Wenyeji wa Kahama naomba kufahamu kuhusu soko la vitunguu kwa muuzaji wa jumla lipoje

Wenyeji wa Kahama naomba kufahamu kuhusu soko la vitunguu kwa muuzaji wa jumla lipoje

Ngopyoro city

Senior Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
144
Reaction score
220
Habari wakuu poleni na majukumu ya kujenga Taifa Mana wazee tunapambana paka inafikia muda unasema sijui niende kigoma kucheki nyota kwanza[emoji16]

By the way nilikua na mission za kununua samaki na kwenda kuuza pale makambako samaki nawatoa bonde la mto kilombero sehemu moja inaitwa gundu mzigo unapatikana fresh sema changamoto ndogo ndogo ila unakomaa nazo ila wakinga wale wachawi balaa anakupa buku mbili alafu baada ya mauzo jioni pesa huna[emoji16][emoji16]

Aaaaah kuna mdau kanilengesha biashara ya kuchukua vitunguu pale singida nikaona iko fresh ameniambi soko ni kahama au Arusha ila kahama ndio pazuri kwa sisi wazee wa kuuza kwa jumla yani unafiksh mzigo unakomaa na dalali alafu muda ya jioni mnapiga hesabu zenu unadandia ndinga kufata mzigo mengine

Sasa wadau wa kahama vipi masoko ya Hapo yanaweza ku accommodate hizi mission mfano nikija na gunia 50 za vitunguu naweza kuuza kwa mda gani bei ya jumla na bei zikoje kwa huko? Pia kama kuna ushauri na maoni yoyote yale hakuna budi kunishauri wazee wenzangu

Natanguliza shukrani huku tukiendelea kupambana na hii hali Mana kwa hii mitano iliyopita Hali ilikua mbaya Sana Sasa hii mitano mingine ni hatari mtaani hapakaliki yani ugali moto ,mboga moto wenye degree Hali ni mbaya zaidi wote wamekua madalali[emoji16][emoji16] au nasema uongo ndugu zangu?
 
Aisee mimi nikupongeze kwa juhudi ulizonazo.! Ila kuulizia soko hapa Jamvini huenda usipate taarifa zakueleweka. Ukipata muda jaribu kufika eneo husika na ufanye market analysis huenda ikasaidia zaidi kuliko kutumia watu wa Humu maana wengine wanachangiaga tu ili mradi ili hali hana ujuzi wowote ila kuna baadhi yao wanatoa mawazo ambayo yamekuwa msaada
 
Aisee mimi nikupongeze kwa juhudi ulizonazo.! Ila kuulizia soko hapa Jamvini huenda usipate taarifa zakueleweka. Ukipata muda jaribu kufika eneo husika na ufanye market analysis huenda ikasaidia zaidi kuliko kutumia watu wa Humu maana wengine wanachangiaga tu ili mradi ili hali hana ujuzi wowote ila kuna baadhi yao wanatoa mawazo ambayo yamekuwa msaada
Shukrani kiongozi Mungu akubariki

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Kahama biashara ipo lakini ukumbuke pale ni njiani na wafanyabiashara wa singida wengi hupeleka pale vitunguu, halafu ukumbuke pia hiyo ni mali kuoza lakini ukiweza kufika Bukoba au Mutukula nadhani utauza sana.
 
Kuhusu hao samaki wala usihangaike wewe beba mzigo wako ukifika makambako nenda inapopakiliwa mizigo ya Songea, Songea ukifika ingia soko moja manzese pale wanakula sana samaki nadhani hata mzigo wa milioni nne hutomaliza siku nne haujaondoka kurudi kufuata mzigo mwingine.
 
Kama ni mtwmbezi safiri hadi kijiji kinaitwa Mpui iko sumbawanga kule wana bonde wanalima vitunguu unajichanganya uanze kupeleka kasumbalesa sema corona itakuharibia
 
Na ukumbuke unapofanya study za kibiashara usiende na mzigo mkubwa wewe chukua gunia kidogo kwanza za kukurudishia nauli yako na matumizi ukisoma game ndio unaingia mazima hakikisha dalali unamuweka chini ya ulinzi mkali ukifika
 
Back
Top Bottom