ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Jana nipo kijiweni kwetu na washkaji tunapiga story za MO jamaa mmoja akaanza kuhadithia jinsi zamani watu tulivyokuwa tunaogopa magari ya msalaba mwekundu Mara wanyonya damu Mara wachuna ngozi akaendelea kusema hata Sasa tutafika Zama hizo za kuishi kutekana.kwamba mwili wa binadamu ni deal Sana kuanzia viungo vyote na kwamba majambazi hao wakikuchukua wanachomoa kimojawapo Kama ni Figo au ini au sehemu za Siri wanapita hivi kwenda kuuza.halafu huku mtaani zinabakia tu story mara serikali mara sijui nini mara sijui utakuwa umejiteka ila ndo hivo utakuwa ushatangulia kinyama.toka asimulie hayo mambo Mimi pressure sijui ndo imeshuka nahisi kabisa moyo unasukuma damu taratibu Sana .usiku silali vizuri Wala Sina hamu ya kula.mawazo ni mengi Sina raha