Kindimbajuu
JF-Expert Member
- Jul 8, 2009
- 710
- 247
kama kuna mijitu mijizi mikubwa bi ewura. inakusanya ewura levy toka kwa wananchi, hakuna inachofanya sanasana ni kutafuta kuongea kwenye vyombo vya habari. kukuta pump 15 zinatatizo mpaka wanaqita mkutano na waandishi wa habari. seria zao zimekaa kinyume nyume. samahani jamani kwa kutumia lugha kali. nitawapa mfano wa mambo ya kupuuzi ambayo mamlaka hii inafanya. wanapita kukagua mafuta vituoni, ni kweli wanakuta diseli iyochanganywa na mafuta ya taa, wamtoza faini mwenye kituo- hilo ni jambo jema, baadae wanatangaza kwenye vyombo vya habari- hilo ni jema zaidi. lakini ikumbukwe mafuta husika tayari hayana uboa wa kutumika kwenye magari,na yayaendelea kuuzwa kituoni. nilitarajia kwa mamlaka yenye kufanya kazi ka umakini wangehakikisha hayo mafuta hayatumiki tena kwa magari. wangehakikisha yanapelekwa nyenye matumizi mengine ya viwanda . kuacha mafuta hayo yatumike tena ni hujuma kali kwani wananchi wanachangia uendeshaji wa ewura ili wapate huduma, na hawana msaada wowote wa ewura