Wenzangu na mimi tulioaminishwa na kutabiri kifo cha CHADEMA na kuinuliwa kwa NCCR na ACT, mpo?

Wenzangu na mimi tulioaminishwa na kutabiri kifo cha CHADEMA na kuinuliwa kwa NCCR na ACT, mpo?

Fya-fyafya

Member
Joined
May 2, 2019
Posts
43
Reaction score
125
Ndugu,

Sio siri tulio wengi tumejawa mate mdomoni na hatuamini hiki kinachoendelea kwenye mikutano ya chama cha CHADEMA.

Kutokana na Sekeseke kilichopata, Kazi kubwa ya kimaendeleo iliyofanywa na CCM ndani ya muda mfupi, hama hama ya madiwani na wabunge, kukosa wawakilishi wenyeviti wa vijiji na mitaa, mlengo wao juu ya Janga la Corona..., basi wengi tulidhani kwenye mikutano yake ya kampeni chama kingedorola. Kuwa watu wangekuwa wa kuokoteza (wachache mno) ila cha ajabu sivyo ilivyo. Hapa nakumbuka kuwa usilolijua sawa na usiku wa giza na Usione na ukadhani.

CHADEMA kwenye kampeni hizi ndio chama ambacho kinachuana kwa karibu na CCM kwenye mahudhurio ya watu mkutanoni na shamrashamra (tention) ya watu mitaani.

Kwa ujumla, hii ndio Derby ya siasa kwenye kampeni hizi CCM vs CHADEMA. Bado tunaona Lisu akiendelea kuwa na mvuto wa aina yake. Yaani jamaa anakismart awapo jukwaani. Sera yao ya Uhuru, Haki na Maendeleo imeonekana kukonga nyoyo za watu wengi.

Kama tumjuavyo Lisu, ni mtaalamu wa kujenga na kutetea hoja. Sasa kwake si shida kuwaelewesha maelfu ya wanaokula kumsikiliza sera ya Utani yao.

Ukiacha na nafasi ya Uraisi, wabunge na madiwani wanapeperusha chadema nao wana morali na wafuatao wengi sana kiasi kwamba unashindwa kupredict matokeo haraka haraka. Hii haikufahamika hivo kabla ya kampeni.

Vyama ambavyo vilitabiliwa kuwa vyama vikuu vya upinzani (NCCR na ACT) mambo si mazuri kwao. Kama wasipoingia mitini na kukacha kampeni A urais basi wanajitafutia magonjwa ya Presha na Sukari kwa kuumia mioyo juu ya mahudhurio hafifu sana.

Leo hii CHADEMA, chama ambacho wabunge na madiwani wengi walikuja na na kujiunga na vyama vya CCM, NCCR na ACT, kwenye kampeni hizi kinaonekana bado ni imara na pendwa kwa watu.

Kuna wengine wanasikiliza wakisema kuwa mvuto wa CHADEMA kwa sasa ni zaidi ya ule wa uchaguzi wa 201 enzi za Mzee Lowasa. Je, ni kweli?

Wao wanasema kuwa chadema ile ilikuwa imejaa mamruki wengi na kuwafanya hii ya sasa ni ya wnachadema halisi. Je ni kweli?

My take: Kuanzia uchaguzi huu, nimeamini kuwa siasa ni imani na imani haitoki moyoni. Kwani mazishi kuona jinsi gani watu wanavyozidi kujitokeza kwenye kampeni za chama hicho huku wakiwa wamevalia sare za chama kifua mbele. Hii ndoa demokrasia sasa.


Viva Tanzania.
 
[emoji16][emoji16][emoji16]kwahiyo chadema ni chama hai.
 
We ulizani chama ni nini? Chama kiko miyoyoni mwa watu,huezi kufuta kitu kilicho miyoyoni,
 
Walianza kustuka pale walipowafunga viongozi wa cdm au fine kubwa wakastuka ndani ya wiki pesa imelipwa hawakuamini mpaka leo wanajiuliza kisirisiri ilikuaje!!
Wakanunua midege ambayo haina faida wakadhani watz watawaelewa
Wakafunga watu hovyo hovyo ili kuwatisha !!!ahhh wapi!
Wakatumia vyombo vyooooote vya habari aaaaah. Wapi!!!
Wanakodi wanenguaji wasaniii aaaah wapi
Sasa wanafanya kampeni kwa kilugha na vitisho .........ukichagua wapinzani sileti naendeleo.....watu wenye akili wanahoji !!!
Mbona majimbo yaliyo ccm tangu Mungu auumbe huu ulimwengu yapo hoi bin taabani!!!!Mfano Kongwa kwa Ayub ,kwa Nape,nk hawanacmajibu
 
Jiwe pumzi imekata... bila wasanii hawezi jaza hata watu mia..

watanzani wajinga wamebaki wachache sana..
1.Jiwe kafisadi Trillion 1.5
2. Jiwe kajijengea uwanja wa ndege ghetto kwake chattle
3. Jiwe kagoma kupandisha mishahara ya watumishi.
4.Jiwe katoa watumishi kwa jina la vyeti feki ila hao hao wameendelea na kazi taasisi za private.. kwa hiyo issue siyo vyeti issue ni kuwatoa kwenye payroll
5. Kapandisha asilimia za bodi ya mikopo from 8% to 15% kinyume na makubaliano wakati wa kuomba mkopo.
6. hapo hapo kaleta 6% ya ku retain mkopo.. unakopa milion 10 unalipa million 30. hata benki hazipo hivyo.
7. Jiwe kigeu geu... haeleweki ni ndege au mnyama.. ana ndimi mbili.
8. Jiwe alikimbia mapambano dhidi ya corona.. alienda kujificha chattle - akawa anaapishia viongozi kibarazani kwake.
 
Ccm pumzi imekata,wameanza kuwatumia uvccm kutoa vitisho.
Mziki wa CDM wameushindwa,upinzani upo mioyoni/damuni.Haupoi kwa vitisho wala mateso.
Ccm inateswa na mzimu wake wa mateso kwa raia wasio na hatia/vitisho/hali ngumu/kutopandisha madaraja na mishahara/ubabe na ukabila.
Ndege/madaraja/Reli /lami /majengo haisaidii kuwapa kiki,kwani vilikuwepo na vitaendelea kuwepo hata wakiachia madaraka.
28/10/2020 ndio pumzi yenu ya mwisho.
Go Lissu Go!
 
Back
Top Bottom