Wenye magari mnatufikiriaje sisi watembea kwa mguu?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Leo nimeomba lift magari zaidi ya matano na hakuna hata moja lilothubutu kusimama na chanzo cha kuomba ni kutokuwa na nauli ilinibidi nianze hamza kanuni huku nikisikiliza nyimbo ya Samba Mapangala - Dunia tunapita.

Je, wenye magari mnatuonaje watembea kwa miguu kiasi cha kutunyima lift?
 
Lifti na akupe na korona ilivyo tawala; atakaekupa ni mjinga Wa mwisho! Kanyaga kwa mguu! Bora ungeomba nauli lakini siyo lifti!
Kwanza watembea kwa mguu wengine majanga tu! Mnapanda na viwembe mnachana siti cover!

Kanyaga tu kwakweli
 
Kila mtu apambane na hali yake, mjini hatuombagi lift, me hata mtu akisimama kunipa lift kama simfahamu nachomoa hakuna kuaminiana tena cha bure mjini shikamoo, unaweza ukataka mserereko ukaishia kutatuliwa malinda bure
 
Nitoke nyumbani salama halafu jioni nirudi na corona kisa nimetoa lift....! Hiiiiiiii aliyo bhagosha.
 
Asili ya maisha ni kusaidiana na kutegemeana kila mmoja kwa wakati wake anamhitaji mwenzake sema ni muendelezo wa unafiki wa Binadamu.
 
Nitoke nyumbani salama halafu jioni nirudi na corona kisa nimetoa lift....! Hiiiiiiii aliyo bhagosha.
Unajuaje kuwa umetoka salama una vipimo vya corona kwako? Usisingizie vitu ambavyo havipo kutetea ubaya wa roho yako afu gari yenyewe Passo.
 
Lifti na akupe na korona ilivyo tawala; atakaekupa ni mjinga Wa mwisho! Kanyaga kwa mguu! Bora ungeomba nauli lakini siyo lifti!
Kwanza watembea kwa mguu wengine majanga tu! Mnapanda na viwembe mnachana siti cover!

Kanyaga tu kwakweli
Our day will come.. Leo mnatuona majanga kisa vigari vya kijapan vyenye kushinda garage.
 
Pole sana mh. Tatizo kubwa nilionalo ni binadamu kutokuaminika. Wapo wengi wamepoteza maisha ama kupata vilema vya kudumu pale walipojaribu kutenda wema kwa binadamu wenzao.
Binadamu tumebadilika sana zama hizi na kuwa zaidi ya wanyama mwitu. Sio tu kukataliwa lifti bali hata kumpatia lifti mtu asiyekufahamu na akikubali labda awe chizi.
Wavivu msiojua maana ya kufanya kazi, wengi wenu mnaunga mkono juhudi uchwara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…