Wenzetu wanatumiaje magari?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
8,581
Reaction score
15,618
Unakuta gari imetembea km 80000. Hii gari unakuta ni ya mwaka 2000. Gari ukiiangalia unaiona kama bado mpya. Wakati mwingine mpaka zile karatasi za kwenye seat zipo. Kwa hapa kwetu tunaziita mpya.

Najiuliza maswali mengi sana. Mbona hizi gari ubora wake ni kama hazijatumika? Huyo aliyetumia aliona mapungufu gani mpaka akaamua kuliuza na kununua jingine? Gari za mwaka 2000-2005 zilizotembea km 80,000 zimetumika kwa muda gani mpaka mmiliki anapoamua kuuza? Maana hapa bongo nyingi ya gari zinazouzwa zina umri kati ya miaka 15-20.

Naomba kujua wenzetu matumizi ya magari wanatumiaje gari ya umri mkubwa inaonekana kama jipya.

Cc: RRONDO
 
Wenzetu maisha yao kuanzia miundo mbinu kwa ukubwa ipo sophisticated saana. Barabara, sheria za utumiaji wa vyombo vyenyewe. Car safety care is very strict... ndinga nyingi zinachoka kwa hili.

Chukulia mfano BMX ya mtoto anayeishi masaki na wa vingnguti...zote mpya zichunguze ndani ya 1 Year.

Pia, wenzetu mfano Kwa japan system ya mikopo kwa ununuaji wa magari inayafanya yadumu.

Wengi, let say unakuta gari ni 60m analichukua kwa mkataba wa mkopo kwa 30m kisha baada ya miaka miwili anamuuzia huyohuyo kwa kuuziwa lingine jipya. Hili linawafanya wayatunze saana.

pia watakuwa wanayapimp kabla ya kuyaingiza tena sokoni.
 
Wenzetu kila mtu ana gari lake siyo kubebana mishikaki kama bongo...gari za bongo shuruba nyingi inatoka asubuh imejaza nyomi inapita kwenye makorongo ikifika job unaiweka juani...tangu asubuh hadi saa kumi na moja then unarudi huku umebeba mshikaki wa job mate..unapita mashimo yale yale..
Gari ikiharibika unaipeleka kwa wagonga nyundo...unategemea gari itadumu kwa miaka mingap
 
Ukumbuke kwanza wenzetu hao wanayatengeneza hayo magari,
Hawahitaji kulitumia gari mpaka lichakae.
Pili moundo mbinu yao ni rafiki.
Hata jinsi wanavyoyatunza,service and maintanance.
Vilevile magari kwao ni necesity sio luxury kama sisi.
Na hayo magari kabla hayajauzwa yanapakwa rangi,yanakatabatiwa na kuvishwa hizo plastic kwenye seat pamoja n kubadilisha seat ikibidi.
 
Majibu mazuri. Sasa gari ya umri wa miaka 15 inapokuwa imetembea km 80000 inakuwaje. Hii ni sawa na km 5300 kwa mwaka. Sasa kwa hali ya kawaida km 5300 kwa hapa kwetu ni safari ya miezi kama miwili.
 
Majibu mazuri. Sasa gari ya umri wa miaka 15 inapokuwa imetembea km 80000 inakuwaje. Hii ni sawa na km 5300 kwa mwaka. Sasa kwa hali ya kawaida km 5300 kwa hapa kwetu ni safari ya miezi kama miwili.
Shaken law
Cc RRONDO
 
Sio gari hata watu. Mimi nilivyorudi Ulaya nilikuwa nang'aa kishenzi sasa hivi nimepauka balaa! Mazingira ya barabara,utunzaji ikiwemo matengenezo na huduma, gari inaoshwa kwenye mashine kwa maji na sabuni maalum,inapigwa wax,polish zote zinasaidia kutunza rangi na ustaarabu wa watu unachangia magari kuwa kama yalivyo.
 
Umepauka kwa sababu kutwa nzima unakimbia kimbia na kitimoto!![emoji53][emoji53][emoji53]....Aliekuambia kuwa kitimoto ni chakula ni nani?!
 
Wanazi recondition kabla ya kuzileta Bongo.
 
Ulaya hukuwa na michepuko! (Haaaah! Haaah! Haaah! JAJ - Just a Joke)
 
Kuna mtu alinambia, mifumo ya usafiri Ulaya ni mzuri sana kiasi mtu ana gari yake lakini bado yuko flexible kupanda public transport mf treni ama Metro! Kwamba wao hawamiliki magari kwa sababu kuna Changamoto ya transport, ni kwa sababu gari zipo tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…