Wenye akili timamu tujadiri hili, yanayoendea simba na yanga ni utani au chuki?

Hivi unajua Haji Manara amechangia kwa asilimia kubwa huu uhasama uliopo? Alianza wakati yuko Simba kuwatukana washabiki wa Yanga kuwa ni hamnazo (wapumbavu) ila Baba yake Mzee Sunday Manara na Mzee JK. Aliwahi kumkejeli Makamu Mwenyekiti wa Yanga Kwa kumuita kilo 800 kutokana na maumbile yake. Na baada ya kufukuzwa Simba kwa utovu huo wa nidhamu ndiyo Yanga wakamdaka na jujumu lake likawa kuwatukana viongozi wa Simba na kuikashifu club ya Simba kila alilopata jukwaa la kuongea.

Nakushangaa wewe kumtetea huyu chanzo cha matatizo na kuona yeye ndiye anaonewa. Hatuwezi kupata ufumbuzi wa tatizo kwa kukwepa kujua chanzo chake.
Asanteeeeee! Chanzo cha tatizo la Manara ni Manara mwenyewe. Ujuaji mwingiiiii!
 
Utani wa simba na yanga ulijengwa kwenye misingi ya ushindani toka huko nyuma hasa uwezo wa uwanjani.

Leo utani umetoka kwenye misingi yake badala yake imekuwa mashambulizi ya mtu na mtu au kundi na mtu.
Imefika mahali chuki imekuwa kubwa hata huku mitaani.

Imefika mahali timu fulani ikikutwa na kadhia fulani au kiongozi wa timu fulani,watu wanatukanana hovyo.
Vijana wanawatukana wazee utadhani kwao hakuna wazee.

HALI HII IKIACHWA IENDELEE HUKO MBELE ITAKUWA NA MADHARA MAKUBWA KWA TAIFA.
Leo hii Haji Manara anatukanwa pande zote,mitandaoni mpk mitaani.
Je huu ni utani?

Tunajua tff imeoza haitamaniki na ndiyo chanzo cha matatizo ya mpira wetu,haiwezi kukemea timu yoyote.

JE WIZARA YENYE DHAMANA NA SOKA LETU HAIONI HAYA?

weusi wenzetu huko ulaya wakiitwa nyani sisi tunalalamika,lakini Mara kadhaa tumeona mamlaka zao zikitoa adhabu kwa timu husika ili mashabiki zao wasiendelee kubagua rangi za binaadam wenzao.

Sakata la manara kufungia,anakula matusi ya nguoni,ana baguliwa na kuitwa majina mengi mabaya kutokana na ulemavu wake,je huu ni utani wa mpira?

Serikali ipo tu!
Moja ya sheria za jamii forum ni kutomshambulia mtu bali kumjibu hoja.

LEO WAPENZI WA SIMBA WANAMKASHIFU HAJI NA KUMTUSI VIBAYA VIBAYA, MAADIMIN MPO KIMYA TU WALA HAMCHUKUI HATUA!!!!

Mfano huyu gentermycine,kwa siku anaanzisha nyuzi nyingi za kumkashifu na kumtusi Haji,lakini kesho na kesho kutwa utamkuta yupo tu humu anatembea na nyuzi zake.
MAADIMIN
Mmelala,macho hayaoni,fahamu hazifanyi kazi au?
Mpk leo hakuna tusi linalothibitishwa waziwazi kuwa Haji kamtukana Karia.

Wasemaji wanamung'unya maneno tu,wanashindwa kuyakaza,lakini wanasimba hawaoni haya wanamchafua haji,kisa alitoka kwao.
HUU NDIYO MPIRA WETU ULIPOFIKIA!!

Haji anafamilia na wazazi pia,mmejiuliza wanajisikiaje mnapomkashifu kwa kumwita sokwe mwekundu? Admin mnawaacha tu! Serikali inaacha tu!
Manara alikua ameibeza Yanga kwa miaka 6 akukua na tatizo tulichukulia kama utani,manara alikua anaenda kaunda pale kutukebehi ila alipoanza kuikebehi simba tu kaitwa kila jina na kutukanwa juu,na sasa hivi hamna kiumbe anaechukiwa na wanasimba kumshinda manara tena hapo toka aanze kuwakebehi hata mwaka bado while wenzao tulimvumilia miaka 6
 
Ni kweli mimi sio muumini wa kuponda udhaifu wa mtu eidha race au weakness yeyote ile

Watu tumetofautiana kihisia, kuna vitu ambavyo kwako vinaweza vikawa vidogo lakini vitu hivyo hivyo kwa mwingine vinaweza kuzuia gumzo.

