Wewe dada mwenye nywele ndefu halafu una ndugu Mwanza nimejua ulikuwa unaniongopea?

Wewe dada mwenye nywele ndefu halafu una ndugu Mwanza nimejua ulikuwa unaniongopea?

Mkogoti

TAPELI Mkubwa
Joined
May 3, 2020
Posts
2,415
Reaction score
3,924
Story ipo hivi huyo dada nilikutana naye pande flani hivi maeneo ya Sokoni ilikuwa Jumapili jioni, nikamwomba namba akanitoa kiroho safi. Mahusiano yetu yakaanza tumekaa kama miezi mitatu kama sikosei.

Sikuwa namtafuta maana namba yake ilikuwa haipatikani mpaka nikaona ngoja nitulie kwanza, ila juma moja nikaamua niende nimtafutie kule maeneo ya kwao.

Kumbe hata kule nilipokuwa namsindikiza kwenda kwao kumbe alikuwa ananichora tu, kiukweli nilikuwa naishia njiani sikuwa namuona anapoingilia basi akiona nimerudi anapitia njia nyingine tofauti ndo anaenda kwao, mtoto mbaya sana yule😞

Okey kama week hii nimeelekezwa kwao nimefika kumbe pale alipokuwa anakaa walikuwa wanakaa wawili tu na rafiki ake! Pia, jina aliloniambia ni jina la rafiki ake na sio lake balaaa🤕

Kingine rafiki yake anasema yeye huyo hayupo kashaenda Mwanza, akaniuliza mimi ndo nilimnunulia kanga na kikoi cha kimasai. Duh! Hapo nikaona kichwa kinauma napepesuka nataka kuanguka, haaaa haaa😂

Nikajua ooh kumbe🤔 sikuwa nahudumia peke yangu😞 ila mi shida yangu ni kwanini anidanganye hadi jina na sehemu anayoishi wakati nilikuwa mtu mwema kwake?
 
Mkuu chai yako haijaiva vizuri na sukari umezidisha, mfano hapo juu unasema umekutana nae sokoni akakupa namba na mwishoni chai yako inasema mambo ya kuhudumia.

Je ulikutana na mtu barabaran siku ya kwanza tuu ukaanza na kumnunulia kikoi au niuchawi wa ccm unakufanya ushindwe hata kupangilia chai yako vizuri
 
Mkuu hujaelewa ni hivi nilipoenda kumuulizia kwao ambapo nilielekezwa ndo nikaambiwa hayo maneno lakini skuwa mimi nilienunua hivyo vitu, yule dada niliemkuta alijua mi ndo nilinunua na tulikaa kimahusiano kama miezi 3
 
alikupa namba mahusiano yakaanza ila ulikua humpigii sababu namba ilikua haipatikani..... WTF!

Capo Dei Capi
Oke tulikuwa tunawasiliana kama miezi hivi lakini ghafla namba haikupatika tena ndo mimi kuona nimtafute Pande za Maeneo ya kule kwao nilipokuwa namsindikiza
 
Akili kumkichwa.. Huyo ni muuzaji acha kuumiza kichwa dogo!
 
Back
Top Bottom