Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema imebaini kuwa Wahusika wa biashara haramu ya dawa za kulevya hutumia mbinu ya kupanga nyumba ambazo zinageuzwa kuwa maghala ya kuhifadhia dawa za kulevya, huku wao wakishi katika maeneo mengine.


Akiongea Jijini Dar es salaam leo November 25,2024, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema "Mamlaka inatoa rai kwa Wamiliki wa nyumba kuwa makini wanapopangisha nyumba zao, kwani nyumba inayotumika kwa shuguli za dawa za kulevya ni kinyume cha sheria na inaweza kutaifishwa"


"Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za


Kulevya, Sura ya 95, imeweka katazo kwa Mmiliki au Msimamizi wa nyumba, Msimamizi wa eneo au chombo cha usafirishaji kuruhusu vitumike wa lengo la kutengeneza, kuvuta, kujidunga, kuuza au kununua dawa za kulevya"


"Mmiliki anapojua kuwa kosa linatendeka kwenye eneo lake, anajukumu la kutoa taarifa kwa Mamlaka, kushindwa kufanya hivyo ni kosa la jinai, na akitiwa hatiani, adhabu yake inaweza kuwa faini kuanzia shilingi milioni tano hadi milioni hamsini, au kifungo cha miaka mitano hadi miaka thelathini jela, au vyote kwa pamoja"
 
Hayo ndo madhara ya watu kunyonya takro na K, mavi kuyaona ya kawaida utafikiri umekuwa mende. Seriously, unatamani mavi? Na wewe ni mtu wa Gavrument? Lazima tuwe na watu wa akili kama huyo jamaa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.
Anatumia kifungu kipi cha sheria kusema hadi nyumba inataifishwa?
Atujuze
 
kwa sheria ipi ya kwako na mpangaji au sheria ya kitaifa ya wenye mamlaka walioshika mpini alafu utegemee kushinda kwanza utaweza kushindana nao.?
Ngoja nifatilie undani wa hiyo Sheria Mkuu

Kwa mawazo yangu, haitakiwa umwajibishe mwenye nyumba Kwa makosa yasiyo yake iwapo amesha-onesha kwenye Mkataba wake na Mpangaji kwamba hatowajibika Kwa makosa ya Mpangaji wake.

Labda waseme kuna watu wao wamewa-target kuelekea Uchaguzi Mkuu Mwakani
 
Relax, haiko automatic hivyo. Kuna mazingira ambayo mwenye nyumba nae anakuwa mshiriki hivyo kuhalalisha nyumba kutaifishwa, ila kama hahusiki nyumba haiwezi taifishwa.
 
Maigizo ya kupambania sijui kupiga Vita madawa waachane nayo Sasa.
Vita miaka nenda miaka Rudi ipo...Vita gani hiyo. ?
 
Kama wakiamua kukutaifishia wanakutaifishia tu mkuu.

Hii nchi ngumu sana
Tutauna walah, hii sheria waifute haraka, hakuna atakaekubari nyumba yake itaifishwe kijinga, mimi nna nyumba huko mbezi nimepangisha, mwenyewe labda nakaa temeke, ntajuaje kama mpangaji wangu kaleta mifuko ya drugs nakuifadhi kwenye nyumba yangu? Wapitishe sheria sasa yakuwapa wenye nyumba haki yakukagua ndani vyumbani kwa wapangaji kila baada ya mwezi chini ya balozi.
 
Labda ana maanisha bandari kuwa ilikutwa na madawa ndo ikataifishwa kwa wakora
 
Acha kupotosha, umeleta habari nusu kwa makusudi. Ameeleza kwamba ni endapo mwenyenyumba alikuwa anafahamu na hakuripoti.., sasa hapo utaprobe vipi mwenye nyumba alikuwa anafahamu?
 
Nini? Hebu "acheni" basi utani!
 
Haitokusaidia hiyo ...unakagua Leo mzigo hana ...fresh unaondoka kesho anaweka mzigo si unakuja kila mwisho wa mwezi!??....
 
Either wanitoe kwenye hiyo nyumba nikiwa maiti wamenibeba au niwaue wote nikafie jela ila sio rahisi Kama wanavyosema .
Kwa mfano mmefahamu mpangaji ndiye anayehusika na hiyo biashara na mmejiridhisha Kabisa kuwa ndiye haswaa!! Hapo nyumba inahusikaje? Kwa nini msidili na mhusika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…