Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 76,039
- 230,142
Hawezi na hakuna sababu ya kufanya hivyo.Basi shem atakubonda soon
Haaa Yan wewe kama mimi tu hivyo, na. Mzee alikuwa Mjeda pia mwenye heshima yake, kukuabisha popote haoni aibu. Makongo pia nilipitaMzee wangu tulimpa majina mengi sana, farasi mweupe, mkoloni, mjerumani etc. Hii haitoshi kuonesha ukali wake ukizingatia alikua afisa mkubwa wa jeshi, nidhamu kwake ndio ilikua kila kitu aisee tumepigwa sana. Mzee sijui nimuelezee katika tukio gani jamani.
Kuna kipindi miaka ya zamani kidogo nikiwa darasa la sita/saba, kuna gazeti linaitwa alasiri walianzisha tabia wana chapisha mitihani ya majribio halafu kesho yake wanachapisha majibu. Hii nitakuja kuielezea pamoja na ile nilirusha baruti (ya plug) nyuma ya chumba cha mzee ukasikika mlio kama bomu [emoji2][emoji2], moto wake ni balaa.
Au sijui nihadithie ile ya mzee kuja kunikung'uta assembly shuleni makongo mbele ya wanafunzi wenzangu wote? Sema respect sana mzee wangu. I am who I am today because of you
Sent from my CPH2059 using JamiiForums mobile app
mshua alikuwa Mjeda pia tulimbatiza jina la mzee Mbuzi hatari sanaHaaa Yan wewe kama mimi tu hivyo, na. Mzee alikuwa Mjeda pia mwenye heshima yake, kukuabisha popote haoni aibu. Makongo pia nilipita
Daah, kweli mkuu. Basi bila shaka tuliishi wote barracks either area A/CHaaa Yan wewe kama mimi tu hivyo, na. Mzee alikuwa Mjeda pia mwenye heshima yake, kukuabisha popote haoni aibu. Makongo pia nilipita
Hahahaha aisee huyu Ni Mimi kabisaaaa yaaniDingi ya jamaang, marehem mzee kadege alikua OCS au OCD kpnd hicho, kulala sero, kutandkwa na msauz/fimbo itumiwayo kuadhb waarfu polic ilikua kawaida kwa jamaang na kakazake. Sku moja mwaka 2001 katka kucheza cheza tukiwa na kbert cha ges, ambach jamaang uyo alimwbia mzee wake uyo uyo, tuliwasha moto fensi ya almashaur ilyokua imeungana na fensi ya hosptal ya wilaya, fens ilkua imepgwa seng'enge uku ikwa imepandwa mit na maua mbalmbal, meng yalkua yamekauka kwan ilikua n kiangaz. Nasema iv bila watu kuingilia kat na kumchomoa jamaang mikonon mwa yule mzeee naamn jamaang angekua marehem leo, kipgo alchopata ilbd tu alazwe. Pia nashukuru Mungu jithada za raia wema walfanikwa kuuzima moto ule japo ulileta madhara kias, miaka iyo zimamoto ilkua mkoan tu uku wilayan hazkuepo kabsa
Haswaa na wazee Kama Hawa kukisanua Ni muda wowote ule halafu huwaga Wana tabia ya kukuona Kama vile mzembe na mpumbavu tu kwakemshua alikuwa Mjeda pia tulimbatiza jina la mzee Mbuzi hatari sana
DHU, mshua wako alikua mwanariadha? maana sio kwa kushindana mbio na mtoto na kumkamataMzee alikua anasema kama unajiona upo vizuri njoo tuzipange.
Alikua hapendi mtu anyoe kipara, kaka yangu akawa mbishi siku hiyo karudi home na kipara. Mzee akamwambia kimbia ukiona upo mbali sema tayari.
Jamaa akakimbia mzee anaona mdau anasogea tu hasemi tayari, akamuungia. Dakika kadhaa mbele tunaona kaka anarudishwa kabebwa begani.
Kufika home akaambiwa tuzipange, ghafla jamaa kapiga magoti analia anaomba msamaha.
Mzee akamwambia adhabu yako utakua unapaka kiwi kichwa hadi nywele ziote.
Majani ya ng'ombe au mboga za majani?Mi nadhani Mzee wangu ndo mkali kuliko wote Tz. nakumbuka mwaka 2002 nilikuwa napenda sana kusikiliza mikanda ya kaseti, siku moja redio ikawa imekorofisha nikaona isiwe taabu nikachukua bisibisi nikaifungua, nilivyoifungua ndo nikawa nimeharibu zaidi alivyorudi jioni kutoka kazini aliyeharibu redio nani nikatajwa mimi nilipewa adhabu ya kula majani pamoja na maziwa pamoja na fimbo kumi na nne kwa muda wa siku mbil.
