WESTGATE MASSACRE: 41 YEARS KENYA's STILL BEHIND

WESTGATE MASSACRE: 41 YEARS KENYA's STILL BEHIND


hivi walishindwa nini kuzima umeme usiku na kuiacha Mall iwe giza ili waingie na silaha huku wakiwa wamevaa night vision goggles au heat vision goggles

huku waki
move, five meter spread, no sound. double pack, heads up

U are exactly on my shoes.!!!!!!!!!
 
Nilikiri ni mimi tu nilikuwa najiuliza vile vifaru na magari ya Deraya ni vya nini? Yale magari ya Kivita yalienda kufanya nini pale wakati hata bastola tu zilikuwa zinatosha kuokoa watu kwa well trained and skilled task force lakini swali la msingi ni je sisi tunao ujuzi huo? Au likitokea la kutokea hata Kenya watakuwa na Afadhali sipati picha jinsi Kova atakavyoshinda mbele ya Kamera akitafuta sifa

sisi ndo itakuwa balaa maana unaweza ambiwa magari hayana mafuta au mpaka tupitishe michango kwanza
 
Kova anapenda sana kuuza nyago ktk tv siombei lakini nyie subirini.
Vijana wake anaowasifia wanapenda bia na viroba kuliko kitu chochote wakati hii shuhuli ikitokea unatakiwa ujikane uangalie maisha ya watu wengine akiwa salama!
 
Kova anapenda sana kuuza nyago ktk tv siombei lakini nyie subirini.
Vijana wake anaowasifia wanapenda bia na viroba kuliko kitu chochote wakati hii shuhuli ikitokea unatakiwa ujikane uangalie maisha ya watu wengine akiwa salama!

Hahahaaaa eti wanapenda Viroba inawezekana wanafuata nyayo za bosi wao Kova akiongea ukimwangalia vizuri machoni unaweza hisi kabisa ni viroba ndo vinaongea mzee wa Media yule 2015 lazima agombee ubunge
 
Naumia pamoja na waloumia wengine ila ukweli lazima usemwe. Kenya, i mean NIS in particular failed to strategize on this na ndo maana walikuwa caught off guard. Imagine naambiwa inawezekana magaidi walitorokea kwenye mfereji wa maji machafu (according to NTV's speculations) wakati KDF wakiwa busy kwenye media. Nilidhani walipaswa kusoma masterplan nzima ya Westgate ili kuziba namna yoyote ya kutorokea but hili halikufanyika zaidi ya kuwa hewani na helcopters ambazo hazikusaidia. Na kuziba barabara as if gaidi angekuwa mjinga kiasi cha kuwalk out majestically.

On this Kenya ilipigwa ngumi za usoni. But kubwa zaidi ni kwa jirani (TZ in particular) kujifunza na kuzuia kitu kama hiki kisitokee. Tupeane pole lakini ukweli tuuseme!

True Jamii Intelligence!

Its sad kwa kweli magaidi walishafanya yao zamani wao hata kuingia wanaogopa wanaishia kusema eti magaidi wamejificha kwenye CINEMAS! what a shame
 
Kova anapenda sana kuuza nyago ktk tv siombei lakini nyie subirini.
Vijana wake anaowasifia wanapenda bia na viroba kuliko kitu chochote wakati hii shuhuli ikitokea unatakiwa ujikane uangalie maisha ya watu wengine akiwa salama!

Nasikia kova huwa ananunua mapanga kariakoo anaita media ije anapiga picha tumekamata majambia 50
 
...meya wa jiji la nairobi alipewa taarifa hizi na mmama mmoja siku kadhaa nyuma kuwapo kwa ulipuwaji wa malls kadhaa (maana mtoa taarifa hakujua ni mall ipi)....! ..meya naye alijaribu mara nyingi kuripoti hizi habari kwa sehemu husika...lakini wapi...alipuuziwa tu!

kuna wakati huwa sielewagi hivi vyombo vya usalama huwa vinataka taarifa zipi au kutoka kwa nani ili wazifanyie kazi! kama mnakumbuka ulipuwaji wa balozi za usa nchini tz na kenya...taarifa za awali zilikuwapo..... mfano mtu aliekuja na taxi akawa anarekodi jengo la ubalozi wa usa siku chache kabla ya huo mlipuko....nk!

