Wenzetu wanajitahidi kukijua Kiswahili, sisi je?

Hawa vijana wanaigiza kwamba wanagombea uraisi wa Tanzania na kiongozi wa mdahalo anawauliza maswali kwa kiswahili na wanajibu kwa kiswahili. Inaleta raha kwa kweli.

Tiba
 
Uganda washa declare kuwa kiswahili will be their official langauge. Wana uhitaji mkubwa wa walimu. Kiswahili kinakua kwa kasi ya ajabu sana ila itashangaza sana dunia kusikia kuwa Tanzania hawaongei kiswahili fasaha kama Kenya. Subiri uone wakenya watakavyo take advantage
 

Ukiisikiliza hii video mgombea uraisi mwanaume (kijana) eti wamempa jina la Mbowe. Sijui kama wamefanya hivyo kwa kujua siasa za Tanzania zinavyokwenda au ni kwa bahati mbaya tu. Kwa wenzetu Wakenya, wao kiswahili wanakisoma kama sisi tunavyosoma Kiingereza kama somo mojawapo ila sio kama major communication language yao.

Tiba
 


Unaongelea wakenya wapi hao mkuu? Kiswahili fasaha Kenya utakisikia Pwani tu kule Lamu na Mombasa wengine hadi wanaona aibu kuongea kiswahili kwa jinsi walivyo shallow wanapokutana na watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…