SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 3,577
- 5,664
Wapendwa wamiliki wa Guest House na Lodge kote nchini,
Kwa heshima zote, nyenyekevu, na kwa maumivu ambayo hayawezi kuelezwa kwa lugha ya kawaida, tunawaomba kwa moyo wa dhati MUONDOE MAGRILL MADIRISHANI!
Hili siyo ombi la kawaida. Huu ni wito wa dharura kutoka kwa sisi watu wa vishughuli vya kimya kimya, siye ndo wale tunaoingia saa nne usiku tukiwa na mademu ambao wana ndoa zao kamili kabisa huko mtaani.
Sisi siyo malaika, lakini hatustahili kunyimwa njia ya kujiokoa pale mambo yanapoharibika ghafla.
Ni haki ya kibinadamu kujinusuru! Si ndiyo jamani?
Sasa inatokea mnampendana na mwanamke baadaye unajua ni mke wa mtu,,, na si mnajua penzi la wizi lilivyo na midadi... kila ukitaka kumwacha, demu anadai anakupenda kuliko hata mme wake.
Sasa siku inatokea mnaenda kula raha zenu,,,,, mnaingia chumbani, mnachangamkia penzi kwa bashasha zote. Ghafla bin vuu! Gari inasimama nje, kuna mlango unagongwa, kuna sauti ya vidume wenzio kam 10 vurugu tupu, unaskia: “Fungua! Najua upo na mke wangu hapo!”
Ukiangalia dirisha unakutana na vyuma,,, unakuta mtu mzima unajificha chini ya kitanda, jasho linakutoka kwa kasi ya ajabu, huku ukijiuliza:
“Kwa nini hawa jamaa waliweka grill hadi chooni?
Huu siyo usalama, huu ni mtego wa kifedhuli!