Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

[emoji2][emoji2][emoji1][emoji1][emoji16][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]loohh!hii Kali kulikoo!!
 
miimi mzee wangu alikuwa hataki hata rafiki wa kiume yani anataka akuon wewe mwenyewe tu alikuwa ana neno moja marafiki wote ni wahuni
Nimegundua hawa wazee wametoka ukoo mmoja ninyii
 
Nakumbuka miaka ya 2001 mama alikwenda Dar .
Sasa huku nyuma alimiacha mimi na ndugu zangu wa 3 .
Hapo njee kulikuwa na maua sasa mimi wakati wa kumwagilia nikawa nacheza na matope basi bwana baada ya hapo baba aka rudi home mida ya saa 5 usiku nusuru adondoke na jinsi nilivyochezea matope haloo mzee akaniamsha na kunihoji nami nikakubali ni kweli mzee nilichezea.


Mzee aliniweka mipira ile ya kuchotea maji haina idadi akaona haina maana ananipaka chumvu mwili mzima asiee
Alikuwa kama anachana na mikanda na alikuwa na mkanda upo na vi (viuvingo)Β²

Niliwekwa kinoma na hapo nilikuwa nimetoka kukata gogo aisee mzigo ulichotwa na nikamwagiwa live aisee hii siwezagi kuisahau na yeye sikuwahi kumweleza maana alinipiga na alinionea sana .

Mzee mpaka now anaakili sana na namkubali all because mpaka now siwezi kurudi home mida ya usiku kama sina ishu.

Nipo na self discipline kali sana.
Siwezagi kuvaa mlegezo kama watu wazima wenzangu wanavyofanya .

All in all bado namkubali sana even though alikuwa mtata hata kwa mama anawekwa mpaka kulazwa .
 
Uliona kama anakuonea hivi, ili baada la kupevuka kiakili ukaona mzee alikuwa sahihi
 
[emoji1787][emoji1787]
 
Madingi wanaokubali kupelekewa wajukuu hao si wakali, wale wababe wa vita mjukuu akija asalimie na kusepa, hawana muda wa kulea mtoto na mjukuu!
Wengine wanapiga simu wanasema tuletee wajukuu kesho, hakuna mjadala hapo.
 
Unasema mzee wako alikumwagia mavi?
 
Si wa kwetu kuanzisha tifu sometimes ilikuwa sio lazima ukosee. Alikuwa na uwezo wa kupiga nyumba nzima kisa mdogo wenu kafanya kosa na nyie mpo. Na alikuwa anaamini hisia zake sana, akihisi umezingua lazima uchezee kichapo hadi ukubali. Na akikuchapa anapomalizana na wewe lazima useme asante vinginevyo adhabu inaanza upya
 
Aisee
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mzee wangu tulimpa majina mengi sana, farasi mweupe, mkoloni, mjerumani etc. Hii haitoshi kuonesha ukali wake ukizingatia alikua afisa mkubwa wa jeshi, nidhamu kwake ndio ilikua kila kitu aisee tumepigwa sana. Mzee sijui nimuelezee katika tukio gani jamani.
Kuna kipindi miaka ya zamani kidogo nikiwa darasa la sita/saba, kuna gazeti linaitwa alasiri walianzisha tabia wana chapisha mitihani ya majribio halafu kesho yake wanachapisha majibu. Hii nitakuja kuielezea pamoja na ile nilirusha baruti (ya plug) nyuma ya chumba cha mzee ukasikika mlio kama bomu [emoji2][emoji2], moto wake ni balaa.
Au sijui nihadithie ile ya mzee kuja kunikung'uta assembly shuleni makongo mbele ya wanafunzi wenzangu wote? Sema respect sana mzee wangu. I am who I am today because of you

Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
 
[emoji23]
 
Yani we unachapwa kistaarabu
Bi mkubwa alikuwa anafanya shambulio
Siyo kuchapa utapigwa bakora kila mahali na ikiisha ni vifinyo unashikwa maskio unainuliwa yananyongolotwa kama yanang'olewa vile hadi yanakuwa kama yanawaka moto utang'atwa, mangumi yani ni shambulio kwakweli ukitoka hapo umeiva

Nimekujagundua mama alikuwa na stress tu nampenda namuombea aishi sana

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Unachezea kichapo heavy na shukran unatoa [emoji23][emoji23]
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…