, eti, una shida ya kufa mtu, una njaa hata kesho hujui utakula nini, ndio maana unahitaji akilikubwa kumjibu vinginevyo ubaki na matatizo yako yakutese au upate jibu la haraka ambalo halita athiri maisha yako na yakwake.
 
Wana JF nisaidien kupata jibu la swala hili mfano, wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga, mambo yamegoma ukalimbikiza deni la kodi ya miezi 3 sawa na Tsh 300,000/= .

Mwenye nyumba akakupa siku tatu uwe umemlipa hiyo pesa ukishindwa anakuondoa kwake,,,, Basi kesho yake ukaamkia kuitafuta hiyo pesa, sasa imefika saa 7 mchana hujapata na unahisi njaa, wakati uko mtaani unajikuta umekatiza karibu na restaurant( hoteli iayouza chakula) ,mara ukasikia mtu anakuita pale restaurant.

Ukaenda ile umefika ukamuona yule mwenye nyumba ndo anakuita, akakuagizia chakula na kukulipia ukaanza kula muda ule ule yeye akaondoka,,,ukahamia kwenye kiti alichokuwa amekalia, ukakuta wallet imejaa noti za elfu 10, ukaichukua na kuiweka mfukoni.

Dakika 3 baadae yule mwenye nyumba akarudi pale akakukuta umekalia kile kiti akakuuliza vipi ndugu umeniokotea waleti yangu hapo kwenye kiti ila sina uhakika kama nimeidondosha hapa ina Tsh Milioni1

Je, UTAKUBALI au UTAKATAA??

Sikubali wala sikatai ila nitamuua kwa hasira.
 
Swali lako halina tofauti na maswali ya KIPIMA JOTO ya ITV.Ova!
 
Kwenye nyumba ambaye anakudai miezi 3 ya pango, na ameshakupa deadline siyo rafiki.

Uwezekano wa kukuona akakuita na akununulie chakula ni 5%.
 
Wewe umefanya maamuzi gani?? Au unasubiri majibu yetu ndo ufanye maamuzi?
 
Huo uamuzi wa hasira utakuwaje twambie

Amenidai na kunipa pressure kisha anakuja kunisanifu kama nimeokota wallet yake, tena mbele za watu....hapa naua tu....atanidhalilishaje mbele ya watu, mie si mwanamme wa Zanzibar, Tanga, wala Dar?
 
Siku nyingine Acha kusumbua hao unaowaita wenye akili kubwa na ufanye maamuzi sahihi
 
Hili nalo linahitaji akili kubwa? CCM imedumaza sana uwezo wa Watanzania kufikiri!
 
Back
Top Bottom