Kwa hii story nawaza watoto wako wakizingua itakuwa vipi, maana ni mtu wa action, hutaki ujinga na huna regretsMimi nakumbuka siku ya mwisho dingi kunichapa.....alinikuta nasoma saa sita usiku yeye yuko nzwiiiii......akaniuliza kwa nini sijalala, nikamjibu huoni nafanya nini.....akajaa povu....akafuata fimbo kwani alikuwa anaziweka sehemu......akaanza kunitandika......nilitulia tuu, ila ikafika wakati nikasema leo lazima nimuonyeshe huyu mzee......niliikamata ile fimbo na nikaivunja vipandevipande.....kulikuwa na music system ya Phillips niliifuata na nikaivunja vipande vipande.......nikaenda kwenye kabati la vyombo....nililiangusha na almost vyombo vyote vya udongo vilivunjika.......ndio ilikuwa mwisho wa mzee kunichapa......
Alihisi kashaua brotherdingi angu alikuwa mkali balaa, nakumbuka kuna siku nilichelewa kurudi home, ile kuingia ndani tu nakutana nae, akaniuliza," unatoka wapi" nikaanza kumung'unya maneno kwa woga, alinizaba kofi moja nikaanza kuhisi nyota nyota, wakati nikiweweseka alinichota mtama nikapaa kimo cha ndama, pembeni kulikuwa na beseni kubwa lina maji nikadondokea mule, pwaa! sikujitambua tena, kuja kushtuka siku ya pili nipo hospitali, ila tangu siku hiyo hakunipiga tena
Aisee nimecheka sana hii story noa sana, yani dingi wako ana akili kweli maana kawafundisha kumuheshimu mke wako, hakutaka kuwadekeza kawafundisha kutafuta vya kwenunyinyi nyote trella... dingi yangu maarufu sana maeneo ya yombo kila mtu hadi majirani wanamuongelea enzi zake.. kuwa alikuwa hatari...
enzi hizo dar bado wenyeji wengi mitaa ya uswahilini kuna ngoma za wamakonde na wazaramo kibao....
kuna siku wazaramo walipita na kigodoro chao mchana nje ya ukuta dingi alikuwa anapalilia majani... wazaramo kibao kama 200 hivi.. dingi akawasimamisha.. na kuwauliza hivi kila kabila hapa likisema lipige ngoma yake si itakuwa balaa.. akawaambia ngoma za wazaramo kwa mchaga, mkurya, mnyakyusa, mhehe etc ni usumbufu.. kama wanataka ngoma wakapigie kwao msanga huko ambapo hakuna makabila mengine... wazaramo wakacharuka si unajua wanaongea sana wakaanza msuta dingi... mzee akajifanya amezidiwa.. akawaambia amependa hoja zao wamsubiri awaletee zawadi ya mwali wao...
wale wazaramo walivyo wajinga wakamsubiri kweli... dingi kazama ndani.. chumbani kwake kachukua gobole lake... kilichotokea ilikuwa story yombo mzima hakuna ambaye haijui..... dingi alivyotoka tu nje na gobole wakaanza kimbia na wapiga ngoma wakaacha ngoma zao.. dingi akazigeuza zile ngoma ni mafunzo ya kulenga shabaha... zile ngoma kubwa akazitia risasi zote.. na gobole lina kelele balaaaaa... mtaa mzima ndanii.. yeye anazitia shaba tu.
hawakurudi tena na ngoma zote zikawa zinapita mtaa wa pili.. hazipiti njia ya kwetu wanaogopa mwanajeshi mstaafu
dingi alikuwa anatubondaaa hadi mama analia yeye...
anakwambia ndani ya nyumba rafiki yake mke wake tu.. ana gari lake land rovee ukiingia humo huruhusiwi kukaa kiti cha mbele ni cha mke wake tu mama yetu.... na hata ukikaa siti ya nyuma ukipigwa wimbo mzuri huruhusiwi kutikisa kichwa anakushusha... enzi hizo watoto wake alikuwa anatushusha kwenda kanisani eti tunatikisa kichwa kwenye gari lake tukisikia mziki mzuri.. so kanisani inabidi twende kwa mguu.. yeye na mama ndio kwenye gari
hahaha , wanawake wengi huamini wanachosikia hata kama akili yake inamwambia unadanganywa mara nyingi huamua kumuamini .nikisema nihadithie yote humu mtachoka.. mzee alikuwa mkoloni hatari... majirani wanamuita mjerumani ila wanamkubali kichizi... unakuta msiba wa jirani au sherehe ya jirani... wakiwa wanabishana bishana kufikia uamuzi wa pamoja... wanamuita mzee kwenye kikao awasaidie kufanya maamuzi.. kwanza cha kwanza anawaomba wanawake wote wanyamaze na wabaki wasikilizaji.. kisa anaongea na wanaume wenzake jinsi marehemu asafirishwe vipi au azikwe wapi.. na hapo marehemu sio ndugu yake.. ila majirani tu wamemualika.. mzee haaamini kabisa wanawake kama wana akili.. dada yangu alipata div 1.8 form 4 na point 5 pcm marian.. ila mzee hawezi mtuma kitu chochote serious anasema akili za wanawake rahisi kutapeliwa... huwa hawawazagi mambo kwa upana hata kama wamesoma sana
Na imani hata ukipata kazi jeshini haitokuwa shida maana kawafundisha kuwa waadilifuSi wa kwetu kuanzisha tifu sometimes ilikuwa sio lazima ukosee. Alikuwa na uwezo wa kupiga nyumba nzima kisa mdogo wenu kafanya kosa na nyie mpo. Na alikuwa anaamini hisia zake sana, akihisi umezingua lazima uchezee kichapo hadi ukubali. Na akikuchapa anapomalizana na wewe lazima useme asante vinginevyo adhabu inaanza upya
Dhu kwanini alimkata masikio mtoto wake?Ngoja nami niandike mambo kadhaa ambayo yamenifanya niamini hakuna mzee kama mzee wangu.
