Wenye Nyumba kaeni kitaalamu: Kama mpangaji wako atakutwa na dawa za kulevya nyumba yako itataifishwa!

Hawa wapuuzi kuna wakati wanalewa madaraka na kuropoka ovyo kama watu waliokula madawa ya kulevya. Huyo aliyetamka hayo maneno inawezekana naye amelewa madawa ya kulevya. Akamatwe apimwi madawa mwilini mwake.
Kabla hajapanda kwenye podium lazima ashtue Embassy km 3/4 hivi na akisema Embassy nazo ni dawa za kulevya basi yeye atakua wa kwanza kukamatwa na kuwekwa ndani

Daktari anakataza watu wasivute Sigara ila kwenye mfuko wa Shati ana paketi la Sigari au anakataza watu wasinywe pombe ila kwenye draw kahifadhi Kisichana (bapa ndogo)
 
Nyumba zangu za kupangisha Kuna kupengele Mali ya mpangaji ni yake haisiani na mwenye nyumba hata ulinzi WA Mali zake ni juu ya mpangaji mwenyewe,Sheria ya Lyimo inakinzana na masharti ya wapangaji wangu
Kwanza kitendo cha kupokea kodi tu kutoka kwa mpangaji, hiyo nyumba si mali yako tena hadi pale kodi itakapo kwisha,ndiyo nyumba inarudi kwa himaya yako na unaweza hata kuingia ndani saa yoyote ukitaka!!
 
Biashara ya nyumba za kupanga, ni changamoto kwa baadhi ya maeneo na kwa baadhi ya wapangaji wasio waaminifu coz anaweza fanya tukio huko au nyumba yako ikahifadhiwa vitu vibaya kama hilo angalizo.
Kila sehemu kuna watu waaminifu, na wengine siyo waaminifu, halkadhalika wapangaji! na hadi huko serekalini wapo pia!!
 
Huyo kamishina hapo atasababisha watu wadhulumiwe nyumba zao na pia ametengeneza mianya ya rushuwa

Watu wenye elimu iliyokamilika hawawezi kutunga Sheria kama hiyo
 
Huyo kijana amenukuu hicho kifungu cha sheria? Au maneno tu. Ndio maana serkali yetu inaingia kesi ambazo itashindwa huko mbele na kulipa gharama kubwa.
Kwani sheria za upangaji zinasema ukipangisha mtu unaingilia faragha zake?
Mahakama ndio inaweza kutofasri hiyo sheria feki na nitashangaa kweli kama ipo
Kijana yupi mkuu?
 
Hapo deal ni kuweka hicho kipengele kwenye Mkataba wakati wa kumpangisha mtu.

Mimi niliwahi kuweka kipengele cha kumtaka Mpangaji kueleza kazi ama shughuli aifanyayo kuendesha maisha yake

Hii ilisaidia kutowapangisha watu Wasumbufu kulipa Kodi

Hopefully na hicho kipengele kikiwepo kwenye Mkataba wa kupangisha, kitasaidia kumlinda mwenye nyumba
Kwamba ukiweka hicho "kipengele" kwenye mkataba halafu mpangaji akakutwa na bangi au heroine ndani ya hiyo nyumba wataacha kuitaifisha?

Hapo dawa ni kuipinga hiyo sheria ya hovyo ifutwe (kama tayari ipo), ila wakiipitisha huwezi kuzuia utekelezaji kwa kigezo cha Mkataba.

Watawala walishagundua kuwa raia ni wapole, watawaonea sana hadi watakapozinduka
 
hapo sasa labda mwenye nyumba nae awe anaishi humo pamoja na wapangaji wake na sheria hii inafaa sana kwa zile nyumba za kupanga chumba kimoja kimoja huku mitaani..ila zile full zenye fensi na mageti hiyo ukishapangisha hauna mamlaka nayo tena mpaka mwisho wa mkataba maana ni ngumu kumbana uliyempangisha ..ila wafanya maamuzi wa nchi hii wanasikitisha sana
Yes, atleast hapo unaweza kupata som sort of proof kwamba mwenye nyimba alikuwa anajua, lakini, nado nayo ni rahisi kukana, maana atasema yeye huwa haingii kukagua vyumba vya wapangaji..
 
Mpangaji endapo amekutwa na Madawa anabidi kuwajibika kupitia Makosa yake yeye mwenyewe.