hapa kwetu tunajua woote, namna gani wasomali wanaingia nchini....na sio siri kuwa, makao yao makuu ni wailaya ya temeke ijapo sasa wameanza kuenea sehemu mbalimbali nchini!...kule temeke kuna nyumba moja niliona wasomali (wamefungiwa hawajui kiswahili hata kidgo) wapo kama 30 hivi....nadhani walikuwa transit pengine....taarifa zikaripotiwa......!
 
bwana Mossad sikuona Snipers waki pinpoint targets
vip inawezekana katika mission kama hizi kusiwe na snipers??

Lazima wawepo.. lakini inapokua siege km ile yenye magaidi wengi katika sorrounding iliyojificha bas snipers wanakua of less priority kinacho fikiriwa sana ni ambush tu km alivyosema CTU! Ukishakua na magaid weng sio preferable kutumia snipers cz hata wao wanajua watakua targeted so hawatatulia sehemu moja na ukimpiga mmoja unawaweka mateka rehani.
 
It was this dude sir mimi nilifikiri ni Polisi kumbe raia tu kajitolea na bastola yake na kaokoa watu wengi tu kuliko hata hao KDF wenyewe


Na hii hapo juu ni weakness nyingine inamaanisha Al Shaabab wangeweza kuingia pale ndani tena na kuua zaidi.

Au imagine huyo jamaa angekuwa Al Shaabab

Inamaana hakukuwa na control ya movements wao walibobea kwenye kupiga picha na CNN tu.

Ndio matatizo ya kuchagua wakuu wa usalama kwa kutumia TV eti mkuu polisi anafanyiwa interview!
 
Jamaa kaelezea vizuri
Nilipoangalia hiyo case ya Kenya nilijikuta naishiwa pozi. Jamaa s ijui ni ujinga au maana aina ya silaha, movements zao, na hata mbinu zilikuwa very poor.
Jeshi la Kenya bado sana
 
Mkuu mossad007 heshima mbele kwa uchambuzi mzuri ILA naomba nitofautiane na wewe katika haya

-1. Katika ile assault zilishiriki unit mbalimbali za ulinzi Kenya. Maroon Commandos walikua ni sehemu tu, kulikua na jamaa wa 20 Parachute Battalion,30 Special Forces (30SF) na 40 Rangers Strike Force (RSF) na unaposema kuwa walikua na M16 si kweli. kenya Rangers standard issue ndio M16 ila pale tumeoshuhudia mpaka SCAR wakiwa nazo jamaa wa 30regiment.

-2.Kwa mtazamo wangu ni kuwa tatizo kubwa la hii disaster ni kukosekana clear command na coordination which implies lack of training. Hilo tu ndio tatizo la waKenya na sio kuhusu tools. Katika vifaa tu they are verry well kitted, pengine kuliko operators wowote Kusini mwa Sahara.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mossad007 heshima mbele kwa uchambuzi mzuri ILA naomba nitofautiane na wewe katika haya

-1. Katika ile assault zilishiriki unit mbalimbali za ulinzi Kenya. Maroon Commandos walikua ni sehemu tu, kulikua na jamaa wa 20 Parachute Battalion,30 Special Forces (30SF) na 40 Rangers Strike Force (RSF) na unaposema kuwa walikua na M16 si kweli. kenya Rangers standard issue ndio M16 ila pale tumeoshuhudia mpaka SCAR wakiwa nazo jamaa wa 30regiment.

-2.Kwa mtazamo wangu ni kuwa tatizo kubwa la hii disaster ni kukosekana clear command na coordination which implies lack of training. Hilo tu ndio tatizo la waKenya na sio kuhusu tools. Katika vifaa tu they are verry well kitted, pengine kuliko operators wowote Kusini mwa Sahara.