Kumbuka huyo manara alishawahi dhihaki weakness ya mtu kumwambia mwakalebela ana kilo 800 kwasababu tu ya unene wake.

Kwa kipindi kile hakuna mtu aliyejitokeza kukemea hilo, hata kwa nyinyi mnao jinasibu kutokuwa na upande lakini hamkuwahi kukemea mlilichukulia poa

Ahmedy ally kila siku anaambiwa anabana pua kwasababu tu ya uongeaji wake. Lini ushawahi kujitokeza kukemea?

Au hao wanaolalamikia haji kudhihakiwa race yake ulishawahi ona wakionesha kutofurahishwa na kauli hiyo?

Mwisho ni kwamba kila mtu aplay role yake, unaweza kuwa msemaji bila kutumia lugha za kejeli zinazogusa moja kwa moja udhaifu wa mtu. Kwasababu nao hao watu watafika hatua wataangalia sehemu gani ambayo wewe una udhaifu halafu watajua watumie vipi udhaifu huo kutengeneza vijembe ambavyo vitakuuma.
Naomba kuanzia Leo fuatilia comments zangu kwenye thread yoyote inayoongelea Kashifa iwe ya Manara, Jembe ni Jembe, Jerry Murro au Jemadari Said maana hao ndo Wanamichezo wasioweza kutofautisha Weekend na siku za mapumziko.
 
Msome hapa shafii dauda

Kuna vitu havipo sawa kwenye mpira kisa Usimba na Uyanga, kuna muda tunataka kubadili nyeupe kuwa nyeusi kisa Usimba na Uyanga, this is not fair.

Nalitazama sakata la Haji Manara na hukumu ya miaka miwili namna watu wengi wanavyopinga hukumu na kuipa presha kubwa sana TFF, hiyo haipo sawa.

Mlikuwa wapi wakati Mbwana Makata anapigwa miaka mitano, Lwitiko wa Mbeya anachukua miaka 10, kuna yule Kiongozi wa Biashara United kafungiwa maisha na hata Mimi nimepigwa miaka mitano.

Haji sio exceptional ni Mwanafamilia ya mpira kama ilivyo kwa wengine, anapopewa hukumu kwa mujibu wa kanuni haipaswi kuonekana ameonewa, kumbuka hata Mimi nilifungiwa kisa tu MAKALA tena ya mtandaoni, why not Haji dhidi ya Rais wa TFF?

Tunaupa taswira gani mpira wetu? Tunamaanisha kosa likifanywa na vigogo wa Kariakoo it means linapaswa kufumbiwa macho? Jibu ni HAPANA, binafsi ni muumini wa utawala wa sheria.

Kila kitu kipo wazi sana, kama Haji hajaridhishwa na hukumu anapaswa kukata rufaa, ni haki yake! Sioni mantiki ya press na kusigana bila sababu, ni kuonesha mnataka kuwa juu ya mfumo.

Sioni sababu ya mvutano, Haji na Yanga wana vitu viwili tu vya kufanya kwasasa, kukata rufaa kama hawajaridhika au kukaa kimya ili Haji atumikie adhabu yake, nje na hapo ni kuunajisi mpira wa miguu na kupoteza sifa nzuri tunayoanza kuijenga

Nawaelewa nyote kuwa mnaamini kwenye haki na sheria, lakini kuna utaratibu wake, napenda sana kumuona Ndugu yangu Haji kwenye mpira ila kuna utaratibu wake nae anafahamu, basi muufuate

Tunapocodify na kuweka mifumo ituongoze ni kwakuwa tunafahamu sie ni Binadamu na huwa tunakosea, hatuwezi kwenda bila mfumo na sio kwa ubaya, inapokuja sheria haipaswi kuwa Simba wala Yanga bali SHERIA

DIGALA
Unaweza kunitafutia Uzi alipofungiwa Shafii Dauda uone tuliongea nini?
 
Mkuu umesema hakuna maneno yaliyothibitika kuwa alimtukana Raisi wa TFF Uko serious???? Hivi " unanifatilia Sana wewe leo ni Mara ya tatu sikuogopi Na huna Cha kunifanyia naweza kukufanya kitu chochote Na Wala huna Cha kunifanya " mwisho wa nukuu.

