Wewe ndio Mfalme wa story yako hapa Duniani

Wewe ndio Mfalme wa story yako hapa Duniani

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
WEWE NDIO MFALME WA STORY YAKO HAPA DUNIANI

: Hapa Duniani unavyoishi Tambua,wewe ndio kiongozi wa story yako😎
Na story yako inaandikwa na wewe mwenyewe maana,ndiye mwenye ufahamu wa halisi wa hali na mapito yako😎
Wengine wote ni wapenzi watazamaji,na wengine ni wapenzi waburudikaji,na wengine ni wapenzi wanufaikaji🥸 kama familia n.k.

: Ukiwa kama kiongozi wa Safari yako🥵🥵 basi zingatia mwenye jukumu halisi la kukamata kalamu wakati unaandika na kuithibitisha historia yako,basi awe ni wewe,usithubutu kumkabidhi mtu mwingine kalamu yako,,,aandike kwenye maisha yako,
Maana hataandika upendavyo wewe atakuchafua,
Mwingine hata kukudhalilisha,
Ilimradi tu umempa uhuru wa kushika kalamu,na kuandika
Habari yako.

KATIKA NYAKATI ZA KUSHINDWA

: Kushindwa kutakupa machaguzi (option) mbili

1: Ni ukubali kushindwa ubakie hapo hapo chini,na watu wafurahie kama maadui na wengine wasikitike kama wanandugu,na marafiki wema.😎

2: Ama uinuke upambane tena na kisha usonge kifua mbele kama mshindi,shujaa,hodari
Jamii ikupatie makofi ya shangwe,na wanafiki wajifiche kwa furaha za uongo huku mioyo yao ikiogopa ukuu wako
Na utukufu...😎😎😎

USIUMIE SHIDA IKO KWAKO😎

: Kwanini unawapigia simu mara ya 1,2,3,4,5 hawapokei,?
: Kwanini unawatumia jumbe (Sms) hawakujibu?
: Kwanini ukiwaulizia wanakukwepa? Hata kama wapo utapewa taarifa kua hawapo?
: Kwanini niwewe tu ndio mwenye mdomo na nguvu ya kujisifu mbele za watu kua watu fulani,ni rafiki yako,ni mpenzi wako,ni baba watoto wako,ni ndugu yako? Lakini
Wao hawana ujasiri wa kukutangaza hata kwa mjumbe wa nyumba kumi kua wanajuana na wewe.
Hawana nguvu ya kukusemea mazuri,
Hawana nguvu ya kujivunia uwepo wako.

Shida iko kwako kwasababu moyo wako umeufanya uamini ya kwamba furaha yako,imeshikiliwa na wao,
Yaani huwezi kuhang out bila wao,
Yaani huwezi kucheka bila sms ya mpenzi umpendae.
Tambua hili ya kwamba wewe huna thamani yoyote kwao.
Kubali hilo kwanza😊😎
Kisha rudi nyuma kabisa,jipe thamani akili yako,
Uamini moyo wako,kila changamoto inayokuja mbele yako.
Amini imo ndani ya uwezo wako.
Hata ukitengwa na wote amini ya kua wewe ndio mfalme mwenye
Nguvu kwenye maisha yako.

Rudi tena chini kabisa ulipo msingi wa maisha yako,
Mwambie MUNGU wako ndani yako,kua haupo duniani kwa makosa
Wala kwa bahati mbaya hata kama kuna sauti za walimwengu wanakuita mtoto haram.😎
Huo msingi wa uhai wako(MUNGU), ufanye kua ni kama upinde jiegeshe kama mshale hapo.
Kisha mwambie akufyatue tena...😎😎😎

: Nakuhakikishia spidi utakayo fyatuka nayo kuna mambo kadhaa yatatokea.
1: waliokupuuza utaona wanaanza kuzungumza maneno maneno
Kama skuizi kajipata anaringa.
Ameanza kua mchawi.
Utageuziwa wewe kibao kua umejitenga wakati walikutenga wao.😎
Lakini hilo lisikuyumbishe maana ushafyatuliwa...na ikiwezekana
Kwa kasi uliyonayo atakae kaa vibaya mbele yako usimkwepe chana utumbo songa.😎

