Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

nikisema nihadithie yote humu mtachoka.. mzee alikuwa mkoloni hatari... majirani wanamuita mjerumani ila wanamkubali kichizi... unakuta msiba wa jirani au sherehe ya jirani... wakiwa wanabishana bishana kufikia uamuzi wa pamoja... wanamuita mzee kwenye kikao awasaidie kufanya maamuzi.. kwanza cha kwanza anawaomba wanawake wote wanyamaze na wabaki wasikilizaji.. kisa anaongea na wanaume wenzake jinsi marehemu asafirishwe vipi au azikwe wapi.. na hapo marehemu sio ndugu yake.. ila majirani tu wamemualika.. mzee haaamini kabisa wanawake kama wana akili.. dada yangu alipata div 1.8 form 4 na point 5 pcm marian.. ila mzee hawezi mtuma kitu chochote serious anasema akili za wanawake rahisi kutapeliwa... huwa hawawazagi mambo kwa upana hata kama wamesoma sana
Hahahahahhahahaha kweliii huyo alikuwa mjerumani
 
nyinyi nyote trella... dingi yangu maarufu sana maeneo ya yombo kila mtu hadi majirani wanamuongelea enzi zake.. kuwa alikuwa hatari...

enzi hizo dar bado wenyeji wengi mitaa ya uswahilini kuna ngoma za wamakonde na wazaramo kibao....

kuna siku wazaramo walipita na kigodoro chao mchana nje ya ukuta dingi alikuwa anapalilia majani... wazaramo kibao kama 200 hivi.. dingi akawasimamisha.. na kuwauliza hivi kila kabila hapa likisema lipige ngoma yake si itakuwa balaa.. akawaambia ngoma za wazaramo kwa mchaga, mkurya, mnyakyusa, mhehe etc ni usumbufu.. kama wanataka ngoma wakapigie kwao msanga huko ambapo hakuna makabila mengine... wazaramo wakacharuka si unajua wanaongea sana wakaanza msuta dingi... mzee akajifanya amezidiwa.. akawaambia amependa hoja zao wamsubiri awaletee zawadi ya mwali wao...

wale wazaramo walivyo wajinga wakamsubiri kweli... dingi kazama ndani.. chumbani kwake kachukua gobole lake... kilichotokea ilikuwa story yombo mzima hakuna ambaye haijui..... dingi alivyotoka tu nje na gobole wakaanza kimbia na wapiga ngoma wakaacha ngoma zao.. dingi akazigeuza zile ngoma ni mafunzo ya kulenga shabaha... zile ngoma kubwa akazitia risasi zote.. na gobole lina kelele balaaaaa... mtaa mzima ndanii.. yeye anazitia shaba tu.

hawakurudi tena na ngoma zote zikawa zinapita mtaa wa pili.. hazipiti njia ya kwetu wanaogopa mwanajeshi mstaafu

dingi alikuwa anatubondaaa hadi mama analia yeye...

anakwambia ndani ya nyumba rafiki yake mke wake tu.. ana gari lake land rovee ukiingia humo huruhusiwi kukaa kiti cha mbele ni cha mke wake tu mama yetu.... na hata ukikaa siti ya nyuma ukipigwa wimbo mzuri huruhusiwi kutikisa kichwa anakushusha... enzi hizo watoto wake alikuwa anatushusha kwenda kanisani eti tunatikisa kichwa kwenye gari lake tukisikia mziki mzuri.. so kanisani inabidi twende kwa mguu.. yeye na mama ndio kwenye gari
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Mwaka 99, enzi hizo simu ya mezani, alikuja mgeni akaomba simu apige hapo simu inakaa chumbani, nikamwambia dingi mgeni anaomba simu, dingi akaguna tu nikajua kakubali nikatoa simu mgeni kaongea alivoondoka mweh!!!!
Nlichezea kichapo heavy yani mvua ya stiki..... Apumzike kwa amani mdingi
[emoji1][emoji1][emoji1] ukome kujifanya maza Theresa!
 
nikisema nihadithie yote humu mtachoka.. mzee alikuwa mkoloni hatari... majirani wanamuita mjerumani ila wanamkubali kichizi... unakuta msiba wa jirani au sherehe ya jirani... wakiwa wanabishana bishana kufikia uamuzi wa pamoja... wanamuita mzee kwenye kikao awasaidie kufanya maamuzi.. kwanza cha kwanza anawaomba wanawake wote wanyamaze na wabaki wasikilizaji.. kisa anaongea na wanaume wenzake jinsi marehemu asafirishwe vipi au azikwe wapi.. na hapo marehemu sio ndugu yake.. ila majirani tu wamemualika.. mzee haaamini kabisa wanawake kama wana akili.. dada yangu alipata div 1.8 form 4 na point 5 pcm marian.. ila mzee hawezi mtuma kitu chochote serious anasema akili za wanawake rahisi kutapeliwa... huwa hawawazagi mambo kwa upana hata kama wamesoma sana
Daah we jamaa bhana.
 
