Wenye uzoefu wa kuagiza bidhaa mitandaoni tuleteeni uzoefu wenu. Huu hapa uzoefu wangu.

Wenye uzoefu wa kuagiza bidhaa mitandaoni tuleteeni uzoefu wenu. Huu hapa uzoefu wangu.

miamiatz

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
505
Reaction score
941
Kwa uzoefu wangu wa kutumia amazon bidhaa nyingi nilizoagiza mtandaoni garama yake mpaka kunifikia imekuwa kubwa kwa zaidi ya 25% kuliko bei ambazo maduka ya hapa tz huuza.

Mfano unakuta Samsung Galaxy A7 ya 2018 4gb ram 128gb rom inauzwa US Dola 390 mtandaoni. Unalipa kwa paypal inakuwa around Tshs 910,000.

Shipping agent unaemchagua anakupiga US Dola 182 ikiwa ni shipping, taxes na duties ambayo unamlipa around Tshs 430,000.

Ukijumlisha Tshs 910,000 na Tshs 430,000 unapata Tshs 1,340,000. Sasa madukani hapa tz simu hiyo hiyo inauzwa around Tshs 800,000.

Hii inaifanya biashara ya kuagiza vitu kwenye mitandao kama amazon kuwa ya hasara sana.

Nipeni uzoefu wenu kwa wale wenye uzoefu na jambo hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ebay Galaxy A7 ya 2018 ni kama inavyoonekana kwa screenshot. Ni zaidi ya US Dola 400 per piece. Kabla hata hujaisafirisha
Screenshot_20190216-101047.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtandaoni agiza bidhaa kama simu non famous brands hapo ndo utapata unafuu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
Njoo na details mkuu mana kuna simu kama xhiaomi, CM, etc nimelinganisha pia bei za madukani. Hata ukiangalia bei za Jumia na za Alibaba ama Ebay bado Jumia wapo chini kabla hata ya ku import.

Mathalan kitochi Nokia 105 (see attacment) ebay brand new ni US $51 hii inakaribia 120,000 kabla haijasafirishwa wakati Jumia brand new kuna jamaa anauza 38,000 kwa duka lake (see screenshot).
Screenshot_20190216-111129.jpeg
Screenshot_20190216-110840.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliexpress is the best very chip aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Bado hujanipa ushawishi wa kutosha hebu weka details mkuu. Angalia attachment ya bei ya galaxy a7 2018 huko aliexpress kwa attachment. Dola 300 uki iconvert to tshs kabla hata ya kuisafirisha kuja bongo ni laki7. Afu huku madukani wanauza laki nane. Kwenye hiyo ya laki saba bado dhl bado ushuru.

Mtu aje na details. Aje na sample product afu ailetee details madukani bei gani na online bei gani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm pia napata tatizo kama lako, kuna baadhi ya watu mtandaoni wanatushauri kuwa si lazima uende nje ya nchi kununua bidhaa, hasa kama mtaji bado mdogo, mbona mtandaoni bei zinakuwa kubwa kuliko madukani kariakoo?
 
Back
Top Bottom