MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Wakuu kuna mambo ambayo kisheria yako sawa ila kiustaarabu yana ukakasi. Kwa mfano hili suala la wazee wa zaidi ya miaka 60 kuwa na mtoto mdogo na kabinti. Yaani kabinti kadogo kanachopaswa kukuamkia. Mbaya zaidi unakuta mzee kiuchumi hayuko poa inabidi tena umpige tafu. Hii naona haiko sawa hata kimaadili. Imagine mtu wa miaka 38 uwe na mdogo wako wa miaka 2 huku mtoto wako akiwa na zaidi ya miaka 10. Yaani hesabu haziji kabisa.
Ninawasihi wazee wote kutulia tu na mama zetu na kuacha kujihangaisha na vibinti. Sisi vijana wenu badala ya kupambania familia zetu tunaanza tena kuwalelea watoto wenu wa uzeeni. Sio sawa kwa sababu ni kama kuendekeza umaskini wa familia. Mungu awatangulie watu wote wanaohudumia watoto wa michepuko ya baba zao.