Wenye elimu ndogo ndio wanapenda kuvaa-vaa vizuri na kupendeza

Upo sahihi mkuu,tazama hata jwenye jamii zetu,wasio wasomi ndo hutaka kuvaa vizur na mavazi ya gharama
 
Unalinganisha wasanii na wasomi? I stand to be corrected
 
Hapo umelinganisha wanamuziki na wanasiasa
Jaribu kulinganisha wanamuziki wasio na elimu na wale wenye zao {walioenda shule na wale ambao hakuenda shule}
Sawa Sawa amelinganisha makundi mawili tofauti
 
mawazo mafupi na ya mgando kama haya kutoka kwa kijana mtanzania,unategemea tunaenda wapi? kuvaa ni personal choice. Ukitaka usiheshimike wala kulata kazi ya maana basi wewe nenda na kanda mbili kazini.
Kwa taarifa yako watu huangalia mtu na kumwelewa ndani ya sekunde chache sana. Je unathani sisi watu tunaangalia nini? fanyeni kazi acheni kuandika upuuzi na ujinga uliotukuka.
 
Kutumia lugha ya matusi ni ishara ya kukosa hoja ya msingi( kushindwa kujenga hoja).
Hii ni mada toa mawazo yako yanini upanic?
Haya unataka akafanye kazi kwani leo lunch amekula kwako?
 
kwanza uo mlinganisho wako sio sahihi uwezi kumlinganisha diamond na prof lipumba,diamond yuko below 30 na lipumba yuko above 60,kitu kingine waafrika wengi mna-fail kwa kukalili maisha let say we mwenye elimu kubwa una nn?,diamond ana nyumba 20 ya chin million 90 na elimu yake ndogo we mwenye elimu kubwa kwasababu mavazi kwako sio issue ume-invest nn cha zaid ya million 100?,acha kukalili maisha na kuwa fake,kuwa real
 
papa wemba alikuwa na elimu ya chekechekea kwa mujibu wa utafiti wako, siyo? maana ndiye aliyeasisi dhana ya kujipenda kimavazi kwa kuyafanya rafiki kwani humsindikiza mvaaji hasi kaburini. hatahivyo umewaza vema kwa ujumla lakini tutoke nje ya mipaka pia mlinganisho wa tasnia mbili tofauti; sanaa na siasa hazitatuletea matokeo yasiyoacha shaka.
 
Kama kuna ka ukweli kidogo lakini
Sio KAUKWELI mkuu, LIUKWELI. Mara nyingi, mtu mwenye kupungukiwa na kitu ambacho hata yeye anatambua kuwa kingempa status, huwa anatafuta kitu kingine anachokimudu kufidia.

Ninaye rafiki yangu ambaye ana tatizo hili. Anajipiga mashati ya mikono mirefu, miwani na kalamu saaaafi mfuko wa shati. The way anaongea akiwa nyumbani na mkewe ni tofauti na anavyoongea akishapiga hizo pamba zake za kuendea kibaruani.
 
Reactions: kui
Usomi ndo nini kwanza? Na wewe ni mmoja wa hao wasomi?
 
Chizi nae kafanya utafiti,kazi ipo. Na kazi inakuwa kubwa zaidi ukiangalia hao watu aliojaribu kuwaringanisha kwenye utafiti wake,eti wasanii wa muziki (ambao muonekano kwao ni kitu cha msingi sana) na wanasiasa.
 
Umepanic brother! Cool down. Hajasema yeye ana elimu kubwa, na ndio maana hakujitolea mfano. Yawezekana kakosea mlinganisho, lakini hajakosea logic.
 
Ha ha ha ha.. umenichekesha mkuu

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Kuvaa vizuri hakuna uhusiano wowote na kiwango cha elimu ya mtu. Kuna waliosoma kwa kiwango cha juu kabisa wanajipenda sana na kupiga pamba mwanzo mwisho na wengi pesa wanayo hivyo wanamudu manunuzi ya nguo nzuri na za bei mbaya.

 
Chizi nae kafanya utafiti,kazi ipo. Na kazi inakuwa kubwa zaidi ukiangalia hao watu aliojaribu kuwaringanisha kwenye utafiti wake,eti wasanii wa muziki (ambao muonekano kwao ni kitu cha msingi sana) na wanasiasa.
kuwaringanisha = kuwalinganisha.

Hata mwanasiasa muonekano wake naye ni kitu cha msingi.
 
"Wasomi nguli" una maanisha nini?
Unguli upo wapi kama profesa mzima aliachia ngazi mwenyewe na leo anataka tena uenyekiti.Kama usomi nguli ndo huo sitatamani uzao wangu wote wawe wasomi.
 
Ni aina ya maisha waliolelewa!
Wasomi wengi wenye level za juu tz kama phd na professors wamezaliwa ktk familia za chini saana kwani watoto wa familia bora wengi wao hawataki kupoteza mda sana ktk elimu badala ya kusimamia biashara za wazazi wao kama vile Mo Dewij, Omary Bakhresa ukiwaangalia dress code zao ni modern sana but kwa wale wa familia maskini wameshazoea kuvaa ili mradi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…