Gobore umesema vzur kuhusu inclusion ya unit nyingne ingawa hao hawakua focus yangu na nilifahamu uwepo wao na sio hao tu uliowataja walikuwepo mpka GRU para military police, NIS, etc. tho kama utakua na uelewa mzuri SCAR rifle ni dizaini ile ile ya family kama za Kalashinikov, M16, na nyingnezo wala huwez kuiweka kwenye group la Mini Assault hivyo Manurvebility yake bado sio rahisi wala nyepesi ukicompare na kitu kama MP5.. Na binafsi sikusema kua kenya hawana vifaa kama utakua umefocus vzur mchango wangu ulikua kwenye tactics to be employed cz kama ni issue ya vifaa basi Ujerumani wanavyo vya kisasa na first class zaidi ila walichemka kwenye tactics in Munich Siege 1972.. My focus kwenye Maroon ndio ilikua basis cz ndio nilioshuhudia kwenye televishen wakiwa na M16 na pia hawa ndio the Most Kenya's Elite Force Unit over the entire State forces kuanzia mafunzo, treatment na hata payment sasa kama wao ndio first class VIP's any fault kama hiyo lazima wadau km mimi na wengineo tuitolee macho.
Kwa mchango wako wa pili naungana na ww 100%..
 
Last edited by a moderator:
Kenya always tunawaambia wako well equipped but with very poor training.
Pamoja na madhaifu yetu lakini issue serious kama ile tungewashughulikia hadi wasifikirie tena kujaribu.
 
Nilidhani baada ya Miaka takribani 41 since makosa yaliyofanyika baada ya matokeo ya Ugaidi kule Munich 1972 kwenye Winter Olympic Games Kenya watakua wamejifunza namna ya kukabiliana na ugaidi lakini wenzetu bado sana.

Kuna vipengele vichache ambavyo Ujerumani ilivikosea na kusababisha Wanariadha 11 wa Kiisrael kupoteza maisha na leo nashuhudia Kenya wakirudia kitu kile kile.

1. Role of Media Coverage

Kutokana na kukua kwa Uhuru wa Habari kwa wenzetu ( Europe ) baada tu Kikundi cha Black September kuwateka wanamichezo wa kiisrael media zilifurika nje ya Apartment waliyotekwa na kuanza kuripoti mwenendo mzima wa tukio. Ndani ya zile apartment kulikua na tv ambazo wale magaidi walikua wanaona na kufuatilia kila kitu. Matokeo yake Rescue Mission ya kwanza iliyopangwa na Polisi (hawakua na counter terrorism unit kipindi hicho) ikawa inapigwa picha live na wale magaidi wanona ni nini kinaendelea.

Ilikuwa kichekesho sababu magaidi waliweza kujua polisi wako wapi na wanafanya nini kwa kupitia tv zao ndani. Mission was aborted baada ya polisi kuona asilimia za ushindi kua chache. Leo wakenya wanafanya kitu kile kile updates zote ziko on air na kwa mujibu wa mashuhuda westgate complex ina dozens of tv sets ni km pale Mliman city tu unapoingia Game!

2. Rescue Team

Kikosi kilichopelekwa kufanya Rescue kinatoka KDF: Maroon Commandos (counter terrorism Unit) ukisoma Article moja online ya hawa jamaa wamesifiwa sana kua ni total replica ya their counterparts the likes of Sayeret Matkal (israel), NAVY SEALS (USA) and SAS (UK) cz huko ndiko wanako watrain. Lakini honestly speaking hawa jamaa wako nyuma kuliko ilivyosemwa cz kwa mission km hizi choice of weapons ina matter sana.

Counter terrorism zote ndani ya majengo au vehicles including ndege hufanywa kwa priority ya Mini Assault Rifles refer operation Entebe, Spring of Youth, Air Sabena (Sayeret Matkal), Operation Barras, Iran Embassy Siege (SAS) na Operation Bin Laden, (SEALS). Mini assault rifles hapa nazungumzia the likes of Heckler and Kotch, Uzi, Mini Galil, AK-74 folding etc. Ambazo ni ndogo, fupi, hubebeka kirahisi na zina range ile ile ya Weapons za kawaida hutumika pia na Makomandoo wa JWTZ km ilivyoonekana juzi Goma na kipindi cha miaka 50 ya Uhuru pale Taifa.

