Kama nilivyoeleza hapo awali, mimi nimenukuu taarifa ya wizara kwamba viwango nilivyoweka ndivyo vilitumika 2012. Lakini hata hivyo, kupanga matokeo mara ya pili haimaanishi kwamba walibadilisha grading system... unless kama bado upo sekondari ukiwa lakini hata vyuo vikuu inapotokea matokeo kuwa mabaya, huwa wanafanya standardization... si kwamba wanatumia new grading system; la hasha. Hivyo basi, hata kama 2012 matokeo walibadilisha, inawezekana kabisa kilichokuwa kimefanyika ni standardization tu na sio kubadilisha grading system... hivi ni vitu viwili tofauti. Taarifa ya Wizara hii hapa:
Muundo wa Pili ni wa viwango vinavyotumiwa na Baraza la Mitihani la Taifa ambapo ambapo kabla ya mwaka 2012 muundo wa viwango nyumbufu (flexible grade ranges) ulitumika. Katika muundo huu uwigo wa alama ulibadilika badilika kulingana na hali ya matokeo ilivyokuwa kwa mwaka husika. Lakini kuanzia mwaka 2012, Serikali iliamua kutumia mfumo wa Upangaji wa Alama Mgando (Fixed Grade Range) kwa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita. Katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 Baraza lilitumia mfumo huu wa alama mgando ambapo: A = 80 100, B = 65 79, C = 50 64, D = 35 49, F = 0 34. Kwa upande wa Kidato cha Sita Baraza lilitumia mfumo wa A = 80 100; B = 75 - 79; C = 65 74; D = 55 64; E = 45 54; S = 40 44 na F = 0 39. Mifumo hii ya Baraza haikuwa inafahamika kwa wadau na hivyo kuwa sehemu ya malalamiko katika sekta ya elimu na mafunzo.