Wenzetu wanatumiaje magari?

Nilisoma mahali pia kuwa huko ughaibuni hawasubiri mpaka gari iwe na mapungufu, ikitoka toleo jipya anaenda kubadilisha anaongezea na pesa kidogo anapewa jipya hilo lake la zamani ndio linaletwa huku.
 
Gari zote zinakuwa zimefanyiwa kurudisha nyuma km na wanafanya full service na kupaka tena Rangi
Akupakie rangi halafu BFoward wakuuzie $1000? Huyo mwenye gari anapata chini ya $1000 hio rangi bei gani? Rangi ni ile ile ila mazingira ya wenzetu hayapaushi rangi na gari haikwanguliwo hovyo.
Bongo ukipaki gari unakuta kundi la watu wamekalia,wameegamia wengine wanaweka ndoo za samaki,beseni ya mihogo unafikiri ikikaa mwaka itatamanika?
 
Taja wapi magari yote yanatuka Japani chunguza vizuri yote ni REPAINT MKUU
NA KM WANARUDISHA HATA MIMI NAWEZA KURUDISHA NYUMA KM
 
Taja wapi magari yote yanatuka Japani chunguza vizuri yote ni REPAINT MKUU
NA KM WANARUDISHA HATA MIMI NAWEZA KURUDISHA NYUMA KM
Unaposema YOTE ndio unapokosea. Labda kama lilipata ajali,lakini kwa hali ya kawaida gari huko hazipauki rangi.
Hata habari ya kurudisha KMs SIO YOTE.
 
Mkuu km 5000 miezi miwili unakuwa unaenda wapi..
Kwa mizunguko yangu ya shughuli tu, tena ndani ya km za mraba 15 nafikisha. Kwani mtu anayekaa mbezi mwisho kama anaamua kutumia gari kwenda posta au kariakoo kwa miezi miwili aende na kurudi hafikishi km 5000 kwa miezi miwili?

Nawaza tu.
 
Km 2500 kwa mwezi sawa na km 600+ kwa week sawa na 80+ kwa siku..yah zinaweza fika mkuu..nilikua sijazigawa vzur
 
Majibu mazuri. Sasa gari ya umri wa miaka 15 inapokuwa imetembea km 80000 inakuwaje. Hii ni sawa na km 5300 kwa mwaka. Sasa kwa hali ya kawaida km 5300 kwa hapa kwetu ni safari ya miezi kama miwili.
Kuna baadhi ya magari watu wananunua kwa fashion au seasonal use..pia mengine anakua nalo zaidi ya moja hivyo hata matumizi yake si ya kila siku (assuming haijachezewa odometer)
 
Majibu mazuri. Sasa gari ya umri wa miaka 15 inapokuwa imetembea km 80000 inakuwaje. Hii ni sawa na km 5300 kwa mwaka. Sasa kwa hali ya kawaida km 5300 kwa hapa kwetu ni safari ya miezi kama miwili.
Nadhani wewe utakuwa engineer.
Short and Clear
 
Nadhani ungekuwa umetembelea mojawapo ya nchi za waliostaarabika pengine ungepata majibu mazuri Sana na huenda usingeshangaa. Akili zao ni zao, na akili zetu ni zao ila akili zetu n zetu.
 
Kitu kinachoharibu Magari bongo ni Maji ya chumvi+ tope lake, barabara mbovu, wese lililochakachuliwa, kuhusu kukwanguliwa rangi, maguta na bodaboda ni adhabu kwangu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…