May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Ni dhahiri kabisa kuwa kuja kwa teknolojia hakujaiacha salama sekta ya uchapishaji wa Magazeti, maana kwa sasa ni rahisi kwa mtu kupata taarifa papohapo tofauti na miaka ya nyuma.
Pamoja na changamoto hii yote lakini bado wapo watu wanaoamini na wanapenda kusoma Magazeti. Kama si Mgeni basi utakuwa unashuhudia Mkusanyiko wa Watu kwenye vibanda au meza za Magazeti, tena unakuta mtu ametulia akijaribu kupata chochote kilichoandikwa kwenye gazeti kwa taarifa iliyomvutia.
Nimeshuhudia mara kadhaa wenye Vibanda au Meza wakihangaika kuyalinda Magazeti yao yasichafuliwe au kushikwashikwa bila sababu kwa wengine kuweka Vioo juu ya Magazeti, na wengine huyapiga Magazeti pini (Stepler) kuyashikanisha ili Wasiohusika wasiyavuruge.
Nadhani ipo haja kwa Wenye Magazeti kukaa chini na kubuni namna bora zaidi ya kuandaa na kuuza Magazeti yao, haswa kwa kundi hili la Watu wa kipato kidogo ambao ni Wapenzi wa kusoma Magazeti. Wanaweza kuandaa vyumba au Vijiwe au Hema (tent) ambapo Mtu anayehitaji kusoma basi atalipa kiasi kidogo cha pesa, kwa mfano shilingi mia mbili ambapo atapata nafasi ya kupitia Magazeti Manne atakayoyachagua kwa muda maalumu mtakaokubaliana, kwa mfano nusu saa au dakika 40 n.k....na hapa kila Gazeti husika litapata mgao wa shilingi hamsini kutoka kwa Msomaji.
Bila shaka kuna uhusiano mzuri kati ya Wamiliki wa Magazeti na Wauzaji. Hivyo bado wanaweza kuwa Wawakilishi wazuri na Waaminifu.
Hii inaweza kufanyika kwa mfumo wa kopi ngumu (hard copy) au kopi laini (soft copy) ambapo kwenye banda kunaweza kuwekwa kifaa/tablet au smart TV ambapo Msomaji atakuwa ana 'touch' kupitia kurasa za Gazeti kwa muda aliolipia.
Bila shaka mtindo kama huu unaweza kupunguza hata gharama za kuchapisha kopi nyingi bila ya sababu na kwenda Mtaani kubahatisha Wateja...hapa zitaandaliwa kopi kadhaa kwa ajili ya Vituo maalum na kopi chache za kuuzia Watu wa maofisini, Majumbani n.k.
Mimi si Mdau wa uchapishaji wa Magazeti hivyo huu ni mtazamo wangu tu nikiamini Wahusika wao wanaweza kuwa na mawazo yao pia.