Lakini nimeshangaa kuwaona KDF: Maroon Commandos wakiwa wamebeba mitutu mirefu, mizito ya M 16 na zile Ranger Rifles za kiingereza tena za kizamani kwenye mission inayowalazimu wepesi na tacktics... its so absurd. Moja kati ya vitu vilivyotolewa duku duku na kamati maalum iliyoundwa after failure in Munich Massacre ilikua ni choice of weapons baada ya Polisi wa kijerumani kutumia Rifles kubwa zinazo punguza Manurvability and accuracy na kuundwa kwa special counter terror unit.

Kwa waliopitia mafunzo watakubaliana na mimi kua Counter Terror Rescue Mission ni zaid ya Uwanja wa Vita cz huokoi maisha yako tu bali na ya mateka na mali. Hivyo SPEED, ACCURACY and TIME are key elements. Ukimkosa gaidi kwa risasi moja analipua jengo zima ni matter of seconds tu ila vitani unaweza ukamimina ile Minimi mpka mkanda ukaisha na bado usiue mtu ukawa hai na wala wewe usife mkatupiana njugu mwezi mzima lakini hii sio sawa kbsa kwenye Rescue Missions ndio maana Choice ya Weapon hata mtu wa kuifanya hiyo kazi inamata sana... nilidhani leo wakenya watakua wamejifunza.

Mwisho kwa yaliyotokea Kenya hata TZ yaweza tokea hivyo tuwe makini na Siasa zetu za Kimataifa na kuboresha Ulinzi katika nyanja zote.

POLE ZANGU KWA WAHANGA!

Ndio maana naipenda sana jf! Ahsante sana mkuu umetupa vitu adimu sana hivi, nashauri jwtz,polisi, na inteligencia yetu ikupe ushirikiano uweze kuwapa mafunzo haraka sana kwa sababu hawa jamaa wameshatangaza tz we are next
 
Ndio maana naipenda sana jf! Ahsante sana mkuu umetupa vitu adimu sana hivi, nashauri jwtz,polisi, na inteligencia yetu ikupe ushirikiano uweze kuwapa mafunzo haraka sana kwa sababu hawa jamaa wameshatangaza tz we are next

Hata mimi aisee nimepata vitu vizito kwenye hii thread.. na katika hili hata kuna msemaji wa alshabaaab alisema kuwa majeshi ya kenya ni DHAIFU
 
Nime enjoy sana kusoma hii thread. Nilihisi naangalia 24 series. Nimejifunza mnoo.
 
It was this dude sir mimi nilifikiri ni Polisi kumbe raia tu kajitolea na bastola yake na kaokoa watu wengi tu kuliko hata hao KDF wenyewe


Kuna video anaonekana yupo na polisi kwenye kona ya korido,the way alivyokuwa akim-cover askari na movement kati yake na polisi anaonekana ana mafunzo.
huyu ni NIS,offcoz kajisema raia wa kawaida sababu mashushushu hawajitangazi.

Back to Topic:nilishuhudia kupitia BBC, kdf wawili wakiwa floor ya juu wakikimbia then wakarusha kama grunet ghorofa ya chini,wakalala,bomu likalipuka.nilipatwa na wasiwasi walichofanya unless walikua wakifanya clearance

unajua kati ya KDF walokufa wawili were very juniors mmoja akiwa ametoka vitani somalia na mwingine ndio alikuwa amepangwa kwenda Somalia.KENYA FORCES hawakuzamisha makomandoo mle ndani!ni kama walikuwa na mashaka na walikua wakijaribu tu
 
Ndio maana naipenda sana jf! Ahsante sana mkuu umetupa vitu adimu sana hivi, nashauri jwtz,polisi, na inteligencia yetu ikupe ushirikiano uweze kuwapa mafunzo haraka sana kwa sababu hawa jamaa wameshatangaza tz we are next

Unachekesha huyu mwanzisha mada kafundishwa na hao unaotaka awafundishe!!
Unaijua nchi yako vizuri? uliza makaburu,wareno na vibaraka wao wakwambie!!
 
Back
Top Bottom