Wenye malori wamwambia Dr. Magufuli barabara zako hazina viwango;

Wimana

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
2,449
Reaction score
718
Kufuatia mgomo wa wenye malori kupinga tozo ya 5% na kauli ya Waziri wa Ujenzi, Dr. Magufuli kuwa wenye malori waondoe malori yao barabarani na kuyapaki majumbani mwao, Wamiliki hao wamemkaba koo Dr. Magufuli na kumwita kuwa Dr. Magufuli ni muongo.

Kwa mujibu wa gazeti la Tanzania Daima [10 Okt. 2013], Mkurugenzi wa Consolidated Ltd, Karim Radha, alisema kuwa, madai ya Dr. Magufuli kuwa wenye Malori wanataka faida kubwa ndio maana wanapinga tozo hiyo ni uongo, na badala yake Dr. Magufuli aseme kuwa anaogopa barabara zake HAZINA VIWANGO, hivyo zitaharibika!

MY TAKE
Ni ukweli kuwa barabara zetu haziba viwango, ni mbovu, na hazijengwi kwa viwango stahiki.
 
Haya malori si ya Ridhiwani Kikwete? Kwa maana hiyo huyu Magufuli anamtunishia misuli JK? Naona siku zake zinahesabika
 
Mwalimu angefufuka leo akaona Chama chake na serikali yake ilivyowekwa mfukoni na wachache angekufa hapo hapo!
 
Ukimuona mtu katoa macho kama golori, midomo inatoa povu na akitoka jasho kutetea msimamo wake ujue kuna kitu hakikukaa sawa anafichaficha ukweli! Magufuli is hidding something! Siamini msomi wa level yake na akiwa waziri wa ujenzi veterani atashindwa vipi kuona an obvious and immediate impact kwenye uchumi wa nchi ukiparalyse transport system! Wasafirishaji wanajua zaidi huenda ni kweli Barabara hazina viwango! Sellby date ya haka kajamaa imepita, ame-expire, he should retire Gracefully kabla hajapata aibu kubwa zaidi!
 
...nahisi yule mzee amevuta harufu ya chemicals flani zinamchanganya,kadri siku zinavyoenda anazidi kushika rekodi ya kuibua maajabu ambayo hata mtu asiyeenda shule asingefanya hivo...
 
hawa ndio wahujumu uchumi wa kwanza, na wanaosaboteji reli ya kati siku zote, kiama chao kimekaribia, kuna siku hatutawahitaji tena hapa tz. tujipe moyo.watu wa malori wajinga sana.
 
Magufuli yupo sahihi kwa upande wake, pia tukumbuke kauli ya Pinda kuwapa mwezi mmoja, sasa hatutarajii mje kugoma utakapoanza kutumika huu utaratibu mpya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…