Wenye kutuma maudhui machafu mtandaoni nchini kukamatwa

Wenye kutuma maudhui machafu mtandaoni nchini kukamatwa

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
620
Reaction score
1,240
π—§π—”π—‘π—­π—”π—‘π—œπ—” π—ͺπ—˜π—‘π—¬π—˜ π—žπ—¨π—§π—¨π— π—” π— π—”π—¨π——π—›π—¨π—œ 𝗠𝗔𝗖𝗛𝗔𝗙𝗨 π— π—§π—”π—‘π——π—”π—’π—‘π—œ π—žπ—¨π—žπ—”π— π—”π—§π—ͺ𝗔

1_20250107_095621_0000.png


Ongezeko la watumiaji wa intaneti Tanzania imezongezeka kutoka mwaka 2023 kwenda 2024/2025, huku zaidi ya watu Milioni 33.3 wanatumia intaneti ni sawa na asilimia 53.5% ya watu wote waliopo Tanzania.

Ongezeko hilo limepelekea watu wengi kutengeneza maudhui mbalimbali mtandaoni ili kujipatia pesa au kuburudisha jamii, wengine kuhelimisha nk lakini asilimia kubwa ya watumiaji wengi wa kitanzania wamekua wakituma maudhui ambayo sio mazuri kabisa.

2_20250107_095621_0001.png


Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum Dkt. Dorothy Gwajima amekemea vikali wimbi la maudhui yasiyofaa mtandaoni yanayosambazwa yakionyesha baadhi ya mambo yasiyofaa.

Dkt. Gwajima amesema mfano kuna mtu alionekana kwenye mitandao ya kijamii akisambaza maudhui ya kuuza figo za mtoto, mwingine anamuuza mtoto, mwingine akionyesha kuandaa vinywaji na vyakula vichafu na kuwauzia watu mbalimbali maeneo ya k/koo.

Maudhui mengine ni wale wanaotuma kuonyesha watu wanafanya mapenzi ya jinsia moja, wengine wakitangaza fursa za kupiga hela mtandaoni kumbe utapeli. Hivyo Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wanaoandaa maudhui mtandaoni kuandaa maudhui ambayo ni manufaa kwa jamii.

Sio kila mtu wa kuandaa maudhui wengine hawana hata Elimu lakini ilimradi na yeye hatume tu taarifa mtandaoni aache mara moja.
 
polisi wakiwa wanamtafuta mtu mwengine huonekana wazembe ila wakutafute wewe sasa!, ukisikia hata sufuria limedondoka unajua tayari wamefika, endelea kusema porojo na hujawahi kuvunja hata sheria...πŸ˜ƒ
Hawajawahi kuwa serious na haya mambo
 
Dkt. Gwajima D fungieni mtandao wa Tiktok huu ni balaa jingine zaidi.
Kule watu wanakuwa live wakifanya mambo ya ajabu mfano tu kuna dada alikuwa live saa7 usiku anatoa no zake kwa wateja kuwa anauza kinyume na maumbile yake.Mbaya zaidi anawaonyesha namna atakavyokatika ukimpa 15k au50k mkatiko ni tofauti.
 
Asante sana Mhe.Waziri. Nimejaribu mara nyingi kuondoka Chaputa ikawa kama mbio za panya zinazoishia sakafuni. Kwa hatua hii utakuwa umenisaidia sana.
 
Maudhui machafu ni pamoja na kampeni za Lissu zizuiwe mara moja..anamchafua Mwenyekiti 🐼
 
Vipi kuhusu hizi bongo movie pamoja na miziki ya kibongo. Vipi kuhusu maudhui ya picha tunayo yaona live huko duniani wadada wakitembea uchi na wavulana wakika kidada kidada na mionekano ya kike kwa kisingizio cha usanii?
 
Back
Top Bottom