1. Siku moja tumeenda kwenye ngoma masikini nikaongozana na dada zangu kwenda huko mzee alikuwa yupo safarini akarudi akakuta milango yote imefungwa na kuku wapo nje yaani full tafrani hapo nje, wazee wa ngoma tukaingia kwa mbwembwe shikamoo baba!!! Hahahha tukafungua mlango kuku wakaingia ndani msosi ukapikwa na watu wakala.
Dingi yupo kimya tu anasoma mchezo nikamaliza kula nikawa naenda kulala kidume nikaitwa njoo hapa unaenda wapi nikamjibu kulala akasema toa godoro lako likunje, nikakunja godoro vizuri nikamaliza akasema liweke chumbani kwangu nikapeleka chumbani godoro haya nenda ulale. Bwana wee Kitanda cha chuma hakina kitu nikafika kidume nikalala kwenye vyuma kwa usimamizi wake hadi majira ya saa 8 hivi nagalagala kwenye vyuma, ngozi imeweka alama kama nimechapwa bakora aiseeee. Wale dada zangu wenyewe walifungwa juu ya kenchi usiku kucha hadi asubuhi, Asubuhi niliamka poa tu nikakanda mwili vizuri nikaendelea na majukumu ya utoto.
2.Kuna mdogo wangu alikatwa masikio.
3.Vikojozi walikuwa wanalala kwenye mfuko, wanaingizwa humo usiku kucha watatolewa asubuhi.
Hakuna kusema neno NITAKUPIGA hata kama ni kwa mdogo wako akisikia hilo neno ni kipigo Heavy kwa aliyesema "alikuwa anadai yeye ndiye mwenye uwezo wa kupiga kwenye ule mji".
Ukizira kula jiandae kula kwa lazima na chumvi ikizidishwa maradufu kwenye mboga chini ya usimamizi wake.
Kuchomwa kwa mvuke ilikuwa kawaida sana kwetu.
Ukipigwa haja kubwa isitoke shukuru Mungu kipigo cha siku hiyo.
Aliwahi kukunja mzazi mmoja ngumi hadi kwenda polisi (ila hiii sisemi).
Nilikuwa nafata maji usiku saa mbili kisimani ambapo ni zaidi ya km 2 pekee yangu nikiwa under 10 years.
Nipo safarini nikifika nitawaambia watu wa Tanga nipokeeni hapo stand. Nipo kwenye basi la Simba Mtoto natokea Isamembwe.
hahaha ila hapa ulizingua mkuu, kweli akili za utotoNakumbuka nilikuwa napenda sana kutengeneza manati.sasa kama mnavyojua manati yanatakiwa yawe na like kingozi cha kushikia jiwe,na lazima kiwe kilaini.sasa bwana huku na huku nikatafuta ngozi bila mafanikio.akili ikanituma nikakate kiatu cha baba anachokipenda kuliko vyote.kilichotokea alivyorudi huwa ctak kukumbuka maana alinipa kichapo kiwango cha lami.
hujamkuta akiwa na wajukuu zake wanavyodekezwaHahaha,
Nimerudi likizo nimekuta madogo wanajiachia mpaka nikashangaa.
Wakati enzi zake shua mkisikiagari getini tu, hata kama kuna kikaratasikidogokikochini inabidi kiokotwekitupwe kwenye jaa, ama sivyo kinaweza kuzua kesi kubwa sana.
Mpaka juzi nikoofisini, kukawana kikaratasi kidogo kwenye carpet, sikuweza kuvumilia nikakiokota na kukitupa kwenye bin.
Discipline ya mshua hiyo.
Lakini kama ulivyosema, ukimkuta sasa utamhurumia.
Ameen, uzidi kumpa faraja, kumnunulia zawadi na kumjulia hali mara kwa maraYani we unachapwa kistaarabu
Bi mkubwa alikuwa anafanya shambulio
Siyo kuchapa utapigwa bakora kila mahali na ikiisha ni vifinyo unashikwa maskio unainuliwa yananyongolotwa kama yanang'olewa vile hadi yanakuwa kama yanawaka moto utang'atwa, mangumi yani ni shambulio kwakweli ukitoka hapo umeiva
Nimekujagundua mama alikuwa na stress tu nampenda namuombea aishi sana
Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
mama je?Sijawahi kupigwa na baba nikiwa nyumbani.