Sasa ikiwa nchi imekosa watu wenye uwezo mzuri wa kufikiri Kwa kina inatia mashaka Sana .

Wanachukulia mambo kiuwepesi Sana kiukweli.
 
Kwamba ukiweka hicho "kipengele" kwenye mkataba halafu mpangaji akakutwa na bangi au heroine ndani ya hiyo nyumba wataacha kuitaifisha?

Hapo dawa ni kuipinga hiyo sheria ya hovyo ifutwe (kama tayari ipo), ila wakiipitisha huwezi kuzuia utekelezaji kwa kigezo cha Mkataba.

Watawala walishagundua kuwa raia ni wapole, watawaonea sana hadi watakapozinduka
Kuna baadhi ya Sheria, kabla hazijapitishwa huwa wanakusanya maoni ya Wadau

Nafikiri kwenye hii Sheria, hawakufanya hivyo

Nafikiri kuna haja tuombe amendment.

Kwasababu halitamgusa mtu mmoja, bali wote

Maana hata Wabunge wanazo nyumba za kupangisha
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
Tz, roho mbaya, daima kutunga sheria za kukandamiza na kuumiza WaTz! Madawa yamekutwa ndani ya Tz, je nchi itaifishwe, maana kama mamlaka mmeshindwa kuyadhibiti, mna kwenda kukomoa Mtz asiyehusika na madawa! Serikali mmeshindwa kazi!
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
kwa mwendo huu polisi ccm watamiliki nyumba za kisasa kabisa
 
Ukishaikamata nyumba, jaribu kutafuta uhusiano wa mwenye nyumba na hiyo biashara,KAMA HAKUNA UHUSIANO MRUDISHIE MWENYEWE NYUMBA YAKE.

Mtu kakupangisha anakwambia ni muajiriwa taasisi fulani na umethibitisha hilo au mfanyabiashara Kariakoo na umethibitisha hilo suala la yeye kuuza madawa ni la siri na NI mamlaka za usalama tu zinazoweza kugundua.
Nina office apartments na mtu kaja kapanga kwa kazi fulani na ana leseni nayo na analipa Kodi, mamlaka zimemkamata kwa biashara yake ya gizani, Mimi nahusikaje?
 
Wakuu,

Kama una nyumba sehemu kaa kwa chonjo kuna habari mpya huku kutoka DCEA.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amewahimiza wamiliki wa nyumba za kupangisha kuwa waangalifu na wapangaji wao.

Alieleza kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wamekuwa wakitumia nyumba walizopanga kama maghala ya kuhifadhi dawa hizo, huku wao wakiishi sehemu nyingine.

Soma pia: Makonda: Ukichagua viongozi wa mtaa waaminifu wasiyojihusisha na madawa ya kulevya utaleta chachu katika ngazi hiyo

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 25, 2024, jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali Lyimo alisisitiza kuwa kwa mujibu wa sheria, mali yoyote, kama nyumba au gari, ikikutwa na dawa za kulevya, itataifishwa.

Kamishna huyo amewataka wamiliki wa mali hizo kuhakikisha wanachukua tahadhari na kusimamia vyema mali zao ili kuepuka hasara na kuhusishwa na vitendo haramu.

Source: Wasafi FM

My take:
Mbona kama kuna watu specific wanatafutwa kwa tochi kupitia agizo hili?

1. Mimi kama mwenye nyumba ntajuaje kama mtu anaweka madawa ya kulevya ndani ya nyumba? Niweke CCTV au niwe nafanya doria za kushtukiza?

2. Hiyo nyumba ikishataifishwa inapelekwa kwa nani au taasisi gani?

3. Kama inaenda kwa serikali hamuoni kwamba kuna baadhi ya vigogo serikalini wanaweza wakatumia mwanya huo kupora nyumba za watu iwapo watazipenda?

4. Huo utaratibu wenu wa kutaifisha nyumba ni watanzania pekee au ni utratibu wa kimataifa? Ni mataifa gani yana utaratibu kama huo?

5. Hiyo sheria ya kutaifisha nyumba ambayo sio ya mtuhumiwa ipo kwenye ibara gani kwenye Katiba yru ya inchi?
KWa huu mwendo itabidi tutaifishe nchi yenyewe
 
Back
Top Bottom