Wewe ndo unaye penda...wengine wanasema....umpendaye lazima awe hivi.

Wewe ndo unaye penda...wengine wanasema....umpendaye lazima awe hivi.

fazaa

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2009
Posts
2,984
Reaction score
1,031
Hello people,

Kuna mambo mengi sana yanatokea duniani kuhusu wewe na unaye mpenda, na watu wanajaribu kukosoa sehemu unayo penda.


Huu ni mmoja wa mifano na mifano iko mingi sana.

Mfano wewe umependa au umependwa, sa umpendaye anaweza kuwa anavaa vinguo kama vile vi short trousers lakini anatabia nzuri sana, yani hana upumbafu wa aina yoyote ile zaidi ya kupenda tu kuvaa vi short trousers.

Sa chukulia unakutana na rafiki zako njiani au family yako wanasema huyo mwanamke/mwanaume ni good choise yani potential future wife/husband....Matatizo yake madogo tu anavaa vi short trousers inabidi uwachane naye kama hataki kuwacha kuvaa hivyo vi short trousers, je utawasikiliza hao jamaa au utaendelea na life yako kama kawaida..

Na wakati unataka kubadili tabia ya umpendaye lazima ujuwe kuna mambo mawili....Umpendaye atakuchukia kwa kuwa una sikiliza maneno ya watu, au atakuona huna msimamo kwa umpendaye, yani unajali ya watu kuliko yake.

Si mnajua dunia hii kuna kelele nyingi, hata kiziwi kuna wakati wanasikia lakini hamjui tu.

Haya jirusheni ndani ya thread na mawazo yenu, kama wewe utachukua uamuzi gani.
 
Kwanini msikie maneno ya watu? kama mnapendana unamueleza mwenzio kama jambo nguo fupi sio nzuri kwa sababu 1,2,3
na kama muelewa ataelewa hao watu wanahusu nini kwenye mapenzi yetu?mie mtu akinambia eti watu wanasema sasa ili wasiseme fanya hivi na vile hapo ntakua sikuelewi sababu sifanyi mtu nakufanyia wewe mboni ya macho yangu ....
 
fanya kile kitu roho inapenda baba....maneneo ya watu sumuuu
 
Hao watu ndio wanaomjua au ni wewe unayemjua yule umpendae
Kwani kuvaa nguo ambazo ni ndefu ndio dhana kuwa huyu ni bora
Mkuu umpendaye ndie utakayekaa nae au utayeanza maisha na yeye na wewe ndio unamjua ni aina gani ya mtu
Hao watu wanaweza kupiga kelele au kuongea mengi ila wewe ndiye mwamuzi wa nini unatakiwa kufanya
Uchaguzi ni wako kuwasikiliza hao watu wa nje au kukaa na yule ambaye moyo wako umemchagua
 
watu wacha waseme tu, wanajuaje kama nimempenda binti na ninapenda jinsi short trauzaz na minisketiz zinavyomtoa bomba
 
Ni kuachana nao 2! Mi wamesema wamechoka nashukuru mungu hny wangu ana mcmamo nami. Alichofanya ni kuziba mackio.
 
Back
Top Bottom