Wenye mitaji hii fursa inasomeka

Conservative gvt haiwezi kukubali mkuu, siunaona hata sekta ya kuzalisha umeme na maji imekuwa ikifanywa na serikali tu.

Wanajua kabisa wakiruhusu ushindani kutoka sekta binafsi basi Tanesco na idara ya maji zitajifia kama Ttcl inavyojifia baada ya kuruhusu sekta binafsi kuwekeza kwenye suala la mawasiliano ya simu.
 
Basi nilikuwa nimekuelewa vingine. Maana aya ya Kwanzaa ulivyosema sio rahisi halafu ukaunganisha BOT Nikadhani unamaanisha BOT ni kikwazo.
 
Basi nilikuwa nimekuelewa vingine. Maana aya ya Kwanzaa ulivyosema sio rahisi halafu ukaunganisha BOT Nikadhani unamaanisha BOT ni kikwazo.


Hapana mkuu, pia nakushukuru kwa ustaarabu wako. Ningoga matusi yanivurugie Jumapili kama usingekua mtulivu na mjenga hoja makini.

Zamani hata makampuni ya simu yanayotoa huduma za kifedha hazikua zikisimamiwa na BoT, siku hizi wametoa mwongozo na sera za usimamizi.

Umuhimu wa kurasimisha hii mifumo una manufaa sana. Kwanza kuhakikisha pesa iliyopo kwenye hiyo mizunguko inakuwa na usimamizi pia kuzuia utakatishaji wa pesa haramu. Kuna watu wamewekeza mabilioni ya pesa kwenye biashara za kukopeshana hauwezi kuwahusianisha nazo kirahisi.

Kingine serikali inapoteza mapato kutokana na kodi kwa hizo taasisi kutokurasimishwa.
Wakifanikiwa vizuri zoezi la usimamizi, ni rahisi kupanua wigo wa huduma kwa wanachama/ wateja kutumia akiba zao kwenye fursa zingine zilizo rasmi.

Mwisho kabisa, licha ya wengi wetu kutokuupenda huu utaratibu, pension lengo lake ni kumsaidia mwanachama anapostaafu au kupata ulemavu wa kudumu unaomzuia kufanya kazi. Huo ndio ukweli mchungu.
 
True.
 
Wazo jema, jinsi ya kutekeleza sasa, hata kama unao huo mtaji.
 
Katika nchi kama kenya, ghana n.k mifuko hii ya private ipo kisheria na inasajiliwa uchangiaji ni wa hiari lakini imeleta faida sana kwa nchi na wananchi. Hizo private fund zinatumia michango kuwekeza kwenye miradi yenye tija na yenye faida na wanachama wanapata faida wakati wa kuchukua mafao yao ambayo wanaweza kuchukua wakati wowote. Nchi hizi kiwango cha kuchangia mifuko ya lazima haizidi 10% hiyo inampa mtu nafasi ya kichangia private sasa hapa kwetu ukishachangishwa 20% utaweza kuchangia tena private fund?

Faida kubwa zaidi ni kuwepo mitaji kwenye hizi private fund inayotumika kwa tija sio hapa yanajemgwa magorofa marefu yaliyotupu miaka nenda miaka rudi.
 
Nchi nyingine pesa hizi hukopeshwa tena serikali kujengea hospitali shule na miradi mikubwa ya maji. Inschangia kuleta maendeleo haraka kwa wananchi
 
Serikali imepitisha sheria za kuilinda hii mifuko hatimaye inakua monopoly. Hawatakua tayari kuona mifuko mingine ikianzishwa nje ya serikali.
 
Good idea kwakweli, lakini kunachangamoto nyingi sana, katika utekelezaji wake hasa kwenye nchi kama hii.
 
Wazo jema, jinsi ya kutekeleza sasa, hata kama unao huo mtaji.
Mbuyu ulianza kama mchicha , ukiwa na nia unaanza kutafuta wakili akupambulie sheria na inakuwa na business proposal unaipeleka kwa wahusika.
 
Sio rahisi. Wakati sheria inatungwa niliwashauri sio private pensions tu bali.
1. Mifuko iwe inatoa pension za dola ili kuondoa inflation. Ni rahisi tu. Inakuwa kunverted at the month of contibution. Hii ingesaidia hata diaspora wajiunge.
2. Kununulia watu pension. Wapo watu wangependa kuwalipia michango wazazi na ndugu badala ya kuwatumia hela kila saa.
3. Kununua pension yako. Fikiria wewe una biashara labda ya kilimo na unazeeka na huna mtoto wa kuendeleza unachikifanya. Unauza unanunua pension unatulia.
4. Kwa wafanyakazi kuamua kiasi cha pensionunachokitaka. Unajiuliza nikitaka nikistaafu pension yangu iwe say 3m nifanyeje? Wanapiga hesabu unaambiwa average michango kwa mwaka isipungue kiasi fulani then unajiwekea akiba ya uzeeni na sio benki kusiko na faida.

Yote yalipuuzwa.
Wenye mamlaka wengi hawana vision na wenye visions wapo pembeni......
 
Inakuwa kama retirement package, ni nzuri sana, ila sidhani kama serikali itaruhusu, pia makampuni sidhani kama watakubali kukuchangia tena after ile social security.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…