Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji109]
 
Siku nimeiba chupa ya bia (Safari Lager) ya mshua nikauza nikaenda video...nilivorudi usiku nilitamani ardhi ipasuke nitumbukie...nilipata cosovo almanusura kulazwa....nikikumbuka huwa namwona dingi mkatili kinoma....
 
Enzi hizo nasoma form six nimerudi likizo! Kuna demu mmoja alikuwa anapenda kupita pita mitaa ya nyumbani ili aninase....basi kumbe jana yake kwenda kutazama mechi za eufa kumbe wadogo zangu nao walitoka pale nyumbani kukawa hakuna mtu wa kufungua geti! Basi mzee alivyorudi alipiga honi alivyoona hakuna response yoyote akaamua ashuke na kufungua geti mwenyewe! Basi bwana kesho yake si ndio akanifuma namaliza na yule demu ili niokoe mzigo. Duh kilichotokea pale siwezi kukisimulia ila ni zaidi ya fedheha.
 
Duh!! Hii itakuwa kanda ya ziwa km ckosei
 
We ni shida
 
True yani huwa najiuliza sana.. yeye alikua anajiita kiboko y a wajinga ila huyu dogo hapa anamnyoosha ipasavyo
 
hahahahahahahahhahaha mzee wangu fair sana nakumbuka baada ya kutairiwa ananiambia unaona icho kichwa ndio kinachomtoa chozi mwanamke kwa utamu huko kwingine hakuna ishu kabisaaa ndio maana nimekutairi.....mengine baadae nitaandika hapa
 
Haaaaa haaaaa....JF duuuh
 
utawaonea hadi huruma maana akijipindua kafinywa akikaa vibaya kakojolewa basi full lawama tu...utamsikia yani huyu hana tofauti na baba ake
Hahaha,

Nimerudi likizo nimekuta madogo wanajiachia mpaka nikashangaa.

Wakati enzi zake shua mkisikiagari getini tu, hata kama kuna kikaratasikidogokikochini inabidi kiokotwekitupwe kwenye jaa, ama sivyo kinaweza kuzua kesi kubwa sana.

Mpaka juzi nikoofisini, kukawana kikaratasi kidogo kwenye carpet, sikuweza kuvumilia nikakiokota na kukitupa kwenye bin.

Discipline ya mshua hiyo.

Lakini kama ulivyosema, ukimkuta sasa utamhurumia.
 
hhahahahahahahahahahahahahaha leo mmenichekesha sana kwa kweli hahahahahahaha
 
Nimesoma comments zote hakuna anayemfikia mshua wangu kwa ukali hadi sasa hivi bado ni kimeo tuu
 
hao wazee wote mnaiwataja hapa hamna kitu asee nakumbuka mwaka 84 ilikua jumamosi mzee akatuagiza majani ya kuku tulikua na kuku wengi sana yeye akaenda kazini ..tulivyoenda tulikaa mpaka saa nane au tisa hivi ndo tukarudi na mizigo yetu ya majani ya kuku watu wa arusha wanayafahamu majani ya sungura..bwana kumbe mzee alikua amesharudi na ameenda kutafuta chakula cha kuku mwenyewe....

Kwakuanzia tuliambiwa kila mtu ale mzigo wake coz tuna njaa na kuku wameshakula hamna pa kuyapeleka...kwa jinsi alivyokua tukaanza kupiga mdogo mdogo tulikua watatu...kaka yangu akaleta ukorofi mzee alimtia kwenye gunia la kuhifadhia kahawa akalifunga kwa juu asee alimtia fimbo zisizo na idadi ..akamtoa kwenye gunia akamtia fimbo kavu kavu mpaka vijiti vikamwingia kama miba then akamfingia kwenye mti wa mlimao kwa minyororo kwa siku 3 day and 9t tulikua tunampelekea msosi kwa siri usiku na alivyotoka hapo ni kumuuguza na kumtoa vijiti mwilini......

pia nakumbua dada yetu mkubwa aliwahi kumpiga mdogo wake mama akamsemea mzee alimpiga then akampeleka kwe ng'ombe zizini akamwambia akae huko siku saba kwasababu anatabia za ng'ombe...kuna matukio mengi sana mfano akikupangia kazi usipifanya mfano ya shamba akirudi hata kama ni saa nne usiku utaenda kulima ...alikua anaogopwa mpaka na mabosi wake
 
[emoji1][emoji1][emoji23][emoji23][emoji23]mkuu huyu mzee bado yupo hai kwelii

amefariki mwaka jana akiwa na miaka 79.. ila mpaka uzee wake hadi wajukuu walikuwa wanamuogopa.. anacheza nao ila akiamua anawatia viboko..

kuna mjukuu aliua kuku wa nyama... mama anafuga kuku sasa kuna siku wanawapa kuku dawa kuna mjukuu akaenda kumkamata kuku wa nyama bahati mbaya akamnyonga mzee alikuwepo jirani akaenda mtia fimbo mjukuu hadi mama yake mke wa kaka akataka kulia... bro akamwabia kama unataka kulia kalilie chumbani maana mzee akikuona unalia hapa anaweza anzisha ugomvi mzito na usikanyage tena hapa
 
Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
mzee wangu ukimtibua aisee anakua mkali kinoma

kwanza sitosahau tuko madogo tulikua na tabia ya kuzurura kitumbo waz bila ndala aisee halafu mzee alikua na cheo tu dah alikua anamind tunamzalilisha
siku hio akatuona live na mdogo wangu kama kawaida kitumbo wazi kufika home tunashangaa milango inafungwa tukajua leo kiama chetu kimefika akajikagua akaona hajavaa mkanda akaona hakijaharibika kitu aisee alituchapa ngumi na mikanda na mdogo wangu tangia siku hio mm ni tawiree tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…