LGE2024 Wenyeviti na Wajumbe 1,953 wa Manispaa wala kiapo cha Uadilifu baada ya kushinda Uchaguzi

LGE2024 Wenyeviti na Wajumbe 1,953 wa Manispaa wala kiapo cha Uadilifu baada ya kushinda Uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Jumla ya wenyeviti na wajumbe 1953 leo Novemba 28.2024 wameongozwa kula kiapo cha uaminifu na uadilifu na Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Illuminata Lutakana mara baada ya viongozi hao kushinda uchaguzi uliofanyika Novemva 27 mwaka huu.

Akizungumza baada ya zoezi la hilo liliofanyika katika Ukumbi wa Donkey Hall Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva amewataka Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji, na Wajumbe wa Serikali za mitaa na Vijij kufanya kazi kwa uadilifu na uzalendo katika kuwatumikia wananchi ili kuleta maendeleo katika maeneo yao.

Soma Pia: Lindi: Matukio yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024


Mwanziva amesema viongozi hao ndio wanakutana na wananchi na kugundua changamoto zao hivyo wanapaswa kushughulika na mambo ya wananchi waliokuchagua bila kujali itikadi za vyama na dini zao.

Naye Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Juma Mnwele amewapongeza viongozi hao kuaminiwa na kuchaguliwa na kuwataka kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, hasa kuepuka kuingilia majukumu ya kisheria ya vyombo vingine ikiwemo uuzaji wa viwanja.
IMG_1081.jpeg
IMG_1082.jpeg
 
Back
Top Bottom