2: Wale wanawake\wanaume na takataka zozote ulizoziuzia hisia zako wakazipigia mnada huko wanakojua...
Hao usiwakaribishe😎
Maana mafanikio yako hayawezi kuitambulisha thamani yako halisi.
Kama simu yako haikupokelewa wakati wa dhiki zako.
Kwanini ya kwako iite wakati umetulia na kujipata...😎😎😎

3: Fika kwenye Target yako kabisa huko nako ndiko utakutana na watu ambao ndio sahihi
Wa kucheka nao,kula nao,kuwinda nao sambamba
Maana hao ndio wanaokuheshimu.
Hao ndio wasiokujua utafanikiwa nao.

HITIMISHO
Usikatishwe tamaa na jaribu lolote kwani hilo
Ndio fuel,ndio gas ya kukufanya ukimbie mbali zaidi.
Ahsante.
 
Niliwahi tazama sinema moja ya Finland inaitwa SISU japo matukio mengi sana mule tunasema yamekaa katika hali isiyo yenye uhalisia ila kwakuitaza nilipenda kujua neno SISU ipi maana yake.

Nikakutana na kitu kama hichi:

Neno "Sisu" linatoka katika lugha ya Kifini (Finnish) na lina maana yenye mizizi ya kina katika utamaduni wa Wafinlandi. Linarejelea mchanganyiko wa sifa kama:

1. Uvumilivu wa hali ya juu - Uwezo wa kustahimili changamoto ngumu bila kujali hali.

2. Nidhamu ya ndani - Msukumo wa ndani wa kuendelea mbele hata pale unapokutana na vikwazo.

3. Ujasiri na ushupavu - Nguvu ya kuendelea na kufanya maamuzi magumu bila kusitasita.

4. Uwezo wa kushinda hali mbaya - Dhamira ya kudumu hata wakati matumaini yanapokuwa madogo.

Kwa kifupi, "sisu" ni falsafa ya maisha inayohimiza kutovunjika moyo, uthabiti wa kiakili na kimwili, na msimamo wa kudumu hata unapokutana na changamoto ngumu zaidi. Ni dhana inayotambua umuhimu wa kutokata tamaa na kujitahidi kufanikisha malengo.

HIVYO NI KWELI HISTORIA YAKO UNAIANDIKA WEWE .. 🤝🤝👊
 
Ukishaona mambo yameharibika usiyatengeneze yawe sawa!

Yaache yaharibike kabisa ,usirudishe nyuma wakati coz kuharibika ndio kujongea Kwa wakati!

Kubali yameharibika halafu ingia mzigoni Mwambie Maanani Kwa msisitizo hasta kutoa sadaka kwamba "simtaki Tena" nipatie mwingine coz nyakati zimeisha Kwa huyu!!

Kwamsisitizo Mwambie "Kwa nguvu ya sadaka ninazokutolea Eeeh yesu naomba uniondolee huyu kwenye mfumo was kiroho,kimwili,kinafsi ,kimoyo ,kimawazo yaani mfute kana kwamba sijawahi muona""

Utashangaa kabisa huo wepesi utakaouona baada ya kuomba hivyo kimya kimya!!!

Msaliti hapewi nafasi tena asije akakuua na kukuangamiza Kwa maelekezo ya mabazazi wake!!!
 
Usijibizane maneno mengi na adui yako,
Kwenye majibizano wewe utakwepo
Uwepo wako utampa Nguvu adui yako
Atasoma hisia zako Atajua wewe unajisikiaje
Hii itampa adui Nguvu ya kukuumiza
Adui atatimiza malengo yake kwa msaada kutoka kwako
 
Back
Top Bottom