Mwaka 99, enzi hizo simu ya mezani, alikuja mgeni akaomba simu apige hapo simu inakaa chumbani, nikamwambia dingi mgeni anaomba simu, dingi akaguna tu nikajua kakubali nikatoa simu mgeni kaongea alivoondoka mweh!!!!
Nlichezea kichapo heavy yani mvua ya stiki..... Apumzike kwa amani mdingi
Wakishua hadi simu za mezani[emoji13][emoji13]
 
Hahahaha!! Umenikumbusha mzee wangu nilikuja home na rafiki yangu mmoja hivi ambaye hajawahi kufika home sasa tukakutana na mzee ndo anatoka, tukamsalimia then akaniuliza kwa kirugha ingawa siwezi kutamka ila nakiskia aliniuliza "huyu rafiki yako sio mwizi huyu na mimi nikajibu sio"[emoji28] nashukuru jamaa hakuelewa mchezo daaah!! Hatari sana enzi hizo....
 
Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kusuka.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alinichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havini umizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
Mara Paaaap nikatoka na mindoo kwenda kuchota maji, mialama ya viboko kwenye matako, mgongoni, mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora
Dah Kiloleni Tabora umenikumbusha mbali sana. enzi hizo tunatoroka tunaenda Rufita Club 1997 kushangaa swimming pool mkirud home tu ni kipigo cha hatari
 
nyinyi nyote trella... dingi yangu maarufu sana maeneo ya yombo kila mtu hadi majirani wanamuongelea enzi zake.. kuwa alikuwa hatari...

enzi hizo dar bado wenyeji wengi mitaa ya uswahilini kuna ngoma za wamakonde na wazaramo kibao....

kuna siku wazaramo walipita na kigodoro chao mchana nje ya ukuta dingi alikuwa anapalilia majani... wazaramo kibao kama 200 hivi.. dingi akawasimamisha.. na kuwauliza hivi kila kabila hapa likisema lipige ngoma yake si itakuwa balaa.. akawaambia ngoma za wazaramo kwa mchaga, mkurya, mnyakyusa, mhehe etc ni usumbufu.. kama wanataka ngoma wakapigie kwao msanga huko ambapo hakuna makabila mengine... wazaramo wakacharuka si unajua wanaongea sana wakaanza msuta dingi... mzee akajifanya amezidiwa.. akawaambia amependa hoja zao wamsubiri awaletee zawadi ya mwali wao...

wale wazaramo walivyo wajinga wakamsubiri kweli... dingi kazama ndani.. chumbani kwake kachukua gobole lake... kilichotokea ilikuwa story yombo mzima hakuna ambaye haijui..... dingi alivyotoka tu nje na gobole wakaanza kimbia na wapiga ngoma wakaacha ngoma zao.. dingi akazigeuza zile ngoma ni mafunzo ya kulenga shabaha... zile ngoma kubwa akazitia risasi zote.. na gobole lina kelele balaaaaa... mtaa mzima ndanii.. yeye anazitia shaba tu.

hawakurudi tena na ngoma zote zikawa zinapita mtaa wa pili.. hazipiti njia ya kwetu wanaogopa mwanajeshi mstaafu

dingi alikuwa anatubondaaa hadi mama analia yeye...

anakwambia ndani ya nyumba rafiki yake mke wake tu.. ana gari lake land rovee ukiingia humo huruhusiwi kukaa kiti cha mbele ni cha mke wake tu mama yetu.... na hata ukikaa siti ya nyuma ukipigwa wimbo mzuri huruhusiwi kutikisa kichwa anakushusha... enzi hizo watoto wake alikuwa anatushusha kwenda kanisani eti tunatikisa kichwa kwenye gari lake tukisikia mziki mzuri.. so kanisani inabidi twende kwa mguu.. yeye na mama ndio kwenye gari
Hahahah imebidi tu ni qoute japo maelezo marefu [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1], nimecheka hadi nimepaliwa mtori!
 
sisi mzee wetu anatajwa kuwa mzee mkoloni zaidi ya mjerumani, tunamuita miko jackson yeye magoma mwanzo mwisho,
akirudi nyumbani usiku kama mlikuwa mnapiga stori itabidi muondoke mmoja mmoja kwenda kulala.
hyu mzee hanaga stori yy ni kipigo tu haijarishi ni mkubwa kiasi madam ni mtoto wake ukiingia anga zake unapokea kichapo.

Hakuna mtu alikuwa na dingi mkali kanda ya kati kama mimi.

Yani Tabora, Dodoma na Singida nna uhakika mzee wangu ndio alikuwa mzee mkali kuanzia miaka ya 1976 mpaka alipofariki mwaka 1997.

Mzee alikuwa fundi umeme, ndani alikuwa na nyaya za umeme za kutosha siku ukifanya kosa anachukua nyaya anaikunja mara mbili anaanza kukupa kichapo. Ukishika umefuta

Maumivu ya nyaya ya umeme yasikie ndugu, ya mkanda yanasubiri sana. Maumivu ya nyaya nadhani ilibaki kidogo yafikie kwenye maumivu ya mapenzi (hahaha, joke)

Tulikuwa na choo na majani, siku moja nikawa nachezea kibiriti nikachoma choo then moto ukaenda kugusa kenchi za nyumba ashukuriwe Mungu majirani waliwahi kabla moto haujapamba lakini aliporudi mzee chamoto nilikiona, nilikuwa siwezi kukaa wiki nzima mfululizo kalio zimevimba balaa.

Pamoja na yote lakini nakukumbuka sana mzee wangu (RIP).

We mzee wako alikuwa mkali? tupe story
 
Back
Top Bottom