MtamaMchungu
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 8,974
- 12,662
Wakuu,
Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.
Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.
Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.
Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.
Source: Wasafi FM
My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?
1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?
2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?
3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?
4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?
5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
Gari sawa ila kwa nyumba nadhani hii sheria wangeiangalia upya. Mfano mimi nina nyumba masaki na ninaishi njiro arusha. Nyumba ya masaki nimempangisha mtu, je ni jukumu langu tena kuwa naenda kumkagua huyo mpangaji kila siku kuona ni nini kiko ndani ya nyumba? Vipi kuhusu sheria ya faragha na haki binafsi za huyu mpangaji?Wakuu,
Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.
Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.
Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.
Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.
Source: Wasafi FM
My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?
1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?
2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?
3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?
4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?
5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
Mahakama gani hiyo?Kuna sheria na Mwana sheria tutakutana mahakaman
Kuna sheria gan inampa kibari mwenye nyumba kuwa anaenda kukagua kila sku kwa mpangaji wake
Ni sheria gan inaniruhusu kuingia nyumban kwa mpangaji wangu na kuingia vumbani kwake kumkagua km anatunza madawa
Kwa ujinga huu tutakutana mahakaman na uyo mkurugenzi wa madawa
Ujaelewa mchezo uliopo apa ,shida sio kazi aliyonayo mpangaji shida ni kosa la mpangaji maafa makubwa unapata ww mwenye nyumbaHapo deal ni kuweka hicho kipengele kwenye Mkataba wakati wa kumpangisha mtu.
Mimi niliwahi kuweka kipengele cha kumtaka Mpangaji kueleza kazi ama shughuli aifanyayo kuendesha maisha yake
Hii ilisaidia kutowapangisha watu Wasumbufu kulipa Kodi
Hopefully na hicho kipengele kikiwepo kwenye Mkataba wa kupangisha, kitasaidia kumlinda mwenye nyumba
mi nikiwa bwege we utakuwa chiziMaaskari hiyo sheria wanaijua sk nyingi we bwege.
Nimeelewa sasa Mkuu, hapo ni kama Kuna mtego mtu ametegewa ili kumnasaUjaelewa mchezo uliopo apa ,shida sio kazi aliyonayo mpangaji shida ni kosa la mpangaji maafa makubwa unapata ww mwenye nyumba
Aibu kubwa sanaSerikali ya Tanzania huwa inashindwa kesi zinazofunguliwa kwenye mahakama za nje ya nchi tu, siyo za ndani ambazo ni zake na hukumu hutolewa kwa kufuata maelekezo kutoka juu