King Josse
Member
- Dec 25, 2016
- 25
- 9
Naomba kufahamishwa vizuri kuhusu hii kitu ya Westphalian kuanzia mwaka na mafanikio gani waliyapataa na inatusaidiaa vipi wakati huu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asantee sanaa sanaaMkataba wa Westphalia ulisaniwa mwaka 1648 baada ya vita ya miaka thelathini (Thirty Years War) huko barani Ulaya baina ya Waprotestani na Wakatoliki. Vita ilianza baada ya dola la Roma Takatifu (Holy Roman Empire) kutaka kulazimisha majimbo yote yaliyoko chini yake yawe ni wakatoliki.
Ikumbukwe kipindi hiki, dini na siasa vilikuwa bado havijatenganishwa: Watawala wengi Ulaya walitawala kwa kupitia mamlaka ya kimungu (Divine Right). Kikubwa zaidi ni kwamba kama mfalme hauko chini ya kanisa Katoliki na Papa basi ni lazima uhesabiwe kama kafiri na mzushi (A Heretic). Hivyo ili mfalme utawale ilikuwa ni lazima uwe Mkatoliki na ufuate kile ambacho kanisa linasema.
Baada ya wakatoliki na waprotestanti kuchinjana kwa muda mrefu zikiongozwa na familia mbili za kifalme zilikuwa zinashindania madaraka (The Habsburg VS The Bourbons), waliamua kukusanyana wote ili kusitisha vita. Makubaliano yalikuwa magumu kwasababu kuna baadhi ya viongozi wa kanisa Katoliki kama Kadinali Richelieu hawakuyataka. Lakini kwasababu hawakuwa na namna yoyote ile, hasa baada ya kushuhudia watu zaidi ya milioni 8 wamekufa kwa njaa na magonjwa ikabidi wakubali kukaa mezani.
Mambo waliyokubaliana ni haya:
1. Kila taifa lina uhuru wa kujiongoza lenyewe bila kupangiwa na kanisa au mfalme yoyote yule. (Sovereignty)
2. Kila taifa lina uhuru wa kuchagua dini ambayo linahisi ndiyo itakuwa dini ya taifa.
3. Kuwatambua rasmi waprotestanti kama dhehebu halali lenye hadhi sawa na wakatoliki.
Leo hii sisi tunajifunza mambo yafuatayo:
1. Kwanza kabisa, mkataba huu ndiyo uliotupa kanuni ya nchi kujitawala na kuwa na mamlaka yake kamili (Sovereignty)
2. Dini na Siasa havitakiwi kabisa kuunganishwa katika utawala, madhara yake huwa ni makubwa mno.
3. Ukiwaonea sana watu na kuwanyanyasa kwa muda mrefu kuna siku tu lazima watafanya uasi na kuleta matatizo.
Yeees tenaa vzurii sanaa