...Shangazi na mkuu Kaizer nashukuru kwa taarifa. I dont mind spending more, ndio maana nikasema kuanzia 35,000/= kwenda juu.
Mkonge Hotel nadhani wana charge 80,000/= kwa usiku mmoja (B & B), je? kuna hoteli nyingine zenye hadhi ya maana Tanga mjini badala ya Mkonge? ... say, wana charge bei kidogo chini ya hapo?
Mkuu Mbu ha!ha1ha!ha! Nilikuwa Tanga juzi juzi mwishoni mwezi wa nane! naweza kukwambia haya!
Mkonge Hotel......ina madhari nzuri sana, iko baharini, ina viunga vikubwa sana vya kupumzikia, ina vyumba vikubwa sana, ina AC nzuri, bacon poa kabisa ina vyumba vya sea facing na vya kawaida, pia wapo na parking kubwa sana!
Mimi nililala pale siku moja tena was room #223 Sea viewing one! Matatizo niliyoyaexperience mimi ni haya:
1. Wana wahudumu wachafu sana (kwa kila kitu hapa)
2. Wanahuduma mbovu sana (customer care), mfano nilikuta toilet chafu, mashuka ni quite old, vikorombwezo like remote controls za TV, AC ni matatizo....nilitaka nicheki game nikashindwa mbali ya kuomba wanisaidie kama mara mbili hivi
3. Wana gharama sana (kulinganisha na huduma) see viewing rooms ni Tshs 70,000 wakati vya kawaida ni Tshs 65,000
4. Wanaopenda kujirusha, viwanja pale karibu hakuna yaani pamejitenga sana mkuu!
5. Vyumbani hakuna the So called MIN BAR....kwa wale wenzangu...!
Siku ya pili nikahamia DOLPHIN hotel
Hawa wako na rooms nzuri sana za aina na bei tofauti;
Zipo za Tshs 50,000 .....zina AC, Simu, breakfast, big room, maji ya moto (if you like), huduma nzuri na wahudumu kidogo wanazingatia usafi binafsi na wako na sare nzuri sana!
Zipo pia 25,000 (min) na 30,000....huku quality ya rooms inapungua kiasi!
Hawa pia wako mjini ambapo ni karibu na viwanja vingi vya kujirusha, like Nyinda bar (pana rost ya maini na nyama choma acha kabisa) Club la Casa, Chichi Club, Ze City Hotel (Hapa mzee pana supu ya pweza acha kabisa)etc!
Tatizo la Dolphin ni parking sio kubwa sana!
Nyinda wana rooms nzuri sana na bei yao ni Tshs 25,000.....! sema hawa pale kwao nje kuna bara ambayo ni very popular na hujaa sana wateja so kelelee!
Panori .....unaweza kugoogle kuna agent wao anawatangaza kwenye net.....ila hawana jipya huduma zao room ni Tshs 40,000, no simu lakini breakfast...ukitaka piga simu hii...
027 2646044 (ni ya Hotel hii) watakwambia what they can offer!
Mbu kama mwenyewe unaenda Tanga na hupenda kujirusha, pitia pale Club la Casa (ni night club), is very nice place kwa wanaopenda kujirusha mkuu!
Kama unapenda nyama choma...ha!ha!ha! nenda pale Ze City Hotel.....mwisho wa matatizo, kuna Mchaga mmoja pale anachoma Kuku, mbuzi, ng'ombe sijawahi ona aisee! Please usisahau...pale kuna SUPU ya pweza sio kama ile inauzwa dar barabarani no iko kny very good quality!
Kama ni mpenzi wa Samaki usisahau kutembelea kule Deep sea wenyewe wanakuita....acha kabisa!
Need wa say more mkuu!