Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Kuna sheria na Mwana sheria tutakutana mahakaman

Kuna sheria gan inampa kibari mwenye nyumba kuwa anaenda kukagua kila sku kwa mpangaji wake
Ni sheria gan inaniruhusu kuingia nyumban kwa mpangaji wangu na kuingia vumbani kwake kumkagua km anatunza madawa

Kwa ujinga huu tutakutana mahakaman na uyo mkurugenzi wa madawa
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?

Tanzania nchi yahovyo sana kuishi ukiwa raia wa kawaida, ila kwa watawala ni nchi poa sana maana unanyonya kwa mrija tuu.
 
Na kuna sheria nyingine ya wizi tuu. Inahusu wanaochimba visima vya maji. Yaani wewe umejenga sehemu ambayo huduma ya maji haipo unajikoki unaona si vyema familia iteseke, unaingia gharama kuchimba maji kwa mamilioni mengi sana kupata underground water. Umefanikiwa kupata maji mita 100 chini ya ardhi. Unatakiwa kulipia drilling permit (hiyo sikatai). Ila sasa umeanza kutumia maji unaambiwa kila mwaka uwe unalipia kodi/ushuru. huu ni wizi kama wizi mwingine. Serikali inashindwa kufikisha huduma ya maji kwa wananchi, anatokea mwananchi anaingia gharama kubwa (ambayo serikali ilipaswa kubeba). badala ya mwananchi huyu kusaidiwa ndo anakandamizwa. Mtu anatumia milioni 15 hadi 20 kwa ajili ya maji tuu, pesa ambazo zingemkwamua huyu mwananchi from other problems lakini badala ya kusaidiwa anakandwa zaidi
 
Hii inafanana na ile ya gar yako ikishikwa imebeba madawa inataifishwa
Sasa mm nimebeba misokoto yangu 10 ya bangi naenda kuenjoy polisi kakushika kakuta bangi kwa gar unataka utaifishe gar yangu ya million53 kwa bangi za elf10 huu ujinga nani atakubari
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
Gari sawa ila kwa nyumba nadhani hii sheria wangeiangalia upya. Mfano mimi nina nyumba masaki na ninaishi njiro arusha. Nyumba ya masaki nimempangisha mtu, je ni jukumu langu tena kuwa naenda kumkagua huyo mpangaji kila siku kuona ni nini kiko ndani ya nyumba? Vipi kuhusu sheria ya faragha na haki binafsi za huyu mpangaji?
 
Kuna sheria na kuna maneno ya jukwaani

Ata jiwe alisema wamachinga waweke biashara zao popote pale ila akuwawekea sheria ya kuwarinda bali aliongea stejini km mwana siasa tu
 
Kuna sheria na Mwana sheria tutakutana mahakaman

Kuna sheria gan inampa kibari mwenye nyumba kuwa anaenda kukagua kila sku kwa mpangaji wake
Ni sheria gan inaniruhusu kuingia nyumban kwa mpangaji wangu na kuingia vumbani kwake kumkagua km anatunza madawa

Kwa ujinga huu tutakutana mahakaman na uyo mkurugenzi wa madawa
Mahakama gani hiyo?
Labda ingekuwa Mahakama za nchi nyingine zonazotenda haki. Ukileta ubishi utabambikiziwa kesi ya uongo tu kuwa na wewe umekutwa na madawa ukatulizwe ndani huko
 
Hapo deal ni kuweka hicho kipengele kwenye Mkataba wakati wa kumpangisha mtu.

Mimi niliwahi kuweka kipengele cha kumtaka Mpangaji kueleza kazi ama shughuli aifanyayo kuendesha maisha yake

Hii ilisaidia kutowapangisha watu Wasumbufu kulipa Kodi

Hopefully na hicho kipengele kikiwepo kwenye Mkataba wa kupangisha, kitasaidia kumlinda mwenye nyumba
Ujaelewa mchezo uliopo apa ,shida sio kazi aliyonayo mpangaji shida ni kosa la mpangaji maafa makubwa unapata ww mwenye nyumba
 
Kwanini MWANANCHI apewe tabu katika Taifa lake lililo na UWAZI NA UKWELI unaohubiriwa na viongozi wake?

Nini maana ya viongozi wa serikali ya mitaa ? Tunakwenda kufanya CHAGUZI kwa ajili ya nini?

Sheria hii IBADILISHWE iwe ya kwanza KUTAMBUA nguvu za viongozi wa mtaa!! AMBAO tunaishi nao! WASIMAMIE mikataba ya upangaaji na wawatambue WAPANGAJI kwani jukumu la usalama linasimqmiwa na wao.

Ukijenga kwa haki huwezi tamka sheria hii.
 
Ujaelewa mchezo uliopo apa ,shida sio kazi aliyonayo mpangaji shida ni kosa la mpangaji maafa makubwa unapata ww mwenye nyumba
Nimeelewa sasa Mkuu, hapo ni kama Kuna mtego mtu ametegewa ili kumnasa

Ukiwa na Bunge linalojitambua, hawawezi kupitisha Sheria za hovyo za namna hii, bahati mbaya huku kwetu Wabunge wetu hawako pale kutusaidia Wananchi wake, isipokuwa Serikali 🙌
 
Inaskitisha sana...

Inabidi wapangaji kuanzia sasa wawe na Police clearance Certificate, ili uweze kupanga nyumba...

Ili wakibainika wana magendo haramu mwenye nyumba hausiki...

Cc: Mahondaw
 
Hata misokoto miwili ya bangi? Je,dawa ikikutwa kwenye nyumba ya serikali?
 
Nyumba ya kupanga si mali ya mwenye nyumba waache ukuda
 
Back
Top Bottom