Mkuu hayo tu amemtishia Hilo ni jinai ilitakiwa aende polisi pengne hizo siku mbili Raisi wa TFF angezulika au kupiga hata Na vibaka au majambazi ni Nani angekuwa suspect namba moja? Jibu ni manara.

Kingne Kama Hana hatia Na hakuwa ametenda kosa ni kwa Nini aliomba msamaha??
Hilo ni tusi?
 
Nilitaka nishangae Yani mwenye Akili timamu ajiite Kambale Mnene...! Umeanza Kwa kujiita mwenye Akili timamu nikakimbilia mbio kuja kuona huyo mwenye Akili timamu anaandika nini

Ningeshangaa kama kweli nawewe ungekuwa na Akili timamu maana tunajua huko Yanga wenye Akili timamu Kwa mujibu wa mtu unaemtetea ni Mzee kikwete na Mzee Sunday

Na ulichoandika kinaashiria ni kweli we haupo kwenye Hilo kundi la watu wawili wenye Akili hapo Yanga, kwa kifupi ni kwamba umejaa unafki tu na huna points maana huyo unaemtetea ndio aliefanya utani wa Simba na Yanga kwenda kwenye uhasama uliopo Leo hii

Ungeanza Kwa kukemea kwanza lugha anazotumiaga huyo mtu mnaepokezana kumtetea tangu Juzi basi angalau tungefikilia kukuongeza kwenye kundi la watu wenye Akili timamu pale Yanga na angalau mkawa watu watatu
 
🚨 KUTOKA KWA BUGATI

Kupanga ni kuchagua. Wakati Yanga akichukua Treble this season kwa kushinda Ngao Ya Jamii, Azam federation na Ligi kuu, Makolo Treble zao ni

👉Mpole Cup

👉Sopu Cup

👉Sakho Cup Kiufupi chake Treble ya Manyonyo inaitwa MSOSA.

Nb :: Tabu ipo pale pale Makolo,,hadi mtueleze kale katwenty mmekaficha wapi MSOSA KAMA MSOSA TREBLE Byuti Byuti 🏆🏆🏆
 
Mkuu umesema hakuna maneno yaliyothibitika kuwa alimtukana Raisi wa TFF Uko serious???? Hivi " unanifatilia Sana wewe leo ni Mara ya tatu sikuogopi Na huna Cha kunifanyia naweza kukufanya kitu chochote Na Wala huna Cha kunifanya " mwisho wa nukuu.

Mkuu hayo tu amemtishia Hilo ni jinai ilitakiwa aende polisi pengne hizo siku mbili Raisi wa TFF angezulika au kupiga hata Na vibaka au majambazi ni Nani angekuwa suspect namba moja? Jibu ni manara.

Kingne Kama Hana hatia Na hakuwa ametenda kosa ni kwa Nini aliomba msamaha??
Ninachokiona hapo haji amerushiana maneno na mamlaka tu. Matusi yote duniani yanatamkika ,taja tusi mkuu
 
Msome hapa shafii dauda

Kuna vitu havipo sawa kwenye mpira kisa Usimba na Uyanga, kuna muda tunataka kubadili nyeupe kuwa nyeusi kisa Usimba na Uyanga, this is not fair.

Nalitazama sakata la Haji Manara na hukumu ya miaka miwili namna watu wengi wanavyopinga hukumu na kuipa presha kubwa sana TFF, hiyo haipo sawa.

Mlikuwa wapi wakati Mbwana Makata anapigwa miaka mitano, Lwitiko wa Mbeya anachukua miaka 10, kuna yule Kiongozi wa Biashara United kafungiwa maisha na hata Mimi nimepigwa miaka mitano.

Haji sio exceptional ni Mwanafamilia ya mpira kama ilivyo kwa wengine, anapopewa hukumu kwa mujibu wa kanuni haipaswi kuonekana ameonewa, kumbuka hata Mimi nilifungiwa kisa tu MAKALA tena ya mtandaoni, why not Haji dhidi ya Rais wa TFF?

Tunaupa taswira gani mpira wetu? Tunamaanisha kosa likifanywa na vigogo wa Kariakoo it means linapaswa kufumbiwa macho? Jibu ni HAPANA, binafsi ni muumini wa utawala wa sheria.

Kila kitu kipo wazi sana, kama Haji hajaridhishwa na hukumu anapaswa kukata rufaa, ni haki yake! Sioni mantiki ya press na kusigana bila sababu, ni kuonesha mnataka kuwa juu ya mfumo.

