Wenye mahitaji maalum waongezewe dakika mitihani ya darasa la 7, kesho Oktoba 5, 2022

Wenye mahitaji maalum waongezewe dakika mitihani ya darasa la 7, kesho Oktoba 5, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA), Athumani Amasi, amewataka wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba inayoanza kesho Oktoba 5, kulinda haki ya watahiniwa wenye mahitaji maalum kwa kuwapatia mitihani yenye maandishi ya nukta nundu kwa wenye uono hafifu.

Na kwamba watahiniwa wote wenye mahitaji maalum waongezewe muda wa dakika ishirini (20) kwa kila saa kwa somo la Hisabati na dakika kumi (10) kwa kila saa kwa masomo mengine.

Aidha, amewaonya wamiliki wa shule binafsi na waratibu elimu, kutojihusisha na udanganyifu wa mitihani na kuwataka polisi walioko kwenye vituo vya mitihani kutoingia kwenye vyumba hivyo isipokuwa kama kuna dharura.

Chanzo: EARadio
 
Back
Top Bottom