Sioni sababu ya mvutano, Haji na Yanga wana vitu viwili tu vya kufanya kwasasa, kukata rufaa kama hawajaridhika au kukaa kimya ili Haji atumikie adhabu yake, nje na hapo ni kuunajisi mpira wa miguu na kupoteza sifa nzuri tunayoanza kuijenga

Nawaelewa nyote kuwa mnaamini kwenye haki na sheria, lakini kuna utaratibu wake, napenda sana kumuona Ndugu yangu Haji kwenye mpira ila kuna utaratibu wake nae anafahamu, basi muufuate

Tunapocodify na kuweka mifumo ituongoze ni kwakuwa tunafahamu sie ni Binadamu na huwa tunakosea, hatuwezi kwenda bila mfumo na sio kwa ubaya, inapokuja sheria haipaswi kuwa Simba wala Yanga bali SHERIA

DIGALA
Pamoja na ushauri na maoni hayo ya Shaffiiiii, acha avurumishiwe maneno ya hovyo!
 
we mwenyewe nawe ndio wale wale huna lolote ungekuwa na busara usingemtaja Gentamycin kama umemtolea mfano ungatafuta wote wenye maudhui kama yake mfano Demigod yeye kila siku maneno ya dharau kwa Simba hata juzi anasema goli la sako Simba wamenunua huyu mbona hujamtaja humu Jamii forum anavyoichafua Simba au hujamuona au na ww unachuki na Gentamycin?
Ili ungekuwa fair ungewataja wote wanaoleta kuchafuana humu lkn ukimtaja mtu mmoja peke yake na wengine wapo hujatendea haki jukwaa nawe tunakuweka katika kundi hilo la ushabiki maandazi
Rudi kwenye thread yangu uelewe nilichoandika na nini maudhui yake.
Kama umeenda shule japo std 7,utaelewa kuwa mifano huwa michache sana na ikibidi mmoja tu kama wanafunzi ni waelewa.
Sikuwa na haja na wengine.
 
Ni kweli mimi sio muumini wa kuponda udhaifu wa mtu eidha race au weakness yeyote ile

Watu tumetofautiana kihisia, kuna vitu ambavyo kwako vinaweza vikawa vidogo lakini vitu hivyo hivyo kwa mwingine vinaweza kuzuia gumzo.

Kumbuka huyo manara alishawahi dhihaki weakness ya mtu kumwambia mwakalebela ana kilo 800 kwasababu tu ya unene wake.

Kwa kipindi kile hakuna mtu aliyejitokeza kukemea hilo, hata kwa nyinyi mnao jinasibu kutokuwa na upande lakini hamkuwahi kukemea mlilichukulia poa

Ahmedy ally kila siku anaambiwa anabana pua kwasababu tu ya uongeaji wake. Lini ushawahi kujitokeza kukemea?

Au hao wanaolalamikia haji kudhihakiwa race yake ulishawahi ona wakionesha kutofurahishwa na kauli hiyo?

Mwisho ni kwamba kila mtu aplay role yake, unaweza kuwa msemaji bila kutumia lugha za kejeli zinazogusa moja kwa moja udhaifu wa mtu. Kwasababu nao hao watu watafika hatua wataangalia sehemu gani ambayo wewe una udhaifu halafu watajua watumie vipi udhaifu huo kutengeneza vijembe ambavyo vitakuuma.
Uwingi wa kilo ni ulemavu? Watu wengine bhana!
Kama hujaelewa kaa kimya, wengine walioelewa wachangie.
UKIMYA NAO NI BUSARA
 
Huyu ndio wale wale hana analojua kwanini amtaje Gentamycin peke yake ni bora asingemtaja uzi wake ungekuwa bora sana ila kitendo cha kumtaja Genta peke yake na kumuacha mtu kama Demi hatuwezi kumuelewa hata kidogo yaan kashaharibu uzi wake maana tunamuona naye anachuki kwa Genta halafu anataka kuelimisha watu hana ajualo
Hapo ndipo ulipofikia ufahamu,na uelewa wako.
 
Utani wa simba na yanga ulijengwa kwenye misingi ya ushindani toka huko nyuma hasa uwezo wa uwanjani.

Leo utani umetoka kwenye misingi yake badala yake imekuwa mashambulizi ya mtu na mtu au kundi na mtu.
Imefika mahali chuki imekuwa kubwa hata huku mitaani.

Imefika mahali timu fulani ikikutwa na kadhia fulani au kiongozi wa timu fulani,watu wanatukanana hovyo.
Vijana wanawatukana wazee utadhani kwao hakuna wazee.

HALI HII IKIACHWA IENDELEE HUKO MBELE ITAKUWA NA MADHARA MAKUBWA KWA TAIFA.
Leo hii Haji Manara anatukanwa pande zote,mitandaoni mpk mitaani.
Je huu ni utani?

Tunajua tff imeoza haitamaniki na ndiyo chanzo cha matatizo ya mpira wetu,haiwezi kukemea timu yoyote.

JE WIZARA YENYE DHAMANA NA SOKA LETU HAIONI HAYA?

weusi wenzetu huko ulaya wakiitwa nyani sisi tunalalamika,lakini Mara kadhaa tumeona mamlaka zao zikitoa adhabu kwa timu husika ili mashabiki zao wasiendelee kubagua rangi za binaadam wenzao.

Sakata la manara kufungia,anakula matusi ya nguoni,ana baguliwa na kuitwa majina mengi mabaya kutokana na ulemavu wake,je huu ni utani wa mpira?

Serikali ipo tu!
Moja ya sheria za jamii forum ni kutomshambulia mtu bali kumjibu hoja.

LEO WAPENZI WA SIMBA WANAMKASHIFU HAJI NA KUMTUSI VIBAYA VIBAYA, MAADIMIN MPO KIMYA TU WALA HAMCHUKUI HATUA!!!!

Mfano huyu gentermycine,kwa siku anaanzisha nyuzi nyingi za kumkashifu na kumtusi Haji,lakini kesho na kesho kutwa utamkuta yupo tu humu anatembea na nyuzi zake.
MAADIMIN
Mmelala,macho hayaoni,fahamu hazifanyi kazi au?
Mpk leo hakuna tusi linalothibitishwa waziwazi kuwa Haji kamtukana Karia.

Wasemaji wanamung'unya maneno tu,wanashindwa kuyakaza,lakini wanasimba hawaoni haya wanamchafua haji,kisa alitoka kwao.
HUU NDIYO MPIRA WETU ULIPOFIKIA!!

Haji anafamilia na wazazi pia,mmejiuliza wanajisikiaje mnapomkashifu kwa kumwita sokwe mwekundu? Admin mnawaacha tu! Serikali inaacha tu!
Serikali haihusiki na masuala ya soka.... Labda kama kutakuwa na jinai.
 
Kwakweli hii nchi kuna tatizo mahala. Simba wameiheshimisha hii nchi kwa misimu 4 lakini Yanga hawajawahi kuipongeza Simba hata indirectly tu.Unadhani huo ni uungwana?

Nilifarijika sana pale Mo Dewji alipowapongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa NBCL musimu wa 2021/22 pamoja kumtukana kote kule,plus wao kutoipongeza Simba kwa misimu yote 4. Watu wa aina ya Mo ni wachache sana kwenye soka letu shithole.
 
Unamuonea bure mleta mada.Yeye peke yake hawezi kuwajua wote wanaopost upuuzi,yeye kamtaja Gentamycene,wewe taja mwingine na kile yule ataje aliyeona .Hapo tatizo litaisha.Kuna watu tuliwambia mapema kwamba Haji anakosea wakapuuza kwakuwa alikuwa upande wao Leo ndo wamekwazika na wanamuombea kila janga Haji.Hata huyu Ahmed Ally naona naye anatoka nje ya mstari,inafaa mtu asifie timu yake bila kubeza nyingine halafu tukutane uwanjani tupeane mkono tushindane.Kwa swala la Haji na Karia haki haijatendeka.Haji kama kweli alikosea angeadhibiwa kulingana na kosa lake,kwa kosa lile na adhabu ile,je angerusha ngumi ingekuwaje?

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
That's why kabla hujaandika kitu fanya kwanza utafiti angefanya utafiti angejua maana jambo linaonekana wazi kabisa kama unaingia mara kwa mara Forum lazima ungejua tu na kama haingii angetulia kabla ya kuja na hitimisho kitendo cha kumtaja mtu mmoja wakati wapo wengi huo ndio ushabiki wenyewe
Kwanini asifanye utafiti wakuwajua hao watu kuliko kumtaja mtu mmoja peke yake huoni hapo tayari kama kashamuharibia peke yake?
 
